Posts

Biden "Putin ni Mchinjaji"

Image
Akiulizwa juu ya maoni yake kuhusu Putin baada ya kukutana na wakimbizi huko Warsaw, Biden alifunguka na kusema namchukulia Putin kama mchinjaji .” Huu ni mfululizo wa kumwita Putin  majina yakukasirisha ambapo hivi karibuni alimwita ni muhalifu wa kivita na anatakiwa kushitakiwa, kitendo hiki kiliikasrisha Kremlin na kumwita baloz wa Marekani kwa mahojiano. Rais wa Marekani pia alisema hana uhakika kwamba Urusi imebadilisha mkakati wake katika uvamizi wake wa Ukraine, baada ya Moscow kusema lengo lake sasa ni “kukomboa” kabisa eneo lililojitenga la Donbass mashariki. “Sina uhakika wameweza,” Biden alisema alipoulizwa na mwandishi wa habari ikiwa Moscow ilikuwa imebadilisha mkakati wake. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/kjcSlfv via IFTTT

Monalisa Asimulia Aliyopitia Sonia Alipokwama Ukraine

Image
Dar es Salaam. Msanii wa filamu, Yvonne Cherrie, maarufu Monalisa ameeleza maisha yake yalivyokuwa baada ya binti yake, Sonia kukwama Ukraine kwa sababu ya vita vilivyotokana na Russia kuishambulia nchi hiyo. Vita hiyo imeingia wiki ya tatu sasa, kubwa ikiwa ni Urusi kupinga Ukraine kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi (Nato). Baada ya kukwama kwa takribani wiki mbili Ukraine, akiwa miongoni mwa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Chuo cha Summy nchini humo, hatimaye wiki iliyopita mtoto wa staa huyo, Sonia alifanikiwa kuvuka mpaka na kuelekea nchini Hungary. Katika mahojiano na gazeti hili, Monalisa ameeleza namna maisha yake yalivyokuwa magumu katika kipindi ambacho binti yake alikuwa amekwama nchini humo, huku mitandao ya nje ikiripoti kuwa hali inazidi kuwa mbaya. “Kama mzazi maisha yalikuwa magumu kiasi cha kuathiri mambo yote niliyokuwa nikiyafanya, ikiwamo kazi, kushindwa kula na kutokana na kukosa hamu ya kula nimepungua uzito wa mwili kilo nane nzima...

Bondia wa Tanzania Twaha Kiduku Amchakaza Mkongo Alex Kabanga

Image
Bondia wa Tanzania Twaha Kiduku [@twaha_kiduku] ameshinda kwa pointi pambano la raundi nane (8) na kuvikwa ubingwa wa UBO baada ya kumtwanga bondia Alex Kabangu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo🇨🇩 from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/oWXNQAs via IFTTT

Mchengerwa afika ofisi za Wasafi Media

Image
Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Mohammed Mchengerwa ameweka bayana lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha inafanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya sanaa nchini. Mchengerwa amesema Serikali itaanza kwa kuwaunganisha wasanii kwa kuondoa makundi na kuwafanya kuwa kitu kimoja ili kujenga ushirikiano utakaorahisisha mafanikio ya juhudi za kuikuza tasnia hiyo. “Kikubwa tunadhamiria kuwaunganisha wasanii, dhamira ya serikali ni kuhakikisha kwamba inainyanyua Sanaa. Rais ametupa heshima kubwa sana, ametoa fedha nyingi kwenye Sanaa, kwa hiyo tulikuwa tunajadili hapa namna ya kuwa kitu kimoja katika Sanaa kumuunga mkono Mhe. Rais kwa kazi kubwa anayoifanya.” Amesema Mchengerwa. Aidha ameongeza kuwa jambi kubwa linalotakiwa ni kuendeleza mapinduzi ambayo Rais anayadhamiria katika Sanaa. Waziri Mchengerwa ameyasema hayo mapema hii leo alipofanya ziara katika kituo cha matangazo cha wasafi ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na mkurug...

Wasanii wa Muziki wanamtaka nani Kuwasemea?

Image
Swali lililobaki miongoni mwa wadau na wafuatiliaji wa kiwanda cha muziki Tanzania ni kuwa ni nani ataihodhi nafasi ya kuwa msemaji wa Shirikisho la muziki Tanzania na lini atatajwa, punde baada ya msemaji mteuliwa kujiondoa katika nafasi hiyo. Kufuatia kupingwa vikali na idadi kubwa ya wasanii pamoja na wadau mbalimbali wa muziki kwa madai hakustahili kuhudumu katika nafasi hiyo, hii leo Steve Mengele amejiuzulu rasmi nafasi hiyo. Wakati maelfu ya watu wakiwa katika sintofahamu hiyo, kutoka kundi la Weusi mwanamuziki mahiri George Sixtus Mdemu, maarufu G Nako ameweka wazi mtazamo wake kuhusu mtu sahihi anayestahili kuhudumu kama msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania na kukidhi hitaji la nafasi hiyo ili kuleta mabadiliko kulingana na matakwa ya katiba inayoliongoza Shirikisho hilo. “Kwanza hiyo nafasi haikuwepo, ndo imekuja sasa hivi lakini inabidi tupate mtu ambaye ana uelewa na kile anachoenda kukifanya nadhani AY, Wakazi, au Mwana Fa wanaweza kuifanya hiyo kazi vizur...

Ulaya Yakataa Kununua Gesi ya Urusi Kwa Sarafu ya Taifa Hilo

Image
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepuuzilia mbali takwa la rais wa Urusi, Vladimir Putin la kuyataka mataifa ya Ulaya kununua gesi kwa sarafu ya Kirusi. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepuuzilia mbali takwa la rais wa Urusi, Vladimir Putin la kuyataka mataifa ya Ulaya kununua gesi kwa sarafu ya Kirusi, huku akimshutumu rais huyo kuwa mwenye nia ya kutaka kuvikwepa vikwazo alivyowekewa kutokana na uvamizi wake wa Ukraine. Macron aliwaambia waandishi wa habari baada ya Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Ulaya wa mjini Brussels kwamba hatua ya Urusi haipo katika makubaliano na haoni sababu ya kutekelezwa kwa jambo hilo. Rais Putin alitoa takwa hilo juma hili katikia kipindi hiki ambacho serikali yake inakabiliwa na vikwazo vikali vinavyoathiri uchumi wa taifa hilo, kutokana na hatua yake ya kuingia kijeshi nchini Ukraine. Rais Joe Biden wa Marekani amesema Rais Vladimir Putin wa Urusi ameshindwa kuyagawanya mataifa ya Magharibi kwa vita vyake vya Ukraine. Umoja wa Kujihami wa NATO h...

SIRI ya AJABU kuhusu BINADAMU wengi KUFARIKl wakati wa USIKU kuanzia MUDA HUU!

Image
  SIRI ya AJABU kuhusu BINADAMU wengi KUFARIKl wakati wa USIKU kuanzia MUDA HUU! VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/sUx1kVp via IFTTT