Tabia za watu wenye usaliti katika mahusiano ya kimapenzi
Usaliti ni jambo baya sana katika mahusiano, usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja. Wanajiona wamefanikiwa pale ambapo wanasaliti na wenza wao kutogundua kama wanasalitiwa. Siku zote anaesaliti huwa anajiona mjanja kwamba yeye anasaliti wakati mwenzake hasaliti. Kwa asilimia kubwa wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao, wanataka wao wasaliti lakini wapenzi wao wasithubutu kusaliti. kwanini hawataki wenzi wao wasaliti? Eti wanaumia, hakuna kitu kinacho mchukiza mwanaume kama kusalitiwa. Kusaliti asaliti yeye, akisaliti mwenzake ni kosa la jinai anaona amedhalilishwa. Anajisikia fedheha kwamba mpenzi wake amemuonaje? Amemchukuliaje? Hajakamilika idara gani? Anawaza sana na kujiuliza jamii nzima inayojua kitendo hichoitamtazamaje? Hapo ndio unakuta mwanaume anaamua kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo hata kuhatarisha maisha ya mwenza wake. Zifuatazo ni dalili za usaliti: Kutopenda kuchimbwa. Mara nyingi anaesaliti huwa hapendi kuchimbwa mambo kwa undani, ana...