Posts

Waziri Mhagama: Waajiri Msiogope Uwepo Wa Vyama Vya Wafanyakazi Kwenye Maeneo Ya Kazi

Image
Na: Mwandishi Wetu, Morogoro Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini kutoogopa uwepo wa Vyama vya Wafanyakazi katika sehemu za kazi kwa kuwa ndio fursa ya pekee ya kutatua changamoto zinazojitokeza katika sehemu za kazi. Ametoa kauli hiyo jana Disemba 29, 2020 alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa sita (6) wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliyopo katika Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro. Waziri Mhagama alieleza kuwa Vyama vya wafanyakazi vimekuwa tegemeo kwa wafanyakazi hususan katika kulinda na kutetea maslahi na haki za wafanyakazi waliopo nchini, hivyo wajibu wa waajiri kutambua uwepo wa vyama vya wafanyakazi ili kuleta tija katika sehemu za kazi. “Uwepo wa Vyama Vya Wafanyakazi imekuwa ni nyenzo muhimu ambayo imeongeza tija na kujenga hali ya msukumo ...

Polisi aliyemuua raia wa Kiafrika afutwa kazi Marekani

Image
Afisa wa polisi aliyehusika na mauaji ya raia mwenye asili ya Kiafrika amefutwa kazi katika mji wa Columbus, jimbo la Ohio nchini Marekani. Mkurugenzi wa Usalama wa Umma wa Columbus Ned Pettus, alitoa taarifa kuhusu mauaji ya Andre Maurice Hill mwenye umri wa miaka 47 na asliye na asili ya Kiafrika, yaliyotekelezwa na polisi mnamo Desemba 21. Pettus alitangaza kwamba afisa wa polisi Adam Coy, ambaye alimuua Hill, alifutwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu na uzembe. Akibainisha kwamba Hill pia alicheleweshwa kupewa huduma ya kwanza, Pettus alisema, "Kitendo cha Hill kufyatuliwa risasi,  ni janga kwa jamii yetu na polisi, na kwa mtu yeyote anayempenda." Pettus aliongezea kusema kuwa vitendo vya Coy havikidhi kiapo cha polisi wala kuendana na vigezo  vya polisi vya Columbus. Coy alisimamishwa kazi wiki iliyopita kama sehemu ya uchunguzi ulioanzishwa dhidi yake, na kesi ya kiutawala ilifunguliwa dhidi ya maafisa wengine katika eneo la tukio. Hill, ambaye aliku...

Mwili wa Mngereza wawasili nyumbani kwao Kilimanjaro kwaajili ya mazishi

Image
Mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngeraza umewasili nyumbani kwao Kilimanjaro, Wilaya ya Same kijiji cha Suji Misheni tayari kwa mazishi. Mwili huo umeambatana na waombolezaji ambao ni familia, wafanyakazi wa Basata, wasanii na wadau wa sanaa. Ibada ya mazishi inatarajiwa kufanyika leo Desemba 30, katika uwanja wa shule ya Sekondari Suji, ambapo maziko yatafanyika katika makaburi ya familia. Marehemu Mngereza alizaliwa mwaka 1969 akiwa mtoto wa 11 kati ya 13 wa familia ya Mzee Lubejo Mngereza, ameacha mke na watoto wa tatu. from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3o4pgFa via IFTTT

Kirusi Kipya cha Corona Kinachosambaa kwa Kasi Chatua Marekani

Image
AINA mpya ya kirusi cha corona kinachoaminka kusambaa kwa kasi, imeripotiwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani na Amerika ya Kusini wakati rais mteule wa Marekani Joe Biden akiapa kuzidisha juhudi za utoaji wa chanjo.   Aina hiyo mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza, sasa kimeripotiwa kuingia Marekani katika mji wa Colorado. Kirusi hicho kimegundulika kwa kijana wa miaka 20 ambaye hana historia ya kusafri. Taarifa za vyombo vya habari za ndani zinasema kuna uwezekano wa kisa kingine cha kirusi hicho.   Wataalamu wanaamini kwamba aina hiyo mpya inaweza kuenea kwa kasi na itakuwa chanzo cha ongezeko la maambukizi Uingereza.   Aina hiyo mpya ya kirusi kinachujulikana kama B.1.1.7 tayari pia imeripotiwa Canada, Italia, India na Umoja wa Falme za Kiarabu. Chile nayo imeripoti aina hiyo mpya na kulifanya kuwa taifa la kwanza Amerika ya Kusini kubaini maambukizi yake.   Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameonya k...

RC Ndikilo aziagiza halmashauri mkoani Pwani kuwabana watendaji ambao ni wezi wa mapato

Image
Serikali Mkoani Pwani, imeagiza halmashauri zote mkoani hapo kuhakikisha zinadhibiti mianya ya wizi wa mapato na kuwabana watendaji watakaokuwa na uroho wa kuingiza mapato mifukoni mwao. Aidha imeelekeza, mikataba tata irejewe upya kwani halmashauri zina haki ya kufanya hivyo ili kujiridhisha. Akifungua kikao cha ushauri mkoani Pwani, Mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo alisema makusanyo ya mapato ya ndani ya baadhi ya halmashauri hayaridhishi kwani zipo halmashauri zenye asilimia 20-50 ya ukusanyaji wa mapato. Aliagiza ,kuziba mianya iliyopo ya upotevu wa fedha za mapato na watendaji wachache wanaovujisha mapato wabainike . “Na kwa hili nipo serious kabisa ,watendaji wababaishaji ,wanaohujumu fedha za serikali wakamatwe,wale wanaotumia posi zao wachunguzwe,watakaobainika kuhusika washtakiwe na wafungwe” alifafanua Ndikilo . Ndikilo alisema, mabaraza ya madiwani wa halmashauri, yakae kuangalia watendaji wazembe na wezi wasiojali maslahi ya wananchi na wawashughuliki...

Kaka Kuona Kiboko ya Matatizo ya Nguvu za Kiume, Mvuto wa Mapenzi na Magonjwa Sugu

Image
"KAKA KUONA" KIBOKO YA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME, MVUTO WA MAPENZI, MAGONJWA SUGU" MONKAR, INSULIN MMEA ASILIA UNAOPONYA KISUKARI KWA ALIYEUGUA MDA MREFU Hurejesha kongosho katika Hali ya utoaji ute mchungu na kuzalisha insulin na sukari Kuwa normo balance ya 4,5,6. Dawa hii ya maji na vidonge tiba -lishe kwa magonjwa sugu hufanya mmeng'enyo wa chakula kuwa katika Hali yake ya kawaida. MONKAR INSULIN Maana yake MHOLA Yaani ''Uzima hutibu Gout ukosefu wa ute sehemu ya viungo, tunanga mifupa, tumbo Kuunguruma vidonda vya tumbo bawasili, ganzi miguu kuwaka Moto gesi, Uzazi. Pumu kukojoa kitandani, tezi dume, dege dege na kifafa Cha mimba kwa wakinamama kusababisha kuvimba miguu, KWA WATU WA MIKOANI HUDUMA HII UNATUMIWA POPOTE ULIPO, KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM ASIYEKUWA NA MUDA WA KUFIKA OFFICENI UNALETEWA POPOTE ULIPO PIGA SIMU: 0713-293988, 0758-078280 from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3heTqTE via IFTTT

Sababu kuu zinazofanya watu wengi kuwa na maisha magumu Muungwana Blog · Muungwana Blog 2 · 9 hours ago Moja ya shauku walionayo watu wengi iwe katika maisha au biashara ni kutaka kufanikiwa. Kutaka kupata mafanikio yawe ya kiuchumi,kiafya, ki-uhusiano, kifedha,na hata kiroho ni moja ya malengo yanayotamaniwa na kila mmoja wetu. Lakini licha ya uwepo wa nia,shauku,na juhudi tunazoziweka ili kuweza kuyafanikisha malengo hayo bado mambo yetu yanaonekana hayasongi. Kuna sababu kadha wa kadha zinazopeleka wengi kushindwa kufanikiwa kaika maeneo hayo, ila katika makala yetu ya leo tutaangalia na kujifunza sababu zinazopeleka wengi kutofanikiwa kuinuka kiuchumi. Hivi umekwishawahi kujiuliza, ni sababu gani zinazowafanya wengi wasiinuke kiuchumi? . kuna sababu kadha wa kadha za wengi kutoikuinuka kiuchumi. Na baadhi ya sababu hizo ni kama zifuatazo: 1. Kukosekana kwa maarifa Kuna nukuu fulani katika biblia isemayo kwamba “ watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”. Msingi namba moja wa mafanikio katika nyanja yoyote ile kaika maisha ni maarifa. Maarifa ni ile njia inayotumiwa katika kujitoa katika shida ama kuweza kupata kitu au hekima.Na kukosekana huko kwa maarifa miongoni mwa watu wengi ndiko kwa kiasi kikubwa hupeleka wengi kutokuinuka kiuchumi. Na kwa maana hiyo, ili kuweza kufanikiwa katika nyanja yoyote ile katika maisha unahiaji kwanza kuwa na maarifa. Na maarifa hayo yanaweza kupatikana kwa kutumia njia kadha wa kadha kama vile kujisomea vitabu, kuwa na mshauri, kuhudhuria semina n.k. Kwa kujipatia kwako maarifa kwa namna moja au nyingine kutakusaidia katika kufungua hazina zilizositilika kichwani mwako na ambazo ikiwa zitatumika kimadhubuti basi zinaweza kukuinua kibinadamu, kiuchumi,ki-uhusiano, na kiroho. 2. Kutokutumia maarifa tuliyonayo Hakuna jambo lililo gumu katika maisha kama nidhamu binafsi, nidhamu binafsi ni ile hali ya kujiwezesha kufanya kile unachopaswa kufanya hata kama haujisikii kufanya. Wengi wetu tunajua kile tunachopaswa kufanya ila kwa namna moja ama nyingine tunashindwa kufanya. Kujipatia kwako maarifa na kisha kutokufanyia kazi maarifa ulionayo ni sawa na kazi bure. Mafanikio katika maisha huwa hayategemei sana kiasi cha elimu au fedha ulizonazo. Mafanikio katika maisha huwa yanategemea uharaka wa kujipatia maarifa mapya mazuri na wepesi wa kuyatumia, ila wengi wetu kwa kutokulitambua hili tumekuwa tukikazana katika kujiongeza maarifa bila ya kuwa na utahayari wa kuyatumia maarifa hayo. Kuna nukuu fulani katika biblia isemayo kwamba” jiangalieni basi jinsi msikiavo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa,na yule asiyekuwa na kitu atanyang’anywa hata kile ambacho anachodhaniwa kuwa nacho”. Na nukuu hiyo ina maana kwamba; kubali kujipatia maarifa ,yatumie kuwanufaisha wengine,usipoyatumia yatayeyuka. Ni muhimu ukajipatia maarifa na kuyatumia maarifa hayo. 3. Matumizi mabaya ya muda Kila mmoja wetu ana masaa ishirini na nne kwa siku,na jinsi unavyoyatumia masaa hayo ndiko kunakoweza kuleta kufanikiwa au kushindwa kwako.Muda ni rasiliamli ya muhimu sana.Muda ni rasiliamli ya pekee isiyoweza kurudi wakati inapotumika. Swali la muhimu unalopaswa kujiuliza ni kwamba; je,unautumia vipi muda wako?.uwekezaji wowote unaoufanya sasa kwa kutumia muda ulionao ndio utakachokuja kuvuna kesho. kamwe usikubali kutumia muda wako vibaya kwa kutokuwa na hiki au kile. Anza na matumizi mazuri ya muda pamoja na akili yako,na mungu atafungua njia ya kile usichonacho sasa. Ila wengi wetu kwa kutokulitambua hili tumekuwa tukiutumia muda wetu katika mambo kadha wa kadha ambayo kwa namna moja au nyingine yanakuwa hayana manufaa kwetu. 4. Matumizi mabaya ya pesa Moja ya elimu ya muhimu sana na inayopaswa kuzingatiwa na kila mmoja wetu ni elimu ya fedha. Na kwa bahati mbaya elimu hii huwa haifundishwi darasani. Kukosekana kwa elimu ya misingi ya fedha ndio kunakosababisha wengi kuwa na matumizi mabaya ya pesa. Tatizo tulilonalo wengi sio upatikanaji wa fedha bali ni usimamizi bora wa fedha.Kupata fedha ni jambo rahisi kwani fedha huwa inapatikana kulingana na kiasi cha thamani unachokitoa kwa wengine, ili uwe huru kifedha, ondoa au punguza kero za mahitaji ya wengine.Na kwa kufanya hivyo watu watakupa pesa zao na utakuwa huru kukamilisha mahitaji yako yote. lakini licha ya hilo, suala la kusimamia kimadhubuti kile tunachokipata bado limekuwa ni tatizo. Kukosekana kwa usimamizi mzuri wa fedha ndiko kunakosababisha wengi wetu kutokuinuka kiuchumi kutokana na uwepo wa matumizi mabaya ya pesa. Ni muhimu tukajifunza jinsi ya kusimamia na kutumia fedha zetu vizuri. 5. Kutafuta pesa ndio lengo la kwanza Kama nilivyosema hapo awali kwamba: ili uweze kuwa huru kifedha, basi ondoa au punguza kero za mahitaji ya wengine. na kwa kufanya hivyo watu watakupa pesa zao na utakuwa huru kukamilisha mahitaji yako yote.ila wengi wetu kwa kutambua ama kutokutambua tumekuwa tukiiweka fedha kuwa lengo letu la kwanza. Na katika kujifunza kwangu kuhusiana na maendeleo binafsi nilichokuja kujifunza ni kwamba; utajiri ni kupata unachokitaka na umaskini ni kukosa unachokitaka.Ukipenda kuhudumia watu kwanza utainuka haraka.maarifa ya kupenda kuhudumia watu yatakuwezesha kuona kile ambacho wengine hawaoni. Yatakuwezesha kuona majibu na kero za watu.Na utatumia maarifa hayo katika ubunifu wa mbinu na huduma mpya. Nakutakia utekelezaji mwema kwa kile ulichojifunza. OPEN IN BROWSER

Image
Moja ya shauku walionayo watu wengi iwe katika maisha au biashara ni kutaka kufanikiwa. Kutaka kupata mafanikio yawe ya kiuchumi,kiafya, ki-uhusiano, kifedha,na hata kiroho ni moja ya malengo yanayotamaniwa na kila mmoja wetu. Lakini licha ya uwepo wa nia,shauku,na juhudi tunazoziweka ili kuweza kuyafanikisha malengo hayo bado mambo yetu yanaonekana hayasongi. Kuna sababu kadha wa kadha zinazopeleka wengi kushindwa kufanikiwa kaika maeneo hayo, ila katika makala yetu ya leo tutaangalia na kujifunza sababu zinazopeleka wengi kutofanikiwa kuinuka kiuchumi. Hivi umekwishawahi kujiuliza, ni sababu gani zinazowafanya wengi wasiinuke kiuchumi? . kuna sababu kadha wa kadha za wengi kutoikuinuka kiuchumi. Na baadhi ya sababu hizo ni kama zifuatazo: 1. Kukosekana kwa maarifa Kuna nukuu fulani katika biblia isemayo kwamba “ watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”. Msingi namba moja wa mafanikio katika nyanja yoyote ile kaika maisha ni maarifa. Maarifa ni ile njia inayotumiwa katika ...