FAIDA 6 ZA KULA PILIPILI MWILINI



Maalumu kwa wale watu wapenda na watumiaji wa pilipili ambao hutumia bila kufahamu faida zinazotokana na kiungo hiki chenye ladha ya uchachu na ukali lakini ndiyo kiungo chenye kuongeza hamu ya kuendelea kula chakula.
Capsaicin ndiyo kiambata ambacho huipa pilipili ladha yake ya uchachu pamoja na kazi yake ya kuongeza ladha ya chakula.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanasayansi wamegundua faida 6 zitokanazo na ulaji wa pilipili kwenye mwili wa binadamu, kama zifuatazo.
1. Hupambana na maumivu na uvimbe
Capsaicin huziondolea nguvu neuropeptides ambazo ndizo husababisha maumivu na kuvimba kwa sehemu mbalimbali mwilini.
2. Huzuia kuziba kwa mishipa ya pua
Capsaicin inajulikana kwa kupambana na kazi mbalimbali za bakteria mwilini ambazo nyingi husababisha kuathirika kwa sehemu ya wazi iliyopo kwenye mifupa hasa kwenye pua, pamoja na kazi yake ya kuunguza/ kuchemsha mwili, pia husaidia kuunguza ute unaoweza kusababisha kuziba kwa pua hivyo kuondoa, kupunguza kabisa maumivu ya sehemu hii ya mwili.
3. Husaidia mmeng’enyo wa chakula na kuondoa gesi
Husaidia kusisimua sehemu zinazozalisha enzymes mbalimbali tumboni hivyo kukifanya chakula kisibaki kimehifadhiwa tumboni kwa muda mrefu kikisubiri hadi pale ambapo enzymes hizi zitakapo zalishwa, pia huua bakteria wanaoweza kushambulia chakula hiko kisichomeng’enywa hivyo kupunguza uwezekano wa tumbo kujaa gesi.
4. Huulinda moyo
Ulaji wa pilipili kwa wingi huufanya moyo uwe imara sana katika kufanya kazi yake, husaidia pia kupunguza msukumo wa damu, kuunguza cholesterol na kuzuia kuganda kwa damu pamoja na kazi hizi huzinyima nguvu gene zinazosababisha kuziba kwa mishipa inayotoa damu kwenye moyo na kuisambaza sehemu mbalimbali za mwili hivyo kuondoa uwezekano wa kupatwa na shambulio la moyo na kiharusi.
5. Husaidia kutunza uzito sahihi wa mwili
Utafiti unasema utumiaji wa pilipili husaidia kusisimua protini aina ya TRPV1 ambazo ndizo hufanya kazi ya kutunza uzito sahihi wa mwili , kulinda kiasi cha sukari kinachofaa na mafuta yanayosababisha kuongezeka kwa uzito.
6. Husaidia kupambana na saratani ya tezi dume
Pilipili huingilia gene zinazopelekea uwepo wa tezi dume, Utafiti uliopo mpaka saivi unaonesha kuwa zaidi ya 80% ya seli zinazosababisha saratani hii hufa baada ya kuwekewa kemikali hii ya pilipili.




from Utundu kitandani http://bit.ly/2Wh5lJl
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI