Sema hisia zako, katika njia ambayo haitakuumiza au kuwaumiza wengine kihisia. Mwili wa hisia:Mwili wa hisia ni jumla ya hisia na mihemko yote. Hiyo ni kama, hasira, furaha, huzuni, sononeko, kero, kijicho, wivu n.k. Kila binadamu ana hisia kwani humsaidia kuishi. Mfano: bila hasira, utakufa baada ya muda mfupi kwani hutaweza kujilinda. Tunapaswa kutumia vizuri hisia zetu ili ziwe msaada kwetu na kwa wengine badala ya kuwa maumivu kwetu na kwa wengine. Maumivu mengi ya kimaisha yanatokana na kushindwa kwetu kuzipeleka mahali bora hisia zetu ili zisitupe maumivu na badala yake ziwe na msaada kwetu. Kwa mfano: upande wa pili wa kijicho ni wa kujenga. Badala ya kuwa na hasira na kulaani na kumshusha aliyefanikiwa, mtu anaweza kujiambia kumbe inawezekana, na mimi nitajitahidi. Hapa ni kijicho kilekile ila kimegeuzwa kuwa wivu wa maendeleo (kutoa nafasi na muda kwenye kijicho katika mkabala wenye kujenga). Watu ambao wanaweza kuitumia miili yao ya hisia vizuri, ni wale ambao wana utam...