Posts

Watoto wa Manara, Baba Levo watoboa matokeo Kidato cha Nne

Image
  Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2023, yakionyesha kuongezeka kwa ufaulu wa watahiniwa kwa asilimia 0.87 na ufaulu wa hisabati ukipanda kuliko masomo yote. Mbali na kuongeza kwa kiwango cha ufaulu, ubora wa ufaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu nacho kimeongezeka kwa asilimia 0.47 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2022. Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed amesema asilimia 37.42 ya watahiniwa wamepata daraja la kwanza hadi la tatu ikilinganishwa na asilimia 36.95 waliopata madaraja hayo mwaka 2022. “Jumla ya watahiniwa wa shule 471,427 kati ya 527,576 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 89.36 wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza hadi la nne. Waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ni asilimia 37.42,” amesema Dk Mohamed. Kwenye matokeo hayo wapo watoto wa watu maarufu akiwemo Msemaji wa Yanga, Haji Manara ambaye kupitia mtandao wa I

Mwakinyo: Mpinzani Wangu Asipotokea Nitazichapa na Promota

Image
Bondia namba moja Tanzania, amewatoa shaka mashabiki wa ngumi kuwa pambano lake litapigwa na kuahidi kuwaonyesha uwezo na kutoa burudani. Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Mbiya Kanku wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika pambano la mtata mtatuzi litakalopigwa Januari 27, 2024 katika Uwanja wa ndani wa New Amaan Visiwani Zanzibar. Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa huenda pambano hilo lililopewa jina la 'Mtata Mtatuzi' likavunjika tena, kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa na nia mbaya humtumia ujumbe mpinzani wake wakimtaka asipigane ili pambano hilo livunjike. Akizungumza na Wanahabari leo Januari 25,2024 bandarini Jijini Dar es Salaam wakati akijiandaa na safari visiwa vya Karafuu (ZANZIBAR) Mwakinyo amesema amejipanga kuonesha mchezo ambao wengi hawajahi kuuona huku, akiahidi kutoa burudani kwa mashabiki wake. “Mpaka sasa kila kitu kipo katika ubora kuelekea pambano langu. Lakini kuna changamoto kidogo kwa upande wa promota n

Kocha Benchikha wa Simba Kwenda Timu ya Taifa ya Algeria

Image
Kocha wa Simba SC Abdelhak Benchikha ni moja ya makocha wanaopewa nafasi ya kwenda kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Algeria. Kocha huyo raia wa Algeria anapewa nafasi hiyo baada ya Tetesi zinazoeleza kuwa Kocha Mkuu wa Algeria Djamal Belmad anataka kujiweka kando na timu hiyo. Benchikha anatajwa kutokana na mafanikio aliyoyapata akiwa na USM Alger mwaka jana Kwa kutwaa Kombe la Shirikisho na CAF Super Cup. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/afCmXdh via IFTTT

Kocha Afcon amng'oa Bacca Yanga

Image
MAKOCHA wawili mahiri waliowahi kuifundisha Yanga wameshtushwa na kiwango cha beki wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Ibrahim Bacca kwenye michuano ya Afcon. Na wameshangaa kuona kwanini bado anacheza ligi ya ndani. Kocha Mbelgiji anayeinoa Gambia kwenye Afcon, Tom Saintfiet katika wachezaji wote wa Stars amemuelewa zaidi Bacca kwenye eneo la ulinzi na kutabiri kwamba muda wowote staa huyo atapata ofa Ulaya kwa vile ameonyesha utofauti mkubwa licha ya matokeo ya timu. Saintfiet ambaye aliinoa Yanga mwaka 2012 kwa muda mfupi, alisema Bacca ni beki anayecheza jihadi wakati wote wa mchezo na kwamba kiwango chake kinastahili awe anajiunga na Stars akitokea klabu kubwa Ulaya au nje ya Afrika. Saintfiet ambaye jana usiku timu yake ilikuwa inacheza na Cameroon kukamilisha ratiba kwenye Afcon, amekumbusha kiwango cha beki wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ lakini akakiri mkongwe huyo amezidiwa na Bacca. “Nilikuwa nahesabu wachezaji ambao wanatoka nje ya Tanzania, nilipofika

AFCON : Hizi Hapa Nchi Zilizoingia 16 Bora Michuano ya AFCON

Image
#AFCON2023 Na hawa ndiyo 16 Bora wa fainali hizi!! Je, kuna ambaye hakustahili!!? 27/01/2024 Angola vs Namibia Nigeria vs Cameroon, 28/01/2024 Guinea ya Ikweta vs Guinea, Misri vs Congo DR 29/01/2024 Cape Verde vs Mauritania, Senegal vs Ivory Coast 30/01/2024 Mali vs Burkina Faso Morocco vs Afrika Kusini from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/51sKWbO via IFTTT

Etoo Awachana Wachezaji wa Cameroon 'Wachezaji Waliozaliwa Ulaya Hawana Uzalendo'

Image
  Samuel Eto'o amewachana wachezaji wa Cameroon waliozaliwa ulaya; Wadogo zangu wapendwa naelewa, wengi miongoni mwenu hamjazaliwa Cameroon wala hamjawahi kucheza vilabu vya Cameroon. Nyie mlizaliwa ulaya huko mna haki juu ya viongozi. Mimi Cameroon ilinifundisha kwamba, napokuwa na timu ya taifa natakiwa kuwa mwanajeshi. Niwe tayari kukikabili kifo napopambania bendera. Leo Cameroon inapitia fedhea sababu wachezaji wengi hawana upendo wa asilimia  kwa taifa hili. Niwieni radhi kwa kujiongelea mimi kama mfano. Kwaajili ya upendo nilionao kwa nchi yangu, nilikuwa na uwezo wa kucheza mechi mbili kwa siku moja. Niliwahi kufanya hivyo, "Roger Milla" aliwahi kufanya hivyo, pia hata "François Omam Biyick." Unafikiri Cameroon ilikuwa ikitulipa zaidi ya vilabu tulivyokuwa tukichezea?! Hapana. Kuichezea Cameroon tulikuwa hatupati hata 1/10 ya kile tunacholipwa sehemu nyingine. Kufa ukiipambania nchi yako, thamani yake inazidi pesa yoyote katika ulimwengu.

Young Africans kucheza mbili za kirafiki

Image
  Uongozi wa Klabu ya Young Africans umesema umeanza mchakato wa kutafuta timu za nje kwa ajili ya mechi za kirafiki itakayokiweka sawa kikosi chao katika kipindi hiki cha maandalizi kabla ya kuanza kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mwishoni mwa juma lililopita Kocha Mkuu wa miamba hiyo ya soka nhini, Miguel Gamondi aliuomba uongozi wa timu hiyo kumtafutia mechi mbili za kirafiki na timu za nje ya Tanzania ili kujui uimara wa kikosi chake kabla ya mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbali na hilo pia Gamondi anataka kuitumia michezo hiyo kuwatambulisha rasmi wachezaji wao wawili wa kimataifa waliowasajili kwenye dirisha dogo la msimu huu ambao ni Augustine Okrah na Joseph Guede. Makamu wa Rais wa Young Africans hiyo, Arafat Haji amesema wameanza kutafuta timu hizo na anaamini mchakato huo hautachukua muda kukamilika sababu wana maelewano mazuri na timu nyingi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. “Lengo letu ni kupata timu imara ambazo zitakip