Posts

Showing posts from August, 2023

Fiston Mayele Aanza Balaa FC Pyramids, Apiga Hat-trick

Image
  Fiston Mayele ameanza na kutupia katika mchezo wake wa kwanza akiwa na Jezi ya timu yake mpya ya Pyramid ambao waliumana na Bardur FC ya Uturuki. Hii ni mehi ya kwanza kuanza katika kikosi cha Pyramids na amefunga bao tatu (3) ikiwa Pyramid imeibuka na ushindi wa bao 7 - 0. Miamba hii ya Misri imepiga Kambi Uturuki ikijiandaa na Ligi kuu ya Misri na michuano ya kimataifa ambapo wapo kwenye Ligi ya mabingwa. Mipango Yao ni kubeba ubingwa wa michuano yote wanayoshiriki na hii ni mara ya kwanza kwao kushiriki Ligi ya mabingwa Afrika. Mpinzani wao kabla ya kutinga makundi ni APR ya Rwanda ambao APR wataanza Nyumbani Rwanda Kisha Cairo Misri. Tazama Video hapa chini; from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/9EsMm3w via IFTTT

Maofisa BOT watua Namanga kudhibiti uuzaji holela dola

Image
Namanga. Kutokana na uwepo wa changamoto ya upatikanaji wa fedha za kigeni, baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wamewataka wafanyabiashara katika mpaka wa Namanga kuwa na Leseni za maduka ya mabadilisha fedha za kigeni. Biashara haramu ya fedha za kigeni imeelezwa kuchangia kupunguza fedha hizo katika mzunguko kutokana na watu wachache kumiliki fedha nyingi na wengine kusafirisha nje ya nchi kinyume cha sheria. Akizungumza na wafanyabiashara na maofisa wa Serikali katika mpaka huo leo Agosti 31, Mkuu wa kitengo cha Uchunguzi wa BOT, Amri Mbarilaki amewataka kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kufanya biashara halali ya fedha za kigeni. "Tukiendelea na biashara hii haramu uchumi utaharibika na ukiharibika hasara itakuwa kwetu sote hata kwa ambao wanafanya biashara hii," amesema. Amesema ni muhimu ambao wanataka kufanya biashara ya kubadilisha fedha kufuata sheria na Kanuni ikiwepo kuwa na Leseni ya biashara hiyo. Kwa upande wake Meneja msaidizi wa usima

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji Arusha na Wenzake Wahukumiwa Kifungo cha Miaka 20 Jela

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imetoa hukumu hiyo kwa Dkt. John Pima aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, na wenzake wawili baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi Wengine waliohukumiwa ni Mariam Mshana (aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha) na Innocent Maduhu (aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji) Aidha, Mahakama imeeleza miezi 14 waliyokuwa kizuizini itazingatiwa katika hukumu yao, pia washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/yuRiMZe via IFTTT

Ajali ya Moto Ghorofani Yauwa 73

Image
Takriban watu 73 wamefariki Dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa, baada ya moto kuzuka katika jengo moja jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, wengi wakihofiwa kuwa ni wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Barani Afrika. Hata hivyo, chanzo cha moto huo uliotokea katika jengo la ghorofa tano katikati mwa jiji hilo hakijafahamika, lakini Msemaji wa Huduma za Dharura, Robert Mulaudzi amesema waokoaji na wazima moto wameweza kuwatoa baadhi ya watu waliokuwa ndani, huku waliokwama manusura wakiendelea kutafutwa. Jengo hilo, lipo katika kitongoji cha ndani ya jiji ambacho kina sifa mbaya kwa majengo ‘yaliyotekwa nyara, neno linalotumiwa nchini Afrika Kusini likimaanisha majengo yaliyochukuliwa kinyume cha sheria na wahamiaji wasio na vibali. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/P7h9TUI via IFTTT

Siri ya Kocha kutimuliwa yafichuka Singida FG

Image
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate FC, Hans van der Pluijm, amesema kitendo cha kuingiiliwa katika majukumu yake, ndio chanzo cha yeye kuamua kuacha kuendelea kuifundisha timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imefahamika. Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo umetoa taarifa ya kuachana na Kocha huyo kutoka nchini Uholanzi, ambaye alipewa mkataba mpya baada yà ule wa awali kumalizika ilipofika Juni 30, mwaka huu. Ofisa Habari wa timu hiyo, Hussein Masanza, amesema pande zote mbili zimefikia makubaliano na sasa timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Mathias Lule. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Dar es salaam zinasema Pluijm amefikia kufanya uamuzi wa kujiuzulu kwa sababu ya kutokubali kuingiliwa majukumu yake ikiwamo upangaji wa kikosi. Chanzo hicho kiliendelea kusema kitendo cha kukosa uhuru wa kufanya kazi ikiwapo kuingiliwa kupanga kikosi katika mchezo wa marudiano ya mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika walipocheza dhidi ya

Mambo Matano ya Kuitengeneza Yanga ya Gamondi Iwe Tishio CAF

Image
Kouassi Yao (26) ni jina linalotajwa na kuzungumzwa sana kwa sasa. Ni beki wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga aliyesajiliwa kutoka ASEC Mimosas kwenye dirisha hili la usajili linalotarajiwa kufungwa Agosti 31. Yao ametua Yanga kuziba pengo la Djuma Shaban aliyeachwa baada ya kuomba kuondoka kwenda kujaribu changamoto sehemu nyingine. Kwa Yao, Yanga imefanikiwa kwa kiasi kikubwa, pia kuna maingizo mapya kama Nickson Kibabage (Singida Fountain Gate), Jonas Mkude (huru), Maxi Nzengeli (AS Maniema Union), Gift Fred (SC Villa), Mahlatsi Makudubela (Marumo Gallants), Pacome Zouzoua (ASEC) na Hafiz Konkoni. Yao anatajwa sana kutokana na ubora wake aliouonyesha kwenye mechi za timu hiyo alizocheza. Hata hivyo, Kocha wa kikosi hicho kinachopambana kufika kufanya makubwa zaidi msimu huu, Miguel Gamondi, ana kazi ya kufanya hasa kwenye kutengeneza safu bora ya ushambuliaji kama ilivyokuwa msimu uliopita iliyoongozwa na Fiston Mayele. Misimu miwili ya mafanikio Yanga, haikuwa

BREAKING: Jeshi la Gabon Lawmpindua Rais wa Nchi hiyo Ali Bongo

Image
Jeshi la Gabon limempindua Rais wa Nchi hiyo Ali Bongo siku kadhaa baada ya Uchaguzi uliomrejesha madarakani, Wanajeshi hao wameongea kupitia Televishion ya Taifa wakisema wameamua kuwalinda Wananchi kwa kuumaliza Uongozi usiofaa ambapo umeingia madarakani kwa kura za wizi. Wanajeshi 12 wameonekana kwenye televisheni wakitangaza kuwa wanafuta matokeo ya uchaguzi na kuvunja Taasisi zote za Jamhuri. Taarifa ya Jeshi hilo imesema “Tume ya Uchaguzi wa tarehe 26 Agosti 2023 haikutimiza masharti ya kura ya uwazi ambayo Watu wa Gabon walitarajia, huu ni utawala usio na uwajibikaji na usiotabirika, unaosababisha kuendelea kuzorota kwa mshikamano wa kijamii, na hatari ya kusababisha Nchi katika machafuko, tunafuta matokeo, mipaka imefungwa hadi taarifa zaidi, Taasisi zote za Jamhuto zimevunjwa ikiwemo Seneti, Bunge la Kitaifa, Mahakama ya Katiba, Baraza la Uchumi, Kijamii na Mazingira na Kituo cha Uchaguzi cha Gabon” from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/jkxLOot via IFTTT

Kocha JKT afunguka kilichomponza akapigwa 5-0 na Yanga

Image
  Kocha JKT Tanzania, Malale Hamsini amefunguka sababu ya kikosi chake kukubali kupokea kichapo cha bao 5-0 kutoka kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga Sc jana katika Dimba la Azam Complex, Chamazi. Malale amesema kilichowaponza ni mabadiliko ya wachezaji aliyoyafanya kwani hawakuweza kutekeleza kile ambacho aliwaelekeza kwenda kukifanya ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kuziba njia za yanga kuwaadhibu. "Mchezo umekwisha, matokeo tumeyakubali. Kilichoniangusha ni zile sub nilizofanya hazikutimiza majukumu yake. Niliwaelekeza wakazibe njia za Yanga lakini sub zangu zimeruhusu njia za yanga kuwa wazi na kusababisha tukafungwa mabao mengi. "Kipindi cha kwanza njia za yanga nilizizuia kwa viungo na winga zao ambazo wanazitegemea sana. Nilitegemea zile sub zangu zitaendeleza kile tulichokifanya kipindi cha kwanza, lakini wao walipoingia wakataka kurudisha lile bao moja tulilokuwa tumefungwa kipindi cha kwanza, hii ndiyo imegharimu timu nzima. "Sub zangu

KIMEUMANA....FIFA Waifungia Yanga Kusajili Mpaka Watakapo Malizana na Bigirimana

Image
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo. Birigimana alifungua kesi FIFA kuhusiana na malipo ya ada ya usajili (sign on fee) ambapo klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo. Wakati FIFA imeifungia Yanga kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani. TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili. “Iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu.” TFF  from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/etAuJEh via IFTTT

Kikosi Yanga vs JKT Tanzania Leo 29 August 2023 NBC Premier League

Image
Kikosi Yanga vs JKT Tanzania Leo 29 August 2023 NBC Premier  League Yanga itaikarbisha JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Agosti 29 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi saa 1:00 usiku Yanga ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi tatu katika mechi sawa na JKT Tanzania ambayo ipo nafasi ya Sita Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi akizuungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam na amesema wamejiandaa vizur katika mchezo huo na anataka mabao ili kuwafurahisha Wananchi “Licha ya kwamba mpinzani wetu tunajua ni timu iliyopanda daraja, najua kwamba wana wachezaji wenye uzoefu kwenye ligi hivyo hatupaswi kuichukulia kama timu dhaifu au ngeni kwenye ligi" "Ni wageni kwa maana ya timu lakini wana idadi kubwa ya wachezaji wenye uwezo lakini sisi ni timu kubwa na tupo nyumbani nafikiri kesho tunapaswa kujiamini na kufunga magoli mengi" amesema Gamondi Kwa upande wake kocha msaidizi wa JKT Tanzania George mketo amesema amejiandaa vizuri na mchezo wa kesho kwa

Msimamo Ligi Kuu NBC 2023/2024 Tanzania Premier League

Image
Msimamo Ligi Kuu NBC 2023/2024 Tanzania Premier League Msimamo Ligi Kuu NBC 2023/2024 Tanzania Premier League – Msimamo NBC Tanzania Premier League 2023/2024 Table Standings,Msimamo ligi kuu NBC Premier League 2023/2024 Tanzania, Ratiba NBC Premier League, GET ALSO: Msimamo NBC Premier League, Wafungaji bora NBC Premier League, NBC Premier League Standings 2022/2023,Tanzania Premier League Table Standings 2023/2024,Msimamo Ligi Kuu NBC Tanzania Premier League 2023/2024, Msimamo NBC Premier League 2023/24, Msimamo Ligi kuu bara Msimamo Ligi Kuu NBC 2023/2024 Tanzania Premier League The scheduling of matches is carefully organized to ensure that all teams have an equal opportunity to compete. The Tanzania Premier League Board takes into account various factors, including travel logistics, stadium availability, and the need for a fair distribution of home and away matches for each team. Standings provided by Sofascore from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Zt0j2nX via IFTTT

Mpenzi wa Mobetto atua Bongo, Mwamba Afunguka Haya Muhimu

Image
   Mpenzi wa Mobetto atua Bongo, Mwamba Afunguka Haya Muhimu Kutoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mpenzi wa mwanamitindo Hamisa Mobetto aitwaye Kevin Sowax ametua Dar es Salaam na kupokelewa na mpenzi wake huyo usiku wa kumakia leo. Kevin amenukuliwa akisema wakati anakutana na Mobetto hakujua kama ni Super Star huku akiweka wazi kumtolea posa mrembo huyo. Kevin Sowax ambaye ni CEO wa Kampuni ya Twinsk ya nchini Kenya ameshukuru kwa kupata mapokezi makubwa aliyopata kutoka kwa Watanzania. Sowax amebainisha kuwa amekuja Bongo kwa ajili ya kumsalimia Mobetto na familia yake sambamba na mambo yake ya kibiashara ambayo hakutaka kuyaweka wazi ni aina gani ya biashara. Aidha, Sowex amesema hakuwahi kukutana na Mobetto tangu mwanzo lakini wamekuwa wakiwasiliana tu kwa njia ya simu lakini sasa wameamua kukutana uso kwa uso. Mfanyabiashara huyo wakati akihojiwa na vyombo vya habari vya Tanzania, amesema kuwa hana mtoto na anatarajia kupata mtoto kupitia kwa Mobet

Rais Samia Akemea Mapenzi ya Jinsi Moja Tanzania

Image
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa kuimarisha ulinzi wa vijana dhidi ya kampeni zinazofanywa na baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi ya kueneza mapenzi ya jinsia moja kwa mgongo wa miradi ya maendeleo. Bila kutaja majina, Rais Samia amesema kumekuwa na mashirika yanapata fedha nyingi lakini lengo kuu ni kuharibu vijana wa taifa. “Kuna miradi mingi inapata pesa huko chini na ukiangalia mingi inajielekeza kwenye eneo la Afya, Mazingira ili wawapate vijana wetu na kutuharibia. Kuweni na jicho zuri huko chini,” amesema akiwataka viongozi hao kubaini lengo la miradi na kile kinachofanyika katika eneo lao. “Dunia inabadilika mpaka inasikitisha. Unakwenda kwenye mkutano, analetwa mwanamme kufungua mkutano, anamtambulisha mme wake au anakuja mwanamke anakuja na mke wake … wanatufanyia hivyo ili tuone ni mambo ya kawaida. Nyie wote humu ndani ni waumini haya mambo yanakatazwa,” amesema Rais Samia. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Sd0KTCy v

Tamu, Chungu za Makonda wa Kike Mabasi ya Abiria

Image
  Safari yangu inaanza saa 11 alfajiri ya Julai 18 mwaka huu, kutoka nyumbani Tabata kuelekea Shekilango jijini Dar es Salaam katika kituo kidogo cha mabasi yanayokwenda mikoani. Nikiwa nje ya gari ninalopanda namuona binti akifungua buti la gari na kuweka mizigo. Namsogelea na kumuuliza kama ni mhusika, ananijibu; "Mimi ni kondakta wa gari hili, wewe unashukia wapi? kama mwisho nitakupeleka upande wa pili kama njiani leta begi lako hapa." Namjibu sina mzigo, nakaa pembeni nikimuangalia anavyofanya kazi kwa kuwa ni mazoea kwa wanaume kufanya shughuli hii. Baada ya dakika 20 anakuja kijana wa kiume kumsaidia. Wanapomaliza kupakia mizigo binti anakabidhiwa karatasi. Nafuatilia kujua ni ya nini, nabaini ni orodha ya majina ya abiria. Sawa na abiria wengine, naingia ndani ya gari kukaa kwenye kiti changu. Saa 12:15 asubuhi safari inaanza kutoka Shekilango kuelekea Kituo cha Mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi Luis. Hakuna msongamano Barabara ya Morogoro, tunatumia da

Singida Fountain Gate Wachapwa Goli 2 na JKU Chamazi

Image
   Singida Fountain Gate Wachapwa Goli 2 na JKU Chamazi Timu ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ imefanikiwa kwenda hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kufungwa mabao 2-0 na JKU ya Zanzibar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya JKU leo yamefungwa na Nassor Juma dakika ya saba na Gamba Matiko dakika ya 42 na kwa matokeo hayo Singida Big Stars inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 kufuatia kushinda 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita na sasa watamenyana na Future ya Misr from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/iTeNgqV via IFTTT

Bondia Mandonga Aibu TUPU Apigwa Tena Huku Zanzibar

Image
Bondia Mandonga Aibu TUPU Apigwa Tena Huku Zanzibar  Bondia Muller Jr ameibuka mshindi kwenye pambano la Raundi Sita dhidi ya Karim Mandonga pambano la Tamasha la Uzinduzi wa Mchezo wa Ngumi Zanzibar lilopigwa katika uwanja wa Mao Tse Tung, Zanzibar. Muller Jr ameshinda kwa uamuzi wa Majaji na kuwa moja ya walioandika historia ya kushiriki kwenye tukio la kuurejesha tena mchezo wa Masumbwi Zanzibar baada ya miaka 60 kupita bila ya mchezo huo. Pambano hilo la Raundi Sita limeshuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ambaye alijuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya ngumi yaliyopigwa marufuku Kisiwani hapo zaidi ya mika 50 iliyopita ambapo Majaji wote watatu wamempa ushindi Kiluwa kwa pointi 55-56, 56-58 na 55-59 Hii ni mara ya tatu mfululizo Mandonga kupigwa. Julai 22 alipoteza pambano la marudiano na Mkenya Daniel Wanyonyi, na Julai 29 alipoteza pambano dhidi ya mganda Moses Golola na sasa Mandonga anasema anajipanga kwa ajili ya pambano jingine. from UD

Simba vs Power Dynamos, Yanga vs El Merrikh Ligi ya Mabingwa Afrika

Image
Mabingwa wa Zambia Power Dynamos watachuana na Simba katika mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika Ni baada ya Power Dynamos kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Stars jana na hivyo kufuzu raundi ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini baada ya kuchapwa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza Mchezo wa kwanza utapigwa Septemba 15 huko Zambia na mchezo wa marudiano kupigwa Septemba 29 jijini Dar es salaam Simba na Power Dynamos zilichuana kwenye Tamasha la Simba Day, Wekundu wa Msimbazi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Timu hizo zinakutana tena mara mbili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi Wakati Simba ikichuana na Power Dynamos, Watani zao Yanga wao watachuana na El Merrikh ya Sudan Jana Yanga ilitinga raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 dhidi ya Asas Fc ya Djibout wakati El Merrikh walifuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Ot

Shamsa Asimulia Walivyokutana na Mlilo Hadi Ndoa...

Image
  Mrembo kutoka kiwanda cha sanaa Bongo, Shamsa Ford amesema yeye na mumewe Mlilo, kabla ya kufunga ndoa walikutana kwenye kazi za uigizaji. Akisimulia tukio hilo, Shamsa alisema walibadilishana namba na wakaja kuwasiliana baada ya kuonana tena kama miezi minne ilipita ndipo wakawa marafiki wa kawaida kabla ya kuingia kwenye mahusiano. "Tulibadilishana namba akawa zile ananitumia ujumbe leo najibu baada ya wiki, lakini tulikutana tena baada ya kama miezi minne hivi ndipo sasa tukawa marafiki. "Akawa ananielezea matatizo yake ya kwenye mahusiano na mimi namuelezea yangu hivyo basi tukajikuta tupo kwenye mahusiano na baadaye akanioa baada ya kuachana na mkewe aliyekuwa naye kabla yangu," alisema Shamsa. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/5ns6l2e via IFTTT

Nchi 10 Duniani Zinazoongoza Kuwalipa Walimu Mishahara Mikubwa

Image
   Nchi 10 Duniani Zinazoongoza Kuwalipa Walimu Mishahara Mikubwa Malalamiko juu ya mishahara midogo kwa walimu yamekuwa yakisikika katika maeneo mengi duniani, lakini licha ya malalamiko hayo yapo maeneo ambayo walimu hulipwa mishahara mizuri zaidi. Huko nchini Luxembourg walimu wa sekondari wa chini walio na uzoefu wa zaidi ya miaka 15, hupata hadi kiasi cha TZS 254,663,728. World Economic Forum imetoa orodha ya nchi 10 duniani zinazowalipa walimu mishahara mikubwa zaidi. 10. Austria : $62,882 (Sawa na TZS 146,640,824) 9. Ireland : $62,906 (Sawa na TZS 146,696,792) 8. Denmark: $64,259 (149,851,988) 7. Mexico: $64,491 (Sawana TZS 150,393,012) 6.United States: $65,248 (Sawa na TZS 152,158,336) 5.Australia: $65,714 (Sawa na TZS 153,245,048) 4: Canada: $71,664 (Sawa na TZS 167,120,448) 3. The Netherlands: $81,064 (Sawa na 189,041,248) 2. Germany: $91,041 (212,307,612) 1. Luxembourg: $109,204 (Sawa na 254,663,728) Utafiti linganishi wa Nation Newsplex na Taasisi ya Masuala ya

Mudathir Afunguka Ishu ya Simu ya Mkewe Uwanjani

Image
  Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya amefunguka staili yake ya kushangilia aloitumia baada ya kufunga bao katika mechi ya ufunguzi kwenye Ligi Kuu dhidi ya KMC iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex wakiibuka na ushindi wa 5-0. Mudathir alionekana akitoa ‘Shin Gurd’ yake mguuni na kuitumia kama ishara ya kupiga simu kuzungumza na mtu. “Nikiwa sina kitu cha kufanya huwa natumia muda mwingi kuzungumza na mtoto wangu ‘Manha’ pamoja na mke wangu, kabla sijaja kwenye mchezo nilizungumza nao wote na niliwaahidi kufunga ndio maana nilitoa Guard nikafanya kuwa kama simu niwapigie niwaambie nimefunga,” amesema. Mudathir amekuwa na muendelezo mzuri wa kiwango chake tangu asajiliwe na Yanga kama mchezaji huru baada ya kuachwa na Azam FC. Kocha Miguel Gamondi amekuwa akionyesha imani kwa kiungo huyo ambaye amekuwa akicheza katika kikosi cha kwanza mara kwa mara chini ya kocha huyo. Yanga katika mchezo wa ufunguzi kwenye ligi iliibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya KMC huku mabao hayo yakifungwa Dicks

Yote Aliyoyasema Rais Samia Mkutano wa BRICS

Image
  Wakati viongozi wa umoja wa mataifa yanayochipukia kiuchumi (Brics), wakitangaza kuzipokea nchi sita kuwa wanachama wapya kuanzia mwaka ujao, Rais Samia Suluhu Hassan ametaka ushirikiano wa umoja huo na Afrika kujikita kwenye kufungua fursa barani humo, ili kufikia azma ya Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDGs). Ili kufikia malengo hayo, alisema kuna haja ya kuuimarisha Umoja wa Mataifa ili kuongeza ushirikiano wa mataifa, huku akipendekeza kubadilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili liwe na uwakilishi wa haki. Brics, inayoundwa na nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, zilikubaliana katika mkutano wao kuzifanya Argentina, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa wanachama kamili kuanzia Januari Mosi, Katika mkutano huo wa siku tatu uliohitimishwa jana huko Johannesburg, Afrika Kusini, viongozi zaidi ya 50 kutoka mataifa yasiyo wanachama wa Brics walihudhuria, akiwemo Rais Samia. Takribani nchi 40 duniani zimeonyesha

Kocha Gamondi Kazi Anayo, Wachezaji Wote Wakali na Wanafanya Vizuri, Nani Aanza Nani Akae Benchi

Image
Hakuna kitu kizuri kama kuiangalia Yanga ya Gamondi ikicheza, kama unadaiwa kodi, una njaa, una uchovu ama unaumwa homa ndogondogo basi ni dawa inayotibu kwa dakika 90 tulizoshuhudia pale Azam Complex, Chamanzi. Hakuna kitu kigumu hivi sasa kama kutabiri kikosi cha Yanga kitakachoanza, kila mchezaji anapata nafasi na anakupa kile unachohitaji kwa ubora wa hali ya juu. Hakuna kitu kigumu kama kutaja man of the match kwenye mchezo wa leo kutokana na namna wachezaji wote walivyomwaga jasho kuipigania bendera ya kijani na njano. Sio Kibwana aliyekosa michezo kadhaa, sio Mkude aliyekua Morogoro kwenye mechi mbili za nyuma, sio Sure boy aliyekaa benchi mechi mbili, sio Max , sio Kibabage, sio Pacoume aliyeingia kutokea Sub, sio Azizi ki aliyezaliwa upya msimu huu, wala sio Mzize ambaye hakuwepo hata sub kwenye mchezo uliopita kila mmoja anakiwasha🔥. Hapo bado man of the match kwenye mchezo dhidi ya KMC, Mudathir yuko benchi mtawala wa dimba la kati Doctor Khalid Aucho yuko jukwaan

Mume wa Diva Atoa MPYA 'Siwezi Kuoa Mwanamke Masikini'

Image
  Mume wa mtangazi maarufu nchini kutoka Wasafi Media, Diva the Bawse aitwaye Abdulrazack amesema kuwa kwa hadhi aliyofikia kwa sasa hawezi kuoa mwanamke masikini ambaye hana pesa. Abdulrazack ambaye hivi karibuni ilionekana kama ameribuana na Diva amesema mkewe huyo (Diva) ni tajiri hivyo itakuwa jambo la ajabu na aibu kwake kuoa mwanamke ambaye hamfikii pesa Diva. "Mimi sipendi kulelewa lakini katika Uislamu tumeambiwa unapomuoa mwanamke angalia vitu vinne kwa mwanamke, Uzuri wake, Dini yake, Ukoo wake na mali yake, mimi sitaki mwanamke ambaye hana kitu, hana kazi yoyote kwasababu maisha yamebadilika kuna watoto kwenye ndoa kwahiyo ni muhimu kuwa na Mwanamke ambaye angalau kichwa chake kinafanya kazi. "Sitaki kuoa mwanamke ambaye ni golikipa kila kitu ananiangalia mimi, kwa levo niliyofikia mimi siwezi kufanya hicho kitu, kwa sasa hivi mshahara ninaowalipa wafanyakazi wangu kwa mwezi haipungui milioni kumi na kuendelea nawezaje kuoa mwanamke ambaye hajishughulishi

Matokeo Yanga vs ASAS Leo 26 August 2023

Image
Matokeo Yanga VS ASAS Matokeo Yanga vs ASAS Leo 26 August 2023 Siku ya kesho Yanga watashuka dimbani Tena kuvaana na Asas Fc katika mchezo wa pili CAF  CHAMPIONS league hatua ya awali. Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Asas Fc Mechi ya kwanza Yanga iliibuka na ushindi wa goli 2-0 katika uwanja wa Azam complex chamazi ambapo kiitifaki Yanga walikuwa wageni kwa ASAS FC. Mechi itapigwa majira ya saa kumi na moja jioni 17;00 MATOKEO YANGA Vs ASAS YANGA 0:0 ASAS from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/SCdoft9 via IFTTT

JKT yataja vigezo kwa Vijana wa nafasi za kujitolea wanaotaka kujiunga Mafunzo ya JKT 2023

Image
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma Jeshi la Kujenga Taifa JKT limewataka vijana wote  kutoka Tanzania Bara na Visiwani wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga taifa JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2023 huku likibainisha kuwa vijana wenye taaluma ya Uhandisi Ujenzi, Ufugaji, Uvuvi, Saikolojia na wanyamapori watapewa kipaumbele. JKT pia limesisitiza kuwa nafasi hizo haziuzwi na waombaji wasirubuniwe na mtu yeyote kwa kumpa fedha ili kufanikisha yeye kupata nafasi za kujiunga na JKT. Akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema usaili utaanza Agosti 28, 2023 kupitia Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani. “Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fulsa kuja kujiunga ili kujengewa uzalendo, Umoja wa kitaifa, Ukakamavu, kufundishwa stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao” a

Shughuli ya Azam FC na Fei toto wao Imeisha Vibaya, Watolewa Shirikisho

Image
Azam FC imetolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) hatua ya awali na klabu ya Bahir Dar Kenema ya Ethiopia kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar. Mechi ya kwanza Ethiopia Bahir ilishinda mabao 2-1 na leo Azam ikiwa nyumbani ilishinda mabao 2-1 hivyo kufanya matokeo ya jumla 3-3. spoti Bahir Dar Kenema inatinga hatua ya kwanza CAFCC na mshindi atatinga hatua ya makundi. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/qArs0b3 via IFTTT

Mchezo wa Bahati na Sibu ulivyonitajirisha na Kubadilisha Maisha yangu

Image
  Frank ndilo jina langu mtoto wa kwanza kwenye familia yetu ya waliosoma, mimi tu ndiye niliyekataa shule mapema wenzangu wote ni wasomi tena waliofanikiwa na wenye kazi nzuri maishani mwao.Kazi yangu kubwa ni kuuza makava ya simu mtaji wenyewe nilipewa na wadogo zangu angalau na mimi nijitafute kidogokidogo huko, mchana nilifanya kazi hiyo lakini kila jioni nilitembelea kwenye mabanda ya casino hususani meridian bet kutafuta bahati yangu huko. Nimejifunza kucheza mchezo huu wa bahati nasibu kuanzia nikiwa mwenye umri wa miaka kumi na nane mara tu baada ya kuacha shule.Nimecheza mara nyingi sana na kila nilipokuwa ninajaribu niliishia kuambulia pesa za nauli tu na vichenji vidovidogo.Kabla ya msaada nilioupata kutoka kwa daktari bingwa BAKONGWA hapo nyuma sikuwahi kupata pesa ya maana ya kufanyia lolote katika shughuli zangu za kubet –ninakumbuka pesa kubwa ambayo niliwahi kushinda ilikuwa ni laki nne na nusu tu pesa ambayo haifikiia hata kwenye mtaji ambao wadogo zangu walinip

Kaizer Chiefs Waanza Kujuta Kwa Kumkataa Kocha Nabi, Wachapwa Kila Kona

Image
  Msimu wa soka wa 2023-2024 umekuwa na changamoto kubwa kwa Kaizer Chiefs chini ya uongozi wa kocha Molefi Ntseki. Hadi sasa, Ntseki amekuwa na kibarua kigumu na hajashinda mchezo wowote tangu kuanza kwa msimu huu. Hii ni hali isiyofurahisha kwa mashabiki wa klabu hiyo. Kaizer Chiefs, chini ya uongozi wa Molefi Ntseki na msaidizi wake Arthur Zwane, wamejikuta katika nafasi ya 13 kati ya timu 16 katika ligi. Timu hiyo imecheza mechi tatu, ikipoteza mara mbili na kutoa sare moja. Hali hii inaashiria mwanzo wa msimu wa kusuasua ambao umewashangaza wengi. Juzi, Kaizer Chiefs ilikuwa ugenini dhidi ya Ts Galaxy na kushuhudia kipigo kikali cha bao 1-0. Kupoteza kwa mchezo huo kumewakasirisha sana mashabiki wa Amakhosi. Hii ilikuwa ni pigo lingine katika safu ya matokeo mabaya chini ya uongozi wa Ntseki. Kutokana na mwenendo huu wa timu, mashabiki wa Kaizer Chiefs wameanzisha vuguvugu la kutaka kufanyika kwa mabadiliko makubwa. Wamehoji ufanisi wa Molefi Ntseki kama kocha na hata k