Usiwe zuzu wa mapenzi kama wataka mume jibebe ipasavyo
WANASEMA mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Na mwenye ndoa ni yule anayetaka ndoa. Dada, iwapo unataka kuingia kwenye uhusiano ambao baadaye utazaa ndoa na familia bora, ni muhimu kuwa makini na mtu unayeanzisha naye uhusiano. Vijana siku hizi wameharibikiwa. Wengi wapo kwa ajili ya kukidhi tamaa zao za binafsi kuliko mapenzi ya dhati. Ninakudokeza kwamba uhusiano mzuri ambao unaweza kuzaa ndoa na familia bora, ni vyema uanzie kwenye urafiki. Iwapo utauliza kwa nini uanze urafiki na mwenzako kabla ya kuchukua hatua za ndoa, maana yangu ni kwamba mnapoanzia kwenye urafiki wa kawaida, ni rahisi mtu kuonyesha tabia zake halisi. Marafiki huzungumza mambo mengi, hata yale yasiyofaa! Marafiki husimuliana mambo mengi sana yanayohusu maisha yao ya baadaye au yaliyopita, rafiki yako atakuwa huru kukueleza yake ya moyoni bila kuhofia kukukwaza ama kukusikitisha. Tofauti yake, wapenzi hawapati muda wa kutosha wa kujadili kwa upana mambo mbalimbali yanayowahusu, tayari kunakuwa n...