Posts

Showing posts from May, 2022

Joyce Kiria "Ukija Kwangu Mwanaume Uwe Umejipanga Siwezi Kulea Mwanaume, Nywele zangu tu Milioni 5"

Image
"Siwezi kuanzisha mahusiano na mwanammme masikini, siwezi kutunza mwanamme,ukija kwangu uwe umejipanga, nakupa invoice kuanzia nyumba ninayoishi, nywele zangu ninasuka kwa 5Milioni,sio uje kwangu na suruali ako"Joyce Kiria from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/QopHWqF via IFTTT

Kamera za CCTV Zilinasa Tukio la Mfanyakazi wa Ndani Kumnyonga Mtoto Hadi Kufariki

Image
Dada wa kazi anadaiwa kumuua Mtoto Erickson Kimaro (8) kwa kumnyonga. Tukio hilo limetokea Mei 30, 2022 eneo la Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku mbili tangu aanze kazi na Waajiri walikuwa hawajamfahamu vizuri. Imeelezwa kuwa, baada ya kufanya ukatili huo Mtuhumiwa alimpigia simu Mama kumjulisha Mtoto anaumwa na hapumui vizuri. Kichwa chake kilikuwa cha baridi na sehemu nyingine za mwili bado zilikuwa za moto. Ilithibitika ameshafariki dunia baada ya kukimbizwa Hospitali ya Mloganzila. Kamera (CCTV) ambayo hakujua ipo nyumbani hapo ilinasa tukio hilo na Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Gn1gQPR via IFTTT

Tuhuma za Gambo Ngoma Nzito, Wanane Wahojiwa

Image
  Tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zilizoibuliwa wiki iliyopita Jijini Arusha na kusababisha watumishi sita kusimamishwa kazi, zinazidi kulitikisa Jiji hilo baada ya idadi ya wanaohusishwa nazo kufikia wanane. Wiki iliyopita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwasimamisha kazi watumishi hao wa Halmashauri ya Jiji la Arusha akiwamo Mkurugenzi wake Dk John Pima kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na kulikabidhi suala hilo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili ichunguze. Katika sakata hilo, Mbunge wa Arusha mjini (CCM), Mrisho Gambo alimtaja Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa, Kenan Kihongosi kujihusisha na vitendo vya rushwa. Hata hivyo, jana Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, James Ruge aliliambia gazeti hili kuwa idadi ya wanaohojiwa na taasisi hiyo imeongezeka kutoka sita wa awali hadi nane kutokana na kubaini kuwepo kwenye mnyororo wa tuhuma hizo. “Ukiachilia mbali wale watuhumiwa sita tuliokabidhiwa, lakini sasa tumeongeza wengi

Hii ndio Video ya Harusi ya Swalha, Mrembo wa Mwanza aliyeuawa kwa Kupigwa Risasi na Mumewe

Image
  Hii ndio video ya harusi ya Swalha, mrembo wa Mwanza aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mumewe VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/JmAb5L1 via IFTTT

Mdogo wa Swalha Aliyeuawa Kwa Risasi na Mumewe Mwanza Asimulia Mapya Mazito, Ushirikina Wahusishwa

Image
Mdogo wa Swalha aliyeuawa kwa risasi na mumewe Mwanza asimulia mapya mazito, ushirikina wahusishwa Tazama VIDEO Hapa: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/JneiRAs via IFTTT

SOMA Habari Kubwa Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo May 31

Image
  Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo May 31 from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/4BVWwNQ via IFTTT

Wydad waivua ubingwa wa Afrika Al Ahly

Image
Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco imeshinda ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Al Ahly ya Misri. Mabao ya ushidi ya Wydad katika mchezo huu yamefungwa na Zouheir El Moutaraji aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 15 na 48. Hii ilikuwa ni fainali ya 5 Wydad wanacheza katika michuano hii na wamekuwa mabingwa kwa mara ya 3, wametwaa ubingwa mwaka 1992, 2017 na 2022. Mchezo huu umecezwa katika uwanja wa Mohammed wa 5 nchini Morocco ambao ni uwanja wa nyumbani wa Wydad hivyo walikuwa na faida ya kuwa na mashabiki wengi katika mchezo huu na wakafainikiwa kuwavua ubingwa Al Ahly ambao walikuwa wametwaa taji hili misimu miwili mfululizo iliyopita. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/IOYd2ul via IFTTT

Edo Kumwembe Ataka Simba Wamchukue Kocha wa Al Ahly Kuonesha Ukubwa wao

Image
Ameandika Edo Kumwembe: "Wakubwa wa MSIMBAZI....Ni wakati wa kuonyesha ukubwa wenu kama inavyosemwa....huyu jamaa anaweza kufukuzwa hapo Al Ahly....na nyie mnaweza kumfukuza Pablo....so chukueni huyu mtu...Al Ahly walikuwa wanamlipa milioni 280 kwa mwezi....Mkubwa MO....wakati wa kuonyesha ukubwa tunaouzungumza mitandaoni.....inawezekana kabisa" Edo from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Rkr9FLC via IFTTT

Mwanza: Mrembo Auawa na Mumewe, yadaiwa Alipigwa Risasi 7 kichwani, Sababu ni Hii *Exclusive Details

Image
Ni msiba mkubwa jijini Mwanza. Mwanamke maarufu jijini humo aitwaye Swalha, ameuawa kwa kupigwa na risasi na mumewe usiku wa kumkia Jumapili ya May 29. Tukio hilo limetokea nyumbani kwa wanandoa hao huko Buswelu. VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/QHVaBuN via IFTTT

Diva Loveness Aguswa na Mrembo Aliyeuawa Mwanza Kwa Risasi Saba na Mumewe

Image
Diva Ameandika haya " Very sad , Huyu Dada @iam_swallher ameuliwa Usiku wa Kuamkia Jumapili Na Mume Wake anaeitwa Said kwa Kupigwa Risasi 7 Kichwani na kufariki hapohapo, alikuwa Maarufu Kwa Mkoa wa Mwanza kwa urembo wake lakini Pia alikuwa Make Up artist Maarufu Jijini humo, Kisa Cha Kufikia Mauaji hayo inadaiwa ni wivu wa Kimapenzi, Mwanaume baada Ya Kufanya mauaji hayo alikimbia na mpaka dakika hii hajulikani alipo, ingawa kuna tetesi zinasema nae amejipiga risasi na haijiadhihirishwa kama ni kweli ila wasifu wake ni inasemekana ni mfanya biashara maarufu na anaejiweza kifedha na mara kadhaa alikuwa akimpiga dada huyu na kumtishia kuwa kuna siku angemiminia kichwani risasi , wazazi walihusika kuwasuluhisha na mara kwa mara alivumilia na kurudi kwa Mume wake, kuna siku alipigwa na kitako cha bunduki na kuzimia Masaa matatu mazima. Mwenyezi Mungu amuweke Mahali Pema Amina!. wanawake wenzangu Pls say NO to Violence .. ondoka kabisa .. anaekupenda ata awe amekuoa kama anaku

Wanafunzi Watangeneza Gari Linalotumia Sola

Image
  Arusha. Wanafunzi wanaosoma kidato cha tano katika shule ya Sekondari Arusha Science iliyopo kata ya Laroi mkoani Arusha wametengeneza gari linalotumia mwanga wa jua (sola) ikiwa ni utekelezaji wa mafunzo kwa vitendo ambayo wamekuwa wakifundishwa shuleni hapo. Gari hilo ambalo linatumia mwanga wa jua lina uwezo wa kutembea kilometa 160 likiwa na mzigo mwepesi baada ya hapo linahitaji kuchajiwa tena na tayari limeshatumia Sh3.5 milioni katika utengenezaji wake. Walter Tairo (19) na  mwenzake  ni Glenyce Amani (17) ni  miongoni mwa wanafunzi waliotengeneza gari hilo ambalo walianza mradi huo mwaka jana na kufanya hivyo ni kuweza kuonyesha kwa vitendo vile vyote wanavyofundishwa shuleni hapo . Walter amesema gari hilo halitumii mafuta na linasaidia kuokoa gharama ambapo linatumia mwanga wa jua na ni miongoni mwa magari ambayo yanatunza mazingira kutokana na utengenezaji wake. Glenyce amesema kuwa wanafunzi walioanzisha wazo la kutengeneza gari hilo wako sita "Wanafunzi

Azam FC chalii, Coastal Union yaifuata Young Africans

Image
  Mkwaju uliopigwa na Mubaraq Hamza umeipeleka Coastal Union hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ya Tanga, wakiitoa Azam FC. Mchezo huo wa pili wa Nusu Fainali ya ‘ASFC’ ulishuhudia hali ya furaha kwa Coastal Union ikitamalaki katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Dakika 120 za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikishindwa kufungana huku zikishambuliana kwa zamu, lakini Coastal Union walifika mara nyingi zaidi langoni mwa Azam FC. Katika mikwaju ya Penati Coastal union ilipata mikwaju 6 dhidi ya 5 ya Azam FC ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo. Ushindi huo wa Coastal Union unaipeleka mbele ya Young Africans iliyotangulia Fainali jana Jumamosi (Mei 28), kwa kuifunga Simba SC jijini Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba. Mchezo wa Fainali utapigwa Julai 02 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao leo Jumapili (Mei 29) umetumika kwa mchezo wa Nusu Fainali. from UDAKU SPECIAL https:/

Mwanamke Maarufu Jijini Mwanza Auawa na Mumewe Kwa Risasi Saba

Image
Mwanamke maarufu jijini Mwanza aitwaye Swalha, aliyekuwa akijishughulisha na masuala ya urembo (make up artist) ameuawa kwa kupigwa na risasi na mumewe usiku wa kumkia Jumapili ya May 29. Tukio hilo limetokea nyumbani kwa wanandoa hao huko Buswelu huku chanzo kikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa mume wa Swalha anayejulikana kwa jina la Said alichukua uamuzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Amesema Swalha alienda kuangalia mpira na akachelewa kurejea nyumbani. Mumewe hakufurahishwa na kitendo cha mkewe kuchelewa kurudi nyumbani hivyo kukazuka ugomvi baina yao hali iliyopelekea mume wa Swalha kumfyatulia risasi. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/71kTer9 via IFTTT

Real Madrid washinda taji la 14 la Ligi ya Mabingwa

Image
Bao moja la Vinicius Junior kunako dakika ya 59 lilitosha kuihakikishia Real ushindi wa 14 wa kombe la Ulaya mbele ya mashabiki 80,000 mjini Paris. Real Madrid kwa mara nyingine inarejea nyumbani na kombe, Madrid imetumia fursa na kuwaacha wengi wakijiuliza ni kwa jisi gani wameambulia ushindi wa konbe hilo.  Jaribio la mshambuliaji Karim Benzema liliamuliwa kwa utata kuwa ameotea.   Mchezaji wa Liverpool Mohamed Salah akinyimwa nafasi ya kuikomboa mara tatu timu yake na mlinsa lango wa Real Madrid Thibaut Courtois. Usalama uwanjani Fainali hio ilicheleweshwa kwa zaidi ya dakika 35 kwa sababu za usalama. Shirikisho la Kandanda Barani Ulaya UEFA ililaumu kuchelewa kuwasili kwa mashabiki, lakini mashabiki walilaumu mamlaka kwa kuchelewa kufungua uwanja wa Stade de France. Mamia ya mashabiki wa Liverpool walimiminika kujaza viti katika uwanja wa Stade de France, polisi wa Ufaransa walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi ili kuwazuia. "Tumesikitishwa sana na m

Manara Afunguka "Kuniroga Hamniwezi Kunipiga ndio Kabisa iliyobaki Mkalambe Sumu tu"

Image
Kuniroga hamniwezi,,kunipiga ndio kabisaaaaaa,,iliyobaki mkalambe sumu tu. Naitwa Haji Sunday Ramadhan Manara, Bugati. Mpira nna Hijaza nao, nna DNA na football, sikukutana nao Mtaani, kisha mimi ni Ahllu Bait ( Kitukuu cha Rasuli) Nimezaliwa ili niwe Msemaji wa Soka, na nna nyota ya Subailah, Kiufupi HAMNIWEZI ,,Niliadhiniwa na Masharifu nilipozaliwa,,, Mkimaindi napost Royal Tour Goal Beauty Beauty 🤪🤪 from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/jBEYwzR via IFTTT

Moo Dewji Afunguka "Hongereni Yanga, Bodi ya Simba inabidi ifanye Maamuzi Magumu"

Image
Kupitia Instagram yake @moodewji ameeleza namna @simbasctanzania ilivyopitia msimu mgumu kwa takribani misimu mitano na kuitaka bodi kufanya maamuzi magumu. Ameandika kuwa: “ Hongereni watani! This has been the worst season for Simba in last 5 years. The board needs to make tough decisions on the way forward. We need to overhaul our team and strategy and go back to the drawing board. We lacked motivation, passion and hunger to win trophies this year.” from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/wpVYrkG via IFTTT

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona YANGA vs SIMBA"

Image
1: MWANZA IS GREEN & YELLOW🟢🟡 WASIOAMINI WAMEAMINI KWA MACHO YAO.. YANGA WAMESTAHILI KWENDA FAINALI✊ 2: PROFESA NABI🙌 SIMPLY, ANASTAHILI KUWA MAN OF THE MATCH 👏 Alimuweka PABLO kwenye kiganja chake na kumpa maswali magumu sana kiwanjani. Mechi Iliisha kwenye Mkoba wake wa mbinu 3: Dakika 180 za Ligi, Nabi alikwenda na mfumo wa 4-2-3-1 Lakini hapa MWANZA AKAJA NA 3-5-2! Approach ikiwa ni kushambulia kwenye kipindi cha kwanza. Hatua za Djuma na Shomari zikileta vurugu kubwa kwa mistari miwili ya ulinzi ya Simba.. Kivipi? 4: Kumbuka Yanga walianza na 'Dabo Straika'! Hapa Henock na Onyango wakawa 'bize' uwanjani. Ile 'Battle' ya 3v3 katikati ya kiwanja ikawa inaamuliwa na 'Movements' za 'Wing back' za Yanga. Taddeo Lwanga akapata mechi ngumu zaidi ya 'Derby' tangu atue Tanzania 5: Bila 'Key Players' wake baadhi, Sielewi kwanini PABLO aliamua kuanza mechi ya 4-3-3 akiwa na mpango wa kushambulia. Kanoute na Muzamir &#

Dahh Maskini Kocha Pablo Abariki Kipigo Kitakatifu Cha Yanga...Inauma

Image
WAMETUZIDI! Ni kauli ya Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco akikiri wapinzani wao, Yanga wamekuwa bora kuliko vijana wake hasa dakika 45 za kipindi cha kwanza. Licha ya kukiri kuzidiwa na Yanga hasa eneo la kati, Pablo amesema kikosi chake kimefanya jitihada mbalimbali za kusawazisha na kupata ushindi ikiwemo kufanya mabadiliko ya wachezaji lakini haikufua dafu na kujikuta wakiwa na siku mbaya kazini. Mbali na hilo Pablo amelia na majeruhi ndani ya kikosi chake ambayo yamesababishwa na idadi kubwa ya mechi za mfululizo na hali ya hewa. Katika mchezo huo Simba imewakosa wachezaji muhimu Clatous Chama, Jonas Mkude, Peter Banda, Aishi Manula, Israel Patrick, John Bocco, Paschal Wawa na Shomari Kapombe. Pablo amesema kukosekana kwa wachezaji wake hao kutokana na kuandamwa na majeraha ni miongoni mwa sababu za kikosi chake kushindwa leo kumfunga mtani wake na kutinga fainali. "Walikuwa bora kwa dakika 45 za kwanza na wamecheza vizuri zaidi yetu, tumejaribu kubadilika na kur

Simba Yapigwa Faini Tena Kisa Hichi Hapa

Image
Klabu ya simba imetozwa faini ya sh 1,000,000(milioni moja) kwa kosa la mashabiki wake kumrushia chupa za maji mchezaji wa Azam Fc Daniel Amoah wakati mchezo wao namba 206 kwenye uwanja wa Azam Complex Mei 18, 2022. Pia simba imetozwa faini ya kwa kosa la timu yake kuchelewa kutoka kwenye chumba cha kuvalia nguo kwa dakika nne hali iliyosababisha mchezo huo uanze saa 1:04 usiku badala ya saa 1:00 usiku. Adhabu hizi ni kwa kuzingatia kanuni ya 47:7 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa klabu. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/6VbUvQs via IFTTT

Mdee Arekebisha Kauli "Sina hizo bilioni 10 nilikuwa nafikisha ujumbe tu"

Image
Dodoma. Hoja ya mbunge wa viti Maalumu Halima Mdee kuhusu Sh10 bilioni imeendelea kutikisa katika mitandao ya kijamii wengi wakihoji alipata wapi kiasi hicho. Hata hivyo jana Mdee alizungumzia jambo hilo na kukanusha kuwa hana kiasi hicho kwenye akaunti yake bali amesema kwa maana ya kufikisha ujumbe kwa Serikali. Juzi wakati akichangia hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mdee alihoji kwanini Serikali inakosa Sh10 bilioni kwa ajili ya kupanga ardhi kwenye vijiji wakati yeye na Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wanazo katika akaunti zao. Katika mchango wake mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Kawe, alionyesha kusikitishwa na Serikali inaposhindwa kutoa kiasi cha Sh10 bilioni ambazo zingewezesha kupima vijiji 750 kwa mwaka lakini ikatoa Sh1.4 bilioni zinazokwenda kupima vijiji 100. Amesema mawaziri wameacha kufanya shughuli zao za msingi wanaingia katika kwenda kutatua migogoro na kwa

CCM Wajibu Mapigo ya NCCR Mageuzi "Selasini ni Anajitafutia Umaarufu kwa Kuipaka Matope CCM"

Image
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema ajenda kubwa kwa sasa ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuhuisha demokrasia nchini. Alisema hayo kupitia taarifa aliyotoa jana akikanusha madai yaliyotolewa na mwanasiasa Joseph Selasini kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewahi kumtumia James Mbatia au kuwa na ushirikiano na NCCR-Mageuzi. Alisema CCM inalo jukumu moja la kumuunga mkono Rais Samia katika safari ya maridhiano aliyoianzisha hivyo haiwezi kurudi nyuma. “Kwa wakati huu CCM kama chama kiongozi na mlezi wa siasa nchini tunalo jukumu moja tu, la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika safari ya maridhiano aliyoianzisha hivyo hatuwezi kurudi nyuma bali kusonga mbele," alisema. Shaka alieleza chama kilivyosikitishwa na madai hayo aliyosema ni upotoshaji unaotaka kuihusisha CCM katika sakata linalotoka ndani ya NCCR-Mageuzi. Alisema kinachofanywa na Selasini ni kujitafutia umaarufu kwa kuipaka matope CCM. “Hivyo kud

Kicheko Tena Posho Watumishi wa Umma..Mama Anaupiga Mwingi Sana

Image
BAADA ya kupandisha mishahara ya watumishi wa umma kwa asilimia 23, Rais Samia Suluhu Hassan amepeleka kicheko kingine kwao, safari hii akitoa kibali cha kurekebisha posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa watumishi wa umma na kiwango cha malipo ya kazi maalum (Extra Duty). Kwa mujibu wa Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora, utekelezaji wa kibali hicho umepangwa kuanza rasmi Julai Mosi, mwaka huu, yaani siku ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/23. Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alibainisha hayo jijini Dodoma jana wakati wa kikao kazi cha wakuu wa idara na vitengo vya utawala na usimamizi wa rasilimali watu katika utumishi wa umma chenye lengo la kutathmini utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Dk. Ndumbaro alisema kuwa kutokana na kibali hicho cha Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa watumishi wa umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka Sh. 120,000 hadi 250,000 na kiwango cha ch

Soma Habari Kubwa Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo May 28, Rais Samia Apeleka Kicheko kingine kwa Watumishi

Image
  Soma Habari Kubwa Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo May 28, Rais Samia Apeleka Kicheko kingine kwa Watumishi from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/WV7rxjT via IFTTT