Posts

Showing posts with the label Habari

Rais Magufuli: Kwenye madini tumechezewa sana

Image
“Nataka korosho tuwe tunazivuna na kuziongezea thamani Tanzania, malighafi zitumike kwenye mambo mengine, kisha tunazisafirisha kwenda kuuza, tuvae viatu kutoka viwanda vyetu, kwenye madini tumechezewa sana yalisemwa mengi, nilisimama kusema bora kufa ukiwa unaitetea Nchi” -JPM from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/33BaNsT via IFTTT

Tutatengeneza nguo za pamba tuzivae halafu mitumba tuwapelekee wao- JPM

Image
“Wakati natoka kuchukua fomu leo na Mama Samia, nikaangalia Majengo yalivyokaa, Dodoma ilivyopendeza nikasema kiukweli tumefanya kazi nzuri, tutaendelea kufanya kazi, ikiwezekana tuwe na viwanda ambavyo tutatengeneza nguo za pamba tuzivae halafu mitumba tuwapelekee wao” -JPM from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2PvDgIg via IFTTT

Tayari nimeshachukua fomu, nitaomba uzinduzi wa kampeni tuufanye Dodoma- JPM

Image
Tayari nimechukua fomu, Kitabu cha mwaka huu cha Ilani ya CCM ni kikubwa kuliko cha mwaka 2015 kwasababu kina mambo mengi siwezi kuyasema yote tutayasema wakati wa kampeni, na nitaomba uzinduzi wa kampeni tuufanye Dodoma kwasababu ndio Makao Makuu ya Nchi”-JPM from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/33uCBiE via IFTTT

JE UNATAFUTA CHUO CHA UDAKTARI NA CLINICAL MEDICINE ?

Image
MASOMO YA UDAKTARI/ CLINICAL MEDICINE CHUO: ST DAVID COLLEGE OF HEALTH SIFA: Alama angalau D katika masomo ya fizikia,kemia na bailojia MUHULA : SEPTEMBER 2020 UDAHIRI UNAENDELEA Nipigie 06831068690 / 748749600 Au fika kimara Temboni eneo la MOA AU ingia  www.stdavidcollege.ac.tz from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2XxKxfc via IFTTT

Mexico yakaribia vifo 50,000 vya wagonjwa wa COVID-19

Image
Wizara ya Afya ya Mexico imesema kwamba watu wengine 6,139 wamethibitishwa kuambukizwa virusi ya korona na wengine 829 kufariki dunia ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita. Hisabu hii inaifanya sasa Mexico kuwa na jumla ya watu 456,100 walioambukizwa, ambapo takribani 50 alfu kati yao wamepoteza maisha.  Taifa hilo la Amerika Kusini ni la tatu kwa kuwa na vifo vingi zaidi vinavyotokana na maambukizo ya COVID-19, ikitanguliwa na Marekani na Brazil. Nchini Marekani, watu wengine 1,262 wamefariki dunia ndani ya masaa 24 yaliyopita, na imeongeza wagonjwa wengine 53,158 ndani ya kipindi hicho.  Kwa sasa, Marekani imeshasajili watu milioni 4, laki nane, alfu 18 na 328 walioambukizwa virusi vya korona. Jimbo la Florida linaongoza nchini Marekani ambapo sasa limepindukia wagonjwa laki tano. Katika jimbo jengine la Arizona, wafungwa zaidi ya 500 wamegunduliwa kuambukizwa virusi vya korona. from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3kffEpz via IFTTT

Watanzania wahimizwa kutumia kitoweo cha nyama

Image
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma. Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa ulaji wa nyama kwani takwimu zinaonyesha kiwango cha ulaji wa nyama kiko chini ambapo sasa ulaji umefikia asilimia 15 huku Shirika la Afya Duniani likitaja Mtu wa kawaida anatakiwa kula angalau kilo 50 kwa mwaka. Akizungumza Jijini Dodoma  kwenye paredi ya mifugo kwenye maonesho ya mifugo na wakulima nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema  kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Tanzania bado ulaji sio mzuri ambapo takwimu zinaonesha mwaka  2017/ 18  ulaji wa nyama ulikuwa kilo 10 kwa mwaka. “Angalau kiwango kimekuwa kidogo sasa tumefikisha kilo 15 mwaka, bado tuko chini sana .Watanzania wajitahidi kula nyama ambayo ni sahihi,” amesema Ole Gabriel. Aidha amesema kwa kiwango sasa unywaji wa maziwa umefikia lita 200 kwa mwaka, lakini mwaka  2018/19 unywaji wa maziwa ulikuwa lita 54 kwa mwaka ka...

Msumbiji yatangaza hali ya dharura kwa mara ya pili

Image
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametangaza siku nyingine 30 za dharuraImage caption: Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametangaza siku nyingine 30 za dharura Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametangaza siku nyingine 30 za dharura kujaribu kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona. Hii ni mara ya pili kwa taifa hilo kutangaza dharura ya hali ya afya tangu mwezi Machi wakati walipothibitisha mtu wa kwanza mwenye virusi vya corona nchini humo. Rais Nyusi alihutubia taifa kupitia matangazo ya televisheni na kuainisha hatua ambazo zitasaidia kupambana na virusi hivyo kwa urahisi . Awamu ya kwanza kuanzia Agosti 18, taasisi za elimu ya juu zitafunguliwa , mafunzo ya jeshi na ufundi. Mikusanyiko ya dini itaruhusiwa kwa watu wasiozidi 50 . Idadi ya watu 20 mpaka 50 wataruhusiwa kuhudhuria katika msiba au mazishi lakini kwa mtu yeyote aliyekufa kutokana na virusi vya corona watu watakaomzika wasizidi 10. Awamu ya pili itaanza Septemba; maeneo ya burudani kama sinema, ‘casino’ na sehemu z...

Mataifa 8 ya Magharibi yaitaka Urusi iondoshe wanajeshi wake Georgia

Image
Marekani na mataifa saba ya Ulaya yameitaka Urusi kuondowa wanajeshi wake katika majimbo ya Abkhazia na Ossetia Kusini nchini Georgia, na kuruhusu huduma za kibinaadamu kufikishwa kwenye maeneo hayo hasa katika kipindi hiki cha korona.  Mataifa hayo ya Magharibi yalisema hapo jana baada ya kikao cha ndani cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Miroslav Jenca, kwamba kuendelea kuwepo kwa ukaliaji wa kijeshi wa Urusi katika majimbo ya Abkhazia na Ossetia Kusini na kuutambuwa kwake kile kiitwacho uhuru wa majimbo hayo, ni hujuma dhidi ya mamlaka ya Georgia.  Georgia iliwahi kujaribu kutwaa udhibiti wa jimbo lake lililojitenga la Ossetia Kusini wakati wa utawala wa Rais Mikhail Saakashivli, hatua iliyogeuka vita kati yake na Urusi vilivyoanza tarehe 7 Agosti 2008. from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2XwKIaL via IFTTT

Tunasubiri Suprise ya Rais Magufuli - Alikiba

Image
Staa wa Bongofleva Alikiba amesema siku ya mchezo wa "Team Kiba Vs Team Samatta" August 8 Uwanja wa Benjamin William Mkapa, kutakuwa na mambo mengi ikiwemo burudani na huenda kukawa na Suprise Rais John Pombe Magufuli kwa sababu amemuomba awepo kwenye mchezo huo. Alikiba amesema Rais John Pombe Magufuli amewaomba watanzania tuweze kudumisha amani kwa sababu yeye amefanya mengi kilichobakia ni sisi kutimiza na usalama utakuepo siku ya mchezo huo. "Nilimuomba Rais Magufuli aweze kutusaidia kitu kwa hiyo kuna uwezekano wa kuwa na suprise, msije mkashangaa Rais akaja kwa sababu yeye ni mpenzi wa burudani na anatukubali wote mimi pamoja na Samatta, Pia amempongeza sana Mbwana Samatta tulivyokuwa Dodoma kwa kazi kazi nzuri, hivyo tunasubiria suprise yake na chochote kinaweza kutokea kwenye siku ya mchezo huo" amesema Alikiba from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/31rEOIO via IFTTT

Facebook, Twitter zaondoa ujumbe wa Trump kuhusu virusi vya korona

Image
Mitandao ya Facebook na Twitter imeondowa ujumbe wa Rais Donald Trump ambao imesema unavunja kanuni zinazokataza kusambaza habari za kupotosha juu ya virusi vya korona.  Ujumbe huo ulikuwa na kipande cha vidio kutokana na mahojiano yake na Fox&Friends, ambapo Trump anadai kuwa watoto wadogo wana kinga dhidi ya COVID-19.  Msemaji wa Facebook amesema kuwa ujumbe huo ni wa uongo. Ujumbe wa Twitter wenye vidio hiyo hiyo ambao awali ulitumwa na timu ya kampeni ya Trump nao pia ulifichwa na Twitter kwa sababu hizo hizo.  Msemaji wa Twitter amesema timu hiyo ya kampeni inapaswa kwanza kuuondowa ujumbe huo kabla hawajaruhusiwa tena kuutumia mtandao huo.  Kituo cha Udhibiti wa Maradhi nchini Marekani, CDC, kimesema hata kama watu wazima ndio waathirika wakubwa wa maambukizo ya virusi vya korobna, haimaanishi kwamba watoto wako salama, kwani kuna visa vingi vya wao kupoteza maisha pia. from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3kp7awn via IFTTT

Papa Francis aondoka Vatican, awaombea wahanga wa Lebanon

Image
Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, aliondoka makao makuu Vatican hapo jana na kusali kwenye kanisa la Basilica mjini Rome kwa ajili ya taifa la Lebanon, baada ya mripuko kwenye ghala la bandari kuuwa zaidi ya watu 135.  Hatua ya kiongozi huyo mkuu wa Wakatoliki kuondoka kwenye makao makuu ya Vatican na kwenda kusali nje katika kipindi hiki cha vita dhidi ya korona, imechukuliwa na wafuasi wake kuwa ishara ya umuhimu wa suala la Beirut kwa Kanisa.  Papa huyo alishawaombea wahanga wa mkasa huo kwenye ibada ya asubuhi mbele ya hadhara yake, lakini ameongeza ibada nyengine maalum kwa Lebanon, katika siku ambayo Wakristo wanaamini Bikira Maria alimtokea Papa Liberius miaka 1,662 iliyopita.  Wageni na watalii walijipanga kwenye mitaa ya Rome kumkaribisha Papa Francis jana Jumatano. from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3gzKAPd via IFTTT

Waziri Junior achaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Julai

Image
MSHAMBULIAJI wa Mbao FC ya Mwanza, Waziri Junior amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Julai wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), msimu wa 2019/20, Waziri amewashinda Peter Mapunda wa Mbeya City na Obrey Chirwa wa Azam FC alioingia nao fainali.  from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3a2islq via IFTTT

Breaking News: Rais Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais

Image
Rais Dk. John Magufuli leo Alhamisi Agosti 06, amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muhula wa pili kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), yaliyopo Njedengwa jijini Dodoma. from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3iapd7m via IFTTT

NEC yaanza kutoa fomu za Urais, wagombea wafunguka

Image
Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imeanza zoezi la kutoa fomu kwa wagombea mbalimbali wa vyama katika ngazi ya urais huku ikitoa taratibu zinazotakiwa kufuatwa na vyama hivyo, ikiwamo namna ya kulipia fomu hizo.                        TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3fv2XDr via IFTTT

Felix Minziro achaguliwa kuwa Kocha Bora mwezi Julai

Image
KOCHA wa Mbao FC ya Mwanza, Fred Felix Minziro amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Julai wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), msimu wa 2019/20, Minziro amewashinda Amri Said wa Mbeya City na Aristica Cioaba wa Azam, ambapo Minziro aliiongoza Mbao kushinda michezo mitano kati ya sita waliyocheza ndani ya mwezi Julai na kupata sare moja. from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/33v6m2H via IFTTT

Mlipuko Lebanon vifo vyaongezeka vyafikia 130

Image
Ripoti kutoka Lebanon zinasema hadi sasa Watu zaidi ya 130 wamethibitika kufariki kutokana na mlipuko uliotokea Bandari ya Beirut juzi August 04,2020, Watu wengine zaidi ya 4000 wamejeruhiwa, Rais wa Lebanon amesisitiza kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea. from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/31pSFj6 via IFTTT

Katibu mkuu ALAT afanya ziara halmashauri ya Singida

Image
HALMASHURI ya Manispaa ya Singida ni mingoni mwa Halmashauri  35 za Tanzania Bara zilizotembelewa na Katibu Mkuu wa wa Jumiya za Mamlaka za serikali za Mitaa ALAT Bw. Elirehema Kaaya kujionea utekelezaji wa  miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Hamashauiri hizo kupitia fedha za Mapato ya Ndani, Serikali Kuu, Wahisani na pia jitihada za jamii. Bwana Kaaya alisema miradi atakayotembelea ni ile ya Huduma kama vile miradi ya Sekta za Afya ,elimu na barabara ambayo imeonesha mafanikio kwa kiwango kikubwa na imetekelezwa kwa njia shirikishi na kwa kuzingatia  ubora . “Serikali ya awamu ya tano imejenga jumla ya vituo 352 vipya vya kutolea huduma za afya na vimejengwa kwa kiwango cha hali ya juu kupitia Force account”, alisema. Kwa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Bw. Kaaya ameweza kutembelea kituo cha Afya Sokoine ambacho kimepanuliwa kwa kuongeza jumla ya majengo 7. Kituo hiki kilipokea kiasi cha Tsh. 500,000,000/- kwa ajili ya upanuzi hu...

Makocha wamiminika Yanga kutuma CV ili kuchukua nafasi ya Luc Eymael

Image
IMEELEZWA kuwa jumla ya makocha 60 wamewasilisha CV za maombi ya kuifundisha Yanga katika msimu ujao wa 2020/21 ili kubeba mikoba ya Luc Eymael ambaye alifutwa kazi Julai 27 baada ya kueneza taarifa ambazo zilikuwa zinaviashiria vya ubaguzi wa rangi jambo ambalo linapigwa vita na familia ya michezo duniani kote. Kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mwingine na wanaotajwa kuingia rada za Yanga ni pamoja na Hans Pluijm, Ernie Brandits, Patric Aussems, Mecky Maxime na Hitimana Thiery. Habari zinaeleza kuwa bado uongozi wa Yanga unaendelea kupokea CV za makocha kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi ili kuweza kukinoa kikosi hicho. "Ndani ya wiki mbili hizi kocha mkuu mpya wa Yanga atajulikana baada ya kumfukuza Eymael hivi sasa uongozi unapitia CV za makocha mbalimbali waliotuma maombi kuja kuifundisha timu," ilieleza taarifa hiyo. Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Simon Patrick hivi karibuni alisema kuwa:"Tutahakikisha tunafanya uamuzi sahihi kwa kuteua ko...

Rais Magufuli kuchukua fomu leo

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Magufuli, leo Tarehe 06 Agosti, 2020 atachukua fomu ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya UchaguziTanzania (NEC) Njedengwa Jijini Dodoma. Rais Magufuli atachukua fomu majira ya Saa tatu asubuhi na atasindikizwa na watu wachache wakiwemo viongozi wakuu wa Chama, ikiwa ni kutekeleza matakwa na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Rais Magufuli anachukua fomu hiyo ili kugombea Urais kwa kipindi cha Pili katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba, 2020. Baada ya kuchukua fomu, Rais Magufuli atakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma (White House) ambako atakutana na wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM na kuwasalimu. from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/30wigYa via IFTTT

Japan yakumbuka miaka 75 ya bomu la atomiki Hiroshima

Image
Japan imefanya kumbukumbu ya miaka 75 tangu kuangushwa kwa bomu la kwanza la atomiki kwenye mji wa Hiroshima, huku meya wa mji huo akiitaka jumuiya ya kimataifa kuukataa ule aliouita uzalendo uliojengwa kwenye ubinafsi.  Hakukuwa na mkusanyiko wa maelfu ya watu kwenye Bustani ya Amani katikati ya mji wa Hiroshima kama inavyokuwa kwenye miaka mingine. Janga la virusi vya korona vilivyosambaa kote duniani limezifanya kumbukumbu za mwaka huu kukosa mahudhurio yake ya kawaida. Watu pekee walioruhusiwa kuhudhuria kumbukumbu hizo ni manusura wa mashambulizi hayo yaliyofanywa na Marekani pamoja na familia zao.  Majira ya saa mbili na robo asubuhi ya tarehe 6 Agosti 1945, ndege ya kijeshi ya Marekani chapa B-29 Enola Gay iliangusha bomu lililopewa jina la "Mvulana Mdogo" na kuwauwa hapo hapo watu 140,000 kati ya wakaazi 350,000 wa mji huo. Maelfu ya wengine walikufa siku za baadaye kutokana na majeraha na mionzi ya atomiki. Alkhamis ya leo, katika muda huo huo bomu hilo lil...