Posts

Showing posts from October, 2023

Ratiba Mechi za Leo Ligi Mbali Mbali Duniani

Image
 RATIBA YA LEO JUMATANO AFRICAN Football League 18:00 - Esparance Vs Wydad 21:00 - Al Ahly Vs Mamelodi NBC Premier League 🇹🇿 14:00 - Singida F.G F.C Vs Ihefu FC 🇹🇿 16:00 - Mashujaa FC Vs Azam FC 🇹🇿 19:00 - Coatal Union Vs Namungo FC 🏆 CARABAO CUP 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 22:30 - West Ham United Vs Arsenal 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 22:45 - Bournemouth Vs Liverpool 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 22:45 - Blackburn Vs Chelsea 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 22:45 - Everton Vs Burnley 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 22:45 - Ipswich Vs Fulham 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 23:15 - Man United Vs Newcastle United 🏆 COPA DEL REY 🇪🇸 14:00 - Lugones Vs Rayo Vallecano 🇪🇸 14:00 - Roque de Lepe Vs Girona 🇪🇸 14:00 - Badalona Vs Cadiz 🇪🇸 17:30 - Quintanar Vs Sevilla 🇪🇸 17:30 - Yuregano CF Vs Celta Vigo 🇪🇸 20:30 - Bunol Vs Real Sociaded 🇪🇸 20:30 - CD Boiro Vs Mallorca 🇪🇸 20:30 - CF Tardienta Vs Getafe 🇪🇸 22:30 - Cortes Vs Real Betis 🇪🇸 23:30 - UE Rubi Vs Athletic Club 🏆 DFB POKAL 🇩🇪 20:00 - Dortmund Vs Hoffenheim 🇩🇪 20:30 -

Kocha Pitso Mosimane apewa "Thank You" Al Wahda, Kisa Matokeo Mabaya

Image
Uongozi wa klabu ya Al Wahda umemfuta kazi kocha wake mkuu, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini kufuatia mwenendo usioridhisha wa matokeo katika klabu hiyo iliyopo ligi kuu ya Falme za Kiarabu (UAE), Hapo jana klabu hiyo ilipokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Shabab Al Ahli Klabu ya Al Wahda sasa inakamata nafasi ya 6 ikiwa na alama 9 latika ligi kuu nchini humo. Unadhani Pitso anafaa kuja Timu gani hapa Bongo? Tupe maoni yako from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/tqDxBYX via IFTTT

TMA yasisitiza uwepo wa El Nino, yatabiri mvua kubwa mikoa 15TMA yasisitiza uwepo wa El Nino, yatabiri mvua kubwa mikoa 15

Image
MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesisitiza uwepo wa mvua za El Nino na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kukabiliana na athari zinazoweza kutokea. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chan'ga. Aidha TMA leo  imetoa utabiri wa uwepo wa mvua za wastani mpaka juu ya wastani kwa mikoa inayopata mvua mara moja kwa mwaka ambayo ni Kigoma, Rukwa, Katavi, Tabora, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara, Ruvuma na  eneo la  Kusini mwa Mkoa wa Morogoro. Akizungumza wakati akitoa utabiri huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chan'ga amesema katika kipindi cha nusu ya msimu (Novemba 2023 hadi Januari, 2024) kinatarajiwa kuwa na mvua nyingi ukilinganisha na nusu ya pili (Februari hadi Aprili 2024), uwepo wa El-Niño unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mvua za msimu. Dk. Chang’a amebainisha athari zinazoweza kujitokeza ikiwa ni vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji w

Mwanamuziki Akon Ajibu Tuhuma za Kumbaka Binti wa Miaka 13

Image
  Baada ya mtayarishaji mkongwe wa muziki kutoka nchini Marekani Suge Knight kudai kuwa mwanamuziki na mfanyabiashara #Akon aliwahi kumbaka binti wa miaka 13, hatimaye, muimbaji huyo amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na jambo hilo Kufuatia mtando wa #X wa #Akon ameandika kuwa “Ulimwengu unafahamu uongo pale tu wanapo usikia, inahudhunisha, kudhalilisha na kutia aibu sana bila kujali historia yetu lakini bado nitaendelea kumuombea” Suge Knight, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 28 jela kwa kuua bila kukusudia, aliyasema hayo kupitia Podcast mpya ya ‘Collect Calls’ ambayo imezinduliwa na #Knight kutoka gerezani. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/J7HL42P via IFTTT

Lionel Messi Mchezaji Bora wa Dunia Ballon d’Or

Image
Staa wa Inter Miami na Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi amefanikiwa kumshinda Erling na kushinda tuzo yake ya nane ya Mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or. Hii inakuwa ni tuzo yake ya nane, Messi amewahi kuchukua Ballon d’Or katika miaka 2009, 2010, 2011, 2012, 2015, 2019 na 2021. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/2aKN3n7 via IFTTT

Ahmed Ally Akubali Mziki wa Yanga, Adai Wamekamilika Idara zote

Image
"Tunakwenda kucheza mechi ngumu kwelikweli, tunakwenda kukutana na mpinzani mgumu kwelikweli, mpinzani ambae amekamilika idara zote, mpinzani ambae yupo fiti kwa asilimia 100, ni mechi ambayo Wanasimba tunapaswa kujitoa muhanga kwelikweli kuweza kupata matokeo" ~ @ahmedally_ Afisa Habari na Mawasiliano wa Simba SC from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/qUP6vGh via IFTTT

Azam FC Wafanya Maamuzi Magumu KISA Kuzomewa Kwa Fei Toto

Image
Zomea zomea ya mashabiki katika Uwanja wa Azam Complex imeifanya klabu hiyo kusitisha kuingia bure katika michezo yao. Tangu Ligi Kuu imeanza mashabiki walikuwa wakipewa ofa ya kuingia uwanjani bure ili kuisapoti timu hiyo, lakini mambo hayakuwa hivyo na ndipo mabosi wakaamua kuondoa utaratibu huo. Kuanzia mchezo wa juzi dhidi ya Namungo ambao wenyeji Azam FC walilala kwa mabao 3-1, mashabiki walioingia walilipia kiingilio cha chini cha Sh3,000. Habari ambazo Mwanaspoti lilipenyezewa ni kwamba uongozi haukufurahishwa na tabia ambayo ilionekana kuwatoa mchezoni wachezaji wanaopambana mwanzo hadi mwisho kupata matokeo badala ya kuwasapoti. “Sasa hivi hakuna tena huo utaratibu mtu unaingia bure halafu unamzomea aliyekufanya uingie bure. Siyo poa hata kidogo tukaona isiwe shida ingia kwa kiingilio chako uzomee vizuri,” kilisema chanzo chetu. Kilisema baada ya kuona hivyo awali uongozi ulivumilia, lakini subira zimeshindwa kuleta matunda na ndio maana wakaamua kufanya uamuzi wa kuond

TANZIA: Mjukuu wa Nyeyere afariki katika ajali Arusha

Image
  Mjukuu wa Mwalimu Nyerere Daudi Makongoro Nyerer, ambaye ni mtoto wa pili wa Makongoro Nyerere, RC wa Rukwa amefariki dunia. Amefariki kwa ajali ya gari Arusha jana mchana, Baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na Lori. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/AVYeS3D via IFTTT

Kiungo mshambuliaji wa Yanga STEPHANIE AZIZI KI ameigomea timu hiyo Kuongeza mkataba

Image
Kiungo mshambuliaji wa Yanga STEPHANIE AZIZI KI ameigomea timu hiyo Kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ya pale Jangwani ikumbukwe Mchezaji huyo alisajiliwa na Yanga tarehe 24/08/2022 akitokea Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast ambapo alimaliza msimu akiwa na timu hiyo kama mchezaji bora wa msimu wa ligi kuu nchini humo mara baada ya kutua yanga alisaini kandarasi ya miaka 2 kuitumikia timu hiyo kwa mshahara wa milioni 27 kwa mwezi na ada ya uhamisho wa dola laki mbili na nusu. Baada ya kuwa na msimu mzuri kwa kumaliza na mabao 10 na assist 7 msimu uliopita kisha kuanza vyema msimu huu mpaka sasa ana goli 6 na assist 7 uongozi wa Yanga ulianza mazungumzo tangu Jana ya kumboreshea maslahi na kutaka kumuongezea mkataba tena wa miaka miwili ili asalie jangwani hapo hadi 2026 mchezaji huyo amegoma kuhusu jambo hilo la kuongeza mkataba jambo ambalo limewafanya viongozi wa Yanga kukuna kichwa na kuwapa wasi wasi na hofu kubwa na kisha kujiuliza je anataka kwenda timu gani m

Baba Amnyonga Mwanaye Kwa Kamba Ya Viatu Na Kupiga Naye Selfie – Aacha Ujumbe Mzito

Image
  Mkazi wa Mtaa wa Kota, Kata ya Mlandege Mkoani Iringa, Goodluck Mgovano aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 33 anadaiwa kumuua Mtoto wake Alvini Mgovano mwenye umri wa miaka minne kwa kumnyonga na kamba ya viatu huku akijirekodi kwa simu yake ya mkononi wakati akimnyonga Mtoto na alipomaliza akapiga selfie na mwili wa Mtoto na kuacha ujumbe ulioelekeza wapi Mtoto huyo azikiwe. Kwa mujibu wa taarifa za Majirani Goodluck alijifungia ndani na Mtoto wake na kumnyonga nyuma ya mlango kwa kutumia kamba ya viatu huku akirekodi tukio hilo kwa simu yake ya mkononi na baada ya hapo alimlaza kitandani na kupiga nae tena picha (Selfie) na kutokomea kusikojulikana na bado anatafutwa “Simu yake yenye picha na video aliiacha hapohapo nyumbani na kwa sasa ipo mikononi mwa Polisi” Mtuhumiwa aliacha ujumbe uliosema “Chanzo cha mauaji haya ni ugomvi uliotokea kati yangu Mimi na Mke wangu mnamo Oktoba 6, 2023 na mimi naenda kujiua na nataka mimi na Mwanangu tuzikwe Kijiji cha Itendulinyi” Diwan

Zifahamu kampuni bora za simu Duniani kwa 2021

Image
1: SAMSUNG • Ni kampuni ya vifaa umeme iliyopo Korea Kusini. Wana shika nafasi ya 1 kutokana na ubora wa simu zao kama; Galaxy S20, Galaxy S11, Note 10 n.k. 2: HUAWEI • Hii ni kampuni kutoka China waanzilishi wa teknolojia ya 5G. Wana matoleo MaTaTa ya simu kama; Huawei P30 Pro, Mate X, Mate 20 Pro n.k. Pato lao ni $ 121.71 kwa mwaka 3: APPLE iPHONE • Hii ni kampuni kutoka Marekani ambayo ina mfumo wake wa kipekee wa kuendesha simu zao iOS. Wana simu kama; iPhone 11 Pro, iPhone X, iPhone XR n.k. Pato lao ni $33.3 kwa robo ya mwaka. 4: XIAOMI (MI) • Hii ni kampuni nyingine kutoka China. MI inasimama badala ya Mobile Internet, wamewekeza kwenye simu, Tv, Viatu n.k. Wana simu kama; Xiaomi Mi9, Xiaomi 8 Pro, Mi Mix 3 n.k. Pato ni $ 494 kwa theluthi ya mwaka. 5: OPPO • Hii ni kampuni nyingine kutoka China ilianzishwa mwaka 2016. Ipo pamoja na Vivo, One plus na Realme. Wana simu kama; Oppo A31, F15, A5, A9 n.k. 6: VIVO • Hii ni kampuni nyingine kutoka China ilianzishwa mwaka 2011

Azam FC Pamoja na Fei Toto Wao Wapokea Kichapo Cha Nguvu Kutoka Kwa Namungo

Image
  Azam FC Pamoja na Fei Toto Wao Wapokea Kichapo Cha Nguvu Kutoka Kwa Namungo Namungo FC kwa mara ya kwanza jana Oktoba 27, 2023 walipata ushindi wa kwanza dhidi ya Azam FC kwa kuitandika 3-1. Namungo walianza kupata goli la kwanza dakika za mapema kabisa za mchezo kupitia kwa Buswita dakika ya 10 na dakika ya 19 wakaweka chuma ya pili kupitia kwa Manyanya kisha dakika ya 50 wakaweka mchi wa tatu kupitia kwa Lusajo. Bao la kufutia machozi la Azam lilifungwa na Ayubu Lyanga dakika ya 70 ya mchezo. Namungo wametoka mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu hadi kushika nafasi ya 12 wakifikisha alama 6 baada ya kucheza michezo saba. Wamepata sare michezo mitatu, wamefungwa mitatu na kushinda mmoja. Kwa upande wao Azam, wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama zao 13. Kinara wa msimamo ni Yanga SC mwenye alama 18 akifuatiwa na Simba mwenye alama 15 akiwa na gepu la michezo miwili kwa Yanga. Simba amechezo michezo mitano, Yanga saba. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Kpf7yqO via IFTTT

Miji miwili ya Misri yashambuliwa kwa makombora

Image
Makombora yamepiga miji ya Taba na Nuweiba iliyoko Bahari ya Sham nchini Misri siku ya Ijumaa, vyanzo na maafisa walisema, na kujeruhi watu sita na kuonyesha hatari ya kuenea kwa mzozo wa kikanda unaotokana na mzozo wa Israel na Gaza. Jeshi la Israeli limelilaumu "tishio la anga" katika eneo la Bahari ya Sham: ikielezea uwezekano huo kufanywa na wanaharakati wa kundi la Wahouthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran ambalo linajulikana kwa kutumia ndege zisizo na rubani. Msemaji wa jeshi la Misri Kanali Gharib Abdel-Hafez alisema "Drone isiyojulikana" ilianguka kwenye jengo lililo karibu na hospitali na kuwajeruhi watu sita katika mji wa Taba ulio kwenye mpaka na Israel, majira ya asubuhi. Baadaye, kombora jingine lilidondoka karibu na kiwanda cha umeme kilichopo katika eneo la jangwani katika mji wa Nuweiba ulioko takriban kilomita 70 kutoka mpakani, vyanzo viwili vya usalama vya Misri vililiambia shirika la habari la Reuters, na kuongeza kuwa bado wanakusan

Mwanamuziki Phina Amjibu Fahyma ishu ya Kuhusudu Wanaume Kupenda Wanawake Weupe

Image
  Msanii wa kike kutoka Tanzania, Saraphina maarufu kama Phina amemjia juu mpenzi wa Rayvanny, Fahyvanny kwa kauli yake kuwapikia upato warembo wenye rangi nyeupe za ngozi kupata mapenzi ya wanaume mara dufu ikilinganishwa na wenzao weusi. Phina alitoa tamko la kumjibu saa chache tu baada ya Fahyvanny kudai kwamba ukweli ni kwamab wanaume wengi hata ndani ya nafsi zao wakiulizwa kuchora taswira ya wanawake wanaowawazia kuwaoa au kutoka nao kimapenzi basi sharti wataje weupe wa ngozi. Kwa mujibu wa Phina, rangi ya ngozi nyeupe haina thamani yoyote kwani siku hizi warembo wengi huinunua katika maduka ya vipodozi lakini ngozi nyeusi huwezi kuipata popote kwa hiyo nit ya bei ghali kuliko vile ambavyo wengi wanafikiria. “Ngozi nyeusi wewe ni expensive asikuambie mtu. Kwa sababu huwezi kuipata dukani unaitolea wapi? Rangi nyeupe watu wananunua, lakini nyeusi ushawahi kuona wapi wewe ikiuzwa? Kwa hiyo maanake ni kitu ambacho kiko priceless,” Phina alisema. Mrembo huyo alikwenda mbele

Tanzania Kimpira Tuko Vizuri: Twiga Stars Yaichapa Botswana Kufuzu Mashindano ya Olimpiki 2024

Image
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana katika mechi ya kufuzu mashindano ya Olimpiki 2024. Mabao ya Tanzania yamefungwa na Oppah Clement na Aisha Masaka na sasa mechi ya marudiano itapigwa Oktoba 31 nchini Botswana. Twiga Stars imeanzia hatua ya pili ya mtoano katika mashindano hayo baada ya timu ya Congo Brazavile kujitoa na ikipenya itaingia raundi ya tatu ambapo atakutana na mshindi wa mechi ya DR Congo vs Afrika Kusini. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/0CyxnHN via IFTTT

Amber Lulu Atoa Mpya: Nikiwa Mkubwa Natamani Kuwa Kama Zuchu

Image
  Msanii wa Bongo Flava Amber Lulu amesema kuwa anampenda sana Zuchu na anatamani akiwa mkubwa awe kama yeye. Kupitia insta story yake Amber ameandika; "Nikiwa mkubwa nataka kuwa kama Zuchu, nampenda huyu msichana jamani uwii from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/GxNKaMP via IFTTT

Masharti Ya Kumtext Mwanamke - Makosa 5 Wanaume Wanayofanya

Image
Kila siku mara moja au nyingine huwa tunawatext wanawake. Aidha wawe ni wapenzi wetu, tunaowatongoza ama marafiki zetu. Na kila siku huwa tunapatwa na changamoto mbalimbali kutokana na matangamano yetu. So huwa kunakosekana nini? Ifuatayo ni orodha ya mambo 5 makuu ambayo wanaume wengi hukosea wakati wanapomtext mwanamke, na jinsi ya kutatua. #1 kukata tamaa mapema kwa mwanamke Kosa kuu ambalo wanaume wengi hufanya ni kukata tamaa mapema wakati wanapomtext mwanamke. Watamtext mwanamke, na kama hatajibu jumbe zake (ama kujibu kiuchache) watachukulia kuwa mwanamke huyu amepoteza interest na wanakata tamaa. Hili ni kosa kuu sana. Kama inavyojulikana kikawaida ni kuwa mwanamke anaweza kutojibu meseji zako, na sababu hizo hazina uhusiano moja kwa moja na kutokuwa na interest kwako. Kwa mfano, anawezakuwa labda yuko busy, katika mood mbaya, ama labda hayuko sure ni kitu gani cha kukujibu kwa meseji. Kiufupi ni kuwa haujui kile ambacho kinazunguka kwa akili ya mwanamke, so haina haja y

Kauli Kwanza ya Paul Makonda Baada ya Kukabithiwa Ofisi Lumumba Leo

Image
Makonda “Nitafanya kazi kwa uaminifu nisimuabishe Mungu na M/Kiti wa Chama kwa kupeleka jina langu” Katibu Mwenezi wa Itikadi wa CCM @baba_keagan amekabidhiwa ofisi na kuzungumza kuhusu majuhukumu yake mpya huku akisema atakuwa mwaminifu ili asimuangushe Mungu pamoja na Mwenyekiti wa Chama Rais Samia Hassan Suluhu. Makonda amesema atajifunza kwa viongozi waliomtangulia kama Shaka, Sophia Mjema pamoja na Nape Nnauye ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake hayo mapya ndani ya siasa. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/GDchks1 via IFTTT

S2Kizzy athibitisha kufanya ngoma na Rihanna "Soon itatoka"

Image
Mtayarishaji wa muziki Bongo, S2Kizzy amethibitisha kufanya kazi na Rihanna na kusema wimbo huo ukiwa tayari watu watausikia. Miezi michache iliyopita, S2kizzy alisema kwamba yeye ndiye mtu wa kwanza kuwahi kutokea kutoka ukanda wa Afrika mashariki kushiriki katika mradi mmoja na staa kutoka Barbados, Rihanna. Producer huyo baadaye alihariri ujumbe huo na kutoa jina la Rihanna ambapo aliweka emoji za mduara wa dunia badala yake, na hili limewatatanisha watu wengi kushindwa kuelewa alichokuwa akimaanishi awali kwa kuweka jina la Rihanna. “Mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa katika kazi ya msanii Rihanna,” ujumbe wa kwanza kabla kuhariri ulisoma. “Mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa katika project hiyo,” ujumbe wa pili baada ya kuhariri ulisoma. Baada ya kuliondoa jina la Rihanna kwenye post yake hiyo, wengi wamesema labda ni kiki tu alikuwa anatafuta kwa kujizolea uhodari kwa kuwa wengi wanamjua Rihanna kama msanii wa kimataifa anayetamba mno. Je, wewe unahi

Kocha Gamondi Afunguka Haya Kuhusu Mchezo wa Yanga na Singida Fountain Gate

Image
  Kocha Mkuu wa Kikosi cha Yanga, Miguel Gamondi, amezungumzia mipango yake kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate. Mchezo huo umepangwa kuchezwa Ijumaa ya Oktoba 27, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa 12:30 jioni. Akizungumzia mchezo huo, Gamondi amesema, wachezaji walitumia nguvu kubwa katika mchezo uliopita tulioshinda magoli 3-2 dhidi ya Azam, hivyo anatumia siku tatu za maandalizi kuwaweka sawa wachezaji ili kuendelea na malengo ya kukusanya alama tatu. “Tumetoka kucheza mechi ngumu sana dhidi ya Azam, wachezaji walitumia nguvu kubwa, tunajaribu kuwa na mazoezi mazuri ndani ya siku tatu hizi kuona utimamu wao umefikia wapi. “Siwezi kusema kama kutakuwa na mabadiliko ya kikosi, hilo litategemea sana tutakachokiona mazoezini. Mechi ya Singida ni ngumu na tunahitaji kuingia kamili ili kuweza kupata pointi tatu,” alisema Gamondi. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/kRuXPSw via IFTTT

CCM yasimamisha viongozi tuhuma kukihujumu chama

Image
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Rukwa kimewasimamisha uongozi viongozi wa chama hicho wanaotuhumiwa kukihujumu kwa kuwauzia kadi za kielektroniki viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili wazitumie katika mikakati yao ya kisiasa. Akitoa taarifa hiyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Godfrey Mwanisawa, alisema viongozi hao walikuwa wakichukua kadi za wanachama na kumuuzia Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Rukwa, Sadrick Malila, maarufu kwa jina la Ikuwo ili atangaze kuwa wanachama hao wamehamia CHADEMA na wamerudisha kadi za CCM. Alisema baadhi ya kadi hizo ni ya aliyekuwa mwana CCM mkongwe marehemu Chrisant Mzindakaya pia marehemu Zuberi Kauzeni ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi tawi la King’ombe Kata ya Majengo pamoja na kadi za wanachama waliohama mkoani Rukwa. Alisema kuwa baadhi ya viongozi wa CCM waliokuwa wakiuza kadi hizo ni Chriss Mwalwanda ambaye ni Katibu Kata ya Majengo, Alexander Kasongo Katibu wa Siasa na Uenezi Kata ya Maje

Mjane wa Marehemu Augustino Lyatonga Mrema Kunufaika na Mali Alizoacha Marehemu

Image
Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke kimetoa uamuzi juu ya urithi wa mali za marehemu Augustino Lyatonga Mrema ambapo imemtaja mjane wa Mremba Doris kuwa mnufaika wa mirathi hiyo. Uamuzi huo umetolewa tarehe Oktoba 20, 2023 na Jaji Augustine Rwizile ambapo ameeleza kuwa Peter Mrema ndiye msimamizi pekee wa mali zilizoachwa na marehemu Mrema huku mjane wake akikataliwa kuwa msimamizi wa mali hizo. Katika uamuzi huo umewaorodhesha watu tisa watakaonufaika ambao ni pamoja na Doris Agness Augustin Mkandala (45) ambaye ndiye mjane wa Mrema, Elizabeth Augustino Mrema (52), Mary Augustino Mrema (48), Cresencia Augustino Mrema (45), Elizabeth Augustino Mrema (43), Michael Augustino Mrema (40), Edward Augustino Mrema (38), Peter Augustino Mrema (37), na Godlove Augustino Mrema (18). from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/4R36og0 via IFTTT

Mange Kimambi "Nimeongea na Hamisa Mobetto Amekubali Kupima DNA Hadharani"

Image
Mange Kimambi Afunguka haya: "Mimi ndio dada yenu wa taifa na sijawahi kuwaangusha. Hili jambo la Dylan, Hamisa na Diamond nitahakikisha mnaujua ukweli. . Kwa vile kelele zimekuwa nyingi eapecially baada ya ile posti nikisema kuwa Dylan ni mtoto wa Dai wengi mlisema kuwa Hamisa akarudie tena hiyo DNA anayoitaka Diamond. Mimi kama dada wa taifa nimeongea na Hamisa leo na nimemuuliza kama yuko tayari wakarudie tena DNA ili Diamond ajifurahishe roho yake, alichojibu Hamisa ni kwamba, yeye kama Hamisa ameshakubaliana na hali kuwa Diamond kaamua tu hamtaki mtoto, ameshakubali kulea mwenyewe, na ameshamwachia Mungu. Hamisa anasema amemkabidhi mtoto wake kwa Mungu, Mungu ndio atakaemlelea mtoto wake na anasema kuna sababu Mungu kamwinua kimaisha ni ili aweze kumlea mwanae bila kupigizana kelele na baba mtu. . Nikamwambia Hamisa hapana, hili jambo sasa hivi limekuwa lakitaifa ndio umemwachia Mungu ila for the sake of your fans una obligation ya kukubali hii DNA irudiwe. Hamisa al

Hamas Yaachilia Mateka Wengine wa Israel

Image
Hamas, Jumatatu iliachilia mateka zaidi ambapo wanawake wawili vikongwe wa Israeli, waliachiliwa wakati Israeli ikiimarisha mashambulizi yake ya anga Gaza. Hayo yakiendelea Marekani, imeonyesha kuwa na wasiwasi kuhusu vita vya Israel na Hamas kwamba vinazidi kuwa vita vya mashariki ya kati. Katika taarifa, Hamas, imesema iliwaachilia mateka hao kwa sababu za kibinadamu. Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu ilisema iliwasafirisha wanawake wa Israel, wenye umri wa miaka 85 na 79 kutoka Gaza Jumatatu jioni hadi Tel Aviv. Kundi hilo la wanamgambo liliwaaachilia mateka wake wawili wa kwanza mama na bintiye wa Kimarekani, Ijumaa, ikiwa karibu ni wiki mbili baada ya kufanyika shambulizi la kushtukiza Israeli, na kuuwa zaidi ya watu 1,400, wengi wao wakiwa raia, na kuwakamata mateka zaidi ya 200 wengine. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/TXL1vrM via IFTTT

AJALI: Bweni la Sekondati ya Umwani lateketea kwa moto

Image
  Bweni lililokuwa linatumiwa na wanafunzi zaidi ya 240 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Umwani iliyopo Manispaa ya Bukoba, limeteketea kwa moto usiku huu. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/aRr7xBh via IFTTT

Mkurugenzi TPA: Mkata wa Bandari Utakuwa na Ukomo wa Miaka 30, sio 100

Image
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema mkataba wa uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam utakuwa wa miaka 30 na sio 100 kama ambavyo ilikuwa ikisemwa awali. Mbossa ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 22, 2023 katika hafla ya utiaji saini wa mikataba mahususi mitatu ya uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam Ikulu ya Chamwino, Dodoma. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/s2o9qma via IFTTT

Zari The Bosslady Apost Picha ya Pamoja ya Tiffah, Nillan na Naseeb Jr na Kuandika haya

Image
  Zari The Bosslady apost picha ya pamoja ya Tiffah, Nillan na Naseeb Jr na kuandika haya VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/ETAjNZK via IFTTT

Chanzo cha Ajali ya Basi na Lori iliyouwa Watu 18 Mkoani Tabora

Image
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amesema chanzo cha ajali ya Basi kugongana na Lori na kupelekea vifo vya watu 18 ni uzembe wa Dereva wa lori kujaribu kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari. Amesema, basi la kampuni ya Alfa lilikuwa likitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam na liligongana uso kwa uso na Lori la mafuta la kampuni ya GBP katika Kijiji cha Undomo Wilayani Nzega Mkoani Tabora. Kamanda Abwao amesema waliofariki ni wanaume 13, wanawake 5 na wengine 36 wamejeruhiwa, idadi ambayo inajumuisha watoto wadogo ambao miili yao imehifadhiwa na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega. Awali, Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu – LATRA, Nelson Mmari alisema abiria waliopanda basi hilo ni 49, huku Serikali ikifanya jitihada za matibabu kwa majeruhi. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/GExyLoz via IFTTT

Billnass kumlipia faini Ally Kamwe TFF

Image
  Msanii wa muziki Bongo Fleva ambaye pia ni mfanyabiashara na shabiki kindakindaki wa Klabu ya Yanga, William Lyimo maarufu kama Billnass amesema atalipa faini ambayo Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe amepigwa na Bodi ya Ligi. Kamwe amepigwa faini ya Tsh million moja na Kamati ya Bodi ya Ligi kwa madai ya kumdhalilisha mwamuzi, Tatu Maologo mtandaoni. Kupitia mtandao wa Instagram baada ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Singida FG FC na Simba Sc ambapo Simba ilishinda kwa bao 2-1, Kamwe alipost picha ya mwamuzi Tatu Malogo kisha akaiwekea wimbo wa Billnass uitwao 'Maokoto' jambo lililotafsriwa kuwa mwamuzi huyo kuhusishwa na kupokea rushwa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Billnass ameandika; "Pole sana (Ally Kamwe). Ila sisi kama Nenga Tronics kwa kidogo tulichojaaliwa tunaomba tumalize sisi (faini) japo tunajua (faini) iko ndani ya uwezo wako. Lakini najua MAOKOTO ni wimbo wako pendwa," amesema Billnass. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/E5TMAmg vi

Fabrice Ngoma Man of the Match Simba Vs Al Ahly

Image
Ile namba 6 iliyonyakuliwa pale AIRPORT sio Mwalimu wa Viungo kweli . Ligi yetu imebarikiwa kuwa na Mwalimu wa Viungo,Fabrice Ngoma Luamba. Kiungo aliyajaliwa nidhamu ya hali ya juu akiwa Uwanjani,huwezi kuona akipata adhabu za kadi ama madhambi ya hatari. Fabrice Ngoma Timu ikiwa inashumbuliwa amekua msaada mkubwa kwa Mnyama katika kurudi chini kabisa katika kuzuia na kuziba nafasi. Wakati yupo na mpira anakua na utulivu wa hali ya juu,pasi yake,hapotezi mipira "kizembe". UTULIVU MKUBWA!KAZI YA KUTOSHA!WHAT A PLAYER. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/9eTFdOI via IFTTT

Simba Yakaza Hasa Kulinda Heshima ya Taifa, Yatoka Sare na Waarabu Al Ahly Kwa Mkapa

Image
KLABU ya Simba imefanikiwa kutoka sare ya 2-2 katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya timu ya Al Ahly ya nchini Misri katika mchezo wa robo fainali Michuano ya African Football League. Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa ufunguzi, Al Ahly ilifanikiwa kupata bao kipindi cha kwanza kabla ya mapumziko kupitia kwa mshambuliaji wao Reda Slim na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 1-0. Simba Sc ilirudi kipindi cha pili wakiwa na hali mpya kwani walitawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kibu Denis dakika ya 53 ya Mchezo. Kocha wa Simba Sc alifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji kipindi hicho cha pili, mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwani baada ya kuingia Sadio Kanoute alifanikiwa kupachika bao zuri na kuwafanya Simba kuwa mbele 2-1. Dakika tatu baadae Al Ahly walisawazisha kupitia kwa nyota wao Karhaba dakika ya 63 ya mchezo. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/AeWOJXy via IFTTT

Al Ahly Vs Simba Sc ni Maalum Kwa Ajili ya Palestina

Image
  Klabu ya Al-Ahly imetangaza kuwa, mchezo wao wa marudiano wa AFL dhidi ya Simba SC utakaochezwa Egypt wameu-dedicate kwa nchi ya Palestina. Wamewataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi Jumanne 24 October 2023 kwa sababu kiingilio cha mchezo huo watakipeleka Nchini Palestine kusaidia wahanga wa vita inayoendelea dhidi ya Israel. Wamewataarifu mashabiki wao kuwa ujio wao uwanjani ni mchango wao kwenda Nchi takatifu ya Kiislamu ya Palestina. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/zlwUhQs via IFTTT

ONGEZA UUME, HAMU YA TENDO NA NGUVU ZA KIUME.

Image
Upungufu wa nguvu za kiume, kukosa hamu ya tendo au maumbile madogo husababisha mwanaume kushindwa kujiamini katika tendo.          DALILI NI KAMA:-  1.kukosa hamu ya tendo 2.Kuwahi kufika kileleni 3.Kushindwa kurudia tendo 4.Dhakari kusinyaa katika ya tendo 5.Kuchoka sana baada ya raundi moja 6.Dhakari kusimama kwa ulegevu          TIBA SAHIHI:- 1.GING SENG PILLS @240,000/= >Hivi ni vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza hamu na nguvu za kiume hata kwa wenye kisukari 2.MAX MAN GEL @240,000/= >Hii uongeza dhakari kwa inch 5-7 3.VIGRX OIL @220,000/= >Huongeza dhakari kwa inchi 6-7 4.MAX MAN, VIMAX @270,000/= >Huongeza dhakari, nguvu na kuimalisha misuli kwa walioathiliwa na kujichua  5.HANDSOME UP @270,000/= >Mashine hii uongeza dhakari kwa size unayotaka pamoja na kuimalisha misuli 6.VIGA SPRAY @180,000/= >Huchelesha kufika kileleni na kuongeza parfomance Fuatilia huduma na vipindi vyetu ktk mitandao ya kijamii ili kupata ushauri na tib

Matokeo Simba vs Al-Ahly Leo 20 October 2023 AFL

Image
  Matokeo Simba vs Al-Ahly Leo 20 October 2023 AFL Matokeo Simba vs Al-Ahly Leo 20 October 2023 AFL, Matokeo ya Simba SC dhidi ya Al ahly today, Simba SC against Al Ahly today Results, Live Score, H2H, how to watch and Kickoffs. Matoke ya Simba dhidi ya Al Ahly leo 20.10.2023 African Football League/Super League Africa. The match between Simba SC and Al Ahly of Egypt is the opening match of the African Premier League (AFL) 2023. This event is important as it officially starts the AFL competition for Africa. The game is scheduled to be played at 6:00 pm at the Benjamin Mkapa Stadium. Simba SC faces this match with hope and a good memory of the match against Al Ahly at the Benjamin Mkapa Stadium. In their previous matches, Simba SC managed to get positive results in both matches. This story adds to the excitement of being the inaugural team of the championship as they aim to create a lasting legacy in this competition. On the other hand, Al Ahly are facing the match with caution,

Kikosi cha Simba vs Al Ahly leo 20 October 2023 Line Up

Image
Kikosi cha Simba SC vs Al Ahly Leo 20/10/2023 Aishi Manula Kapombe Shomari Muhamed Hussein Enock Inonga Che Fondoh Malone Fabrice Ngoma Mzamiru Yassin Clouts Chama Jean Baleke Kibu Denis Luis Miqussion Kikosi cha Simba vs Al Ahly leo 20 October 2023 Line Up, Kikosi cha Yanga sc vs Al Ahly, Kikosi cha Simba vs Al-Ahly,  Kikosi cha Simba dhidi ya Al Ahly leo, Kikosi cha Simba vs Al Ahly,Kikosi Cha Simba Vs Al Ahly Leo October 20 2023 from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/UoAra1S via IFTTT

Habari Njema...Straika Hatari wa Ahly Kuwakosa Simba SC

Image
  Modeste hatakuwa sehemu ya kikosi cha Al Ahly kitakachoondoka kuja Tanzania kuvaana na Simba SC. Modeste alikuwa kwenye mipango ya kocha wa Ahly Marcel Koller lakini cha kusikitisha ni kwamba amepata baridi kali na ndiyo maana atakosa safari ya Tanzania from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/6MjAV3h via IFTTT

Harmonize Afunguka Sababu ya Mashabiki Kuondoka Ukumbini Kwenye Show yake na Sauti Sol

Image
Ameandika ..✍️.. @harmonize_tz ''Tena Kuna Baadhi Ya medias Zimeenda Mbali Hadi Kwenye Show Yangu Last Week Speaking of that!! Nilipangwa Niwe wa Mwisho Kama Ilivyo Jadi. Tena Siku Hizi Nitaanza Kukataa !!! Kumaliza Show Maaana Haya Ndio Malipo Ya Kuwa Mkarim Nimepanda Jukwaani Saa 3:45AM Ukiachilia Matatizo Ya Kiufundi Ambayo siwezi Elezea Zaidi ni Kawaida kutokea!! sautisol is the one Of Best Bands in Africa Walijitahidi Saaana & i Love it kila mtu Alifurahi SWALI JEE NINGEANZA MIMI THEN KONDEGANG WOTE WAKATOKA MLE NDANII WANGEAMSHAJE!!!??? Achilia Mbali Hilo PLAY LIST YANGU ILIANZA NA NYIMBO ZA Slow mwanzoni Zamauwa mengi Kitendo Cha BFF Kuto Tokea Pia Kilinikata Kidogo, MWIJAKU ALIJITAHIDI SANAAA Next time sitowaambia Nimemualika Yeyote Anyways DAR ES SALAAM nawatangazia Show Yakufungia Mwaka Soon !!!!!! NILIKUWA SIJALEWA WALA SILEWI !!!! wakunifanya Nilewe Hayupo Mimi Ni Rafiki Wa Kila Nilie wahi Kuwa Nae Naamini Anamaana Kubwa Kwangu iwe Mbaya Au NZURIIIIIIII'.

Ukweli Mchungu kwa Fei Toto na Jezi ya Taifa Stars

Image
  Kwa sasa kiungo wa klabu ya Azam fc Faisal salum (Feitoto) hana nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya kocha Adel Amrouche. Watu wengi wamekuwa wana jaji kwa nini mchezaji ambaye kwenye Nbc Premier league anashikilia nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora mpaka sasa akiwa nyuma ya Jean Beleke mwenye mabao (5), Fei toto akiwa na mabao (4) ndani ya ligi kuu Tanzania bara Tukumbuke Feisal ni mchezaji anyecheza eneo la kiungo wa kati na pia anaweza kucheza kama kiungo wa kati mshambuliaji, Timu yetu ya Taifa kwa sasa inahitaji zaidi viungo wenye sifa ya kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, Uwezo mkubwa wa kukaba,Uwezo wa kukimbia umbali mrefu uwanjani endapo timu inapokuwa na mpira na pia timu inapokuwa nyuma ya mpira Timu yetu ya taifa kwa sasa inahitaji sana kuwa na viungo kama Mudathiri, Mzamiru, Bajana, Himid Mao, Ambao wanasifa za kutengeneza uwiano mzuri katika eneo la kiungo dhidi ya Mpinzani, Timu kwasasa inahiatahi sana kupata wachezaji w

Serikali Yafunguka Tetesi za Uwepo wa Kiwanda Cha Mayai Goba Dar es Salaam

Image
  Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imekanusha taarifa za uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mayai katika eneo la Goba wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam kama ilivyokuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii  Hatua hiyo imekuja baada ya uwepo wa picha zinazosambaa mitandaoni iliyoambatana na maneno yasemayo, "Serikali hailali kama alivyo shetani halali!! wanajua kabisa kwa sababu shetani halali kwahiyo kuna mambo mabaya atayatenda tu!! kiwanda cha mayai Goba kwa wachina kimekamatwa sasa hayo mayai yote sijui yametagwa na kuku gani? tusubiri yanayojiri, usikie teknolojia ilivyo hapo ndiyo utakapojua kwanini kila mtu ana kitambi,". Aidha Wizara imesema kwamba inawatoa hofu wananchi kuwa imefuatilia suala hilo kwa kina na kujiridhisha kuwa tarifa hizo sio za kweli, ni upotoshaji na hivyo kuitaka jamii kuipuuza. Wizara pia imesema taarifa hizo zimetengenezwa kwa nia ovu ya kuharibu tasnia ya kuku nchini inayokuwa kwa kasi na kwamba katika kufuatilia zaidi, Wi

Mtoto Aliyebambikiwa Kesi ya Mauaji, Akanyongwa Hadi Kufa Kimakosa

Image
  Yapo matukio ambayo ukiyasikia, lazima moyo wako uumie kupita kiasi! Miongoni mwa matukio hayo, ni hili linalomhusu mtoto George Stinney, Mmarekani mweusi ambaye alibambikiwa kesi ya mauaji, akanyongwa lakini miaka kibao baadaye, ikaja kujulikana kwamba alinyongwa kimakosa! VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Zc68Vdx via IFTTT

Ukweli Haupingiki SIMBA Wana Record Nzuri Mashindano ya CAF, Kelele za Yanga Tunasikia Lakini Bado

Image
  Kuna historia nyingine ni ngumu sana kuzivunja. Ni kama hii historia ya Simba na mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Ni historia ya kuvutia sana. Nimeona kelele nyingi sana huko mitaani kwa baadhi ya watu wa Yanga wakijinasibu kuwa, wao ndio wababe kwenye mashindano hayo. Inashangaza sana. Ukweli upo wazi. Simba ndio timu ya kwanza nchini kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya CAF. Ilianza 1974 na inafanya vizuri hadi leo. Mwaka 1974 ilifika nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika (sasa Ligi ya Mabingwa). Ndio rekodi ya kwanza kubwa kwenye mashindano ya Afrika kuwekwa na timu ya Tanzania. Ilikuwa ni kama nyota inayoanza kuangaza kwa Simba. Miaka 19 baadaye ikafika fainali ya Kombe la CAF (michuano iliyoungwanishwa na Kombe la Washindi na kuwa Kombe la Shirikisho Afrika la sasa). Ikawa timu ya kwanza kwa Tanzania kufika fainali ya mashindano hayo. Baada ya Simba kufika fainali mwaka 1993, imechukua miaka 30 kwa timu nyingine ya Tanzania kufika katik

TCRA Haijakataza Matumizi ya VPN

Image
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kwa Mkuu wake wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Rolf Kibaja imesema taarifa kwa Umma iliyotolewa juzi October 13,2023 haijakataza matumizi ya VPN kama baadhi ya Watu wanayopotosha kupitia mitandao ya kijamii. Kibaja amesema kwamba TCRA imetoa utaratibu kwa Watumiaji wa VPN kutoa taarifa za matumizi ya VPN lakini haijazuia matumizi ya VPN “Watu wanaoshiriki kutoa taarifa kuhusu VPN wataendelea na shughuli zao kama kawaida kupitia VPN” Kibaja amesema "Ni muhimu kwa Watumiaji wa VPN kutoa taarifa kwakuwa kusajili huduma ya VPN ni kama kujisajili kwa namba ya simu, Nchi nyingi zilizoendelea duniani zimechukua hatua kama hizi kuimarisha usalama mtandaoni, kama vile Uturuki, India, Belarus, Misri, China, na nchi nyingine” “Ni muhimu kufahamu kuwa matumizi ya VPN nchini hayakatazwi bali yanapewa utaratibu rasmi, kutoa taarifa hizo hakuna gharama yoyote ya malipo na hakuingilli masuala ya faragha wala usalama wa watumi

Feisal Salum Fei Toto Kutua Simba Sports Club, Ataka Afrika Nzima Imjue

Image
Kiungo mshambuliaji wa Azam Fc FEISAL SALUM ABDALLAH FEI TOTO hana furaha ndani ya klabu ya Azam na chanzo cha karibu cha mchezaji huyo kimenithibithia kuwa mchezaji huyo anataka kucheza Simba Sports Club msimu ujao timu kongwe kubwa na bora ukanda huu wa CECAFA. Chanzo hicho kinasema malengo yake ni kujibrand Africa nzima imjue na hawezi kufikia malengo hayo kama ataendelea kubakia kucheza Azam Fc timu ambayo haiwezi kuchukua ubingwa wa ligi kuu au kumaliza nafasi ya pili ili ipate tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Africa CAF CHAMPIONS LEAGUE. Feisal Salum Abdallah Fei Toto anasema timu pekee itakayofanya aonekane Africa nzima na afike mbali kimataifa ni Simba Sports Club pekee kwa sasa ndio anaiona timu yenye malengo makubwa ya kuliteka soka la Africa yeye kama kijana mdogo mwenye ndoto za kufika mbali anatamani sana kucheza Simba Sports Club atafanya kila linalowezekana ili atue kwenye klabu hiyo ambayo itatimiza ndoto zake kwa vitendo na sio maneno. from UDAKU SPE