MKASA: NILIPO SHINDWA KUMTUMIA PESA UKAWA MWISHO WA UCHUMBA




Kwa utangulizi ni kwamba mimi ni kijana wakiume, wa pekee katika familia ya watoto watatu, nina mchumba ambae tunaelekeana umri na niko nae kwa mda mrefu kidogo... tumepitia changamoto nyingi lakini Mungu mwema tunaendelea kusonga mbele;
Katika maisha yangu kuna kiumbe anaitwa Mama huwa namuheshimu na kumpenda sana, kuna mengi yanayofanya nimpende lakini kubwa ni kutokana na namna alivopitia mengi mpaka kupatikana kwangu (kwa kifupi ni kwamba nlipatikana kama ectopic pregnancy) kitu kilichopelekea afanyiwe oparesheni mara 2 mpaka kupatikana kwangu ni mengi alipitia lakini Mungu mwema mpaka leo mimi na yeye tuko salama.
Siwezi kuandika yote lakini kwa kifupi mnielewe kwamba Mamaangu ndie hero wa maisha yangu mpaka nilipo, na hata kwa huyo mchumba nilisha declare interest juu ya nafasi ya mama kwene maisha yangu.
Kisa kipo hivi, huyu mchumba tumekuwa tukisapotiana mambo mengi sana, ila ilitokea siku ya Valentine ameniomba kihela kidogo tu aenjoy na yeye huko aliko na kwa huo muda mamaangu alikuwa anaumwa na tukawa tunafanya mipango ya kumpeleka hospital, so hela iliyokuwepo nikatuma kwa mama isaidie matibabu yake na nyingine nikaweka akiba endapo niliyotuma haitatosha
Yeye aliponikumbusha juu ya hela aliyoniomba nikamwambia hela nimemtumia mama anaumwa ngoja nione maendeleo yake then ntakutumia alichonijibu ndo huwa kinanipa taabu mpaka leo, bila hata kutaka kujua hali ya mama ikoje alinijibu, "KWANI BABAAKO HUWA HAWEKI AKIBA MPAKA WEWE UTUME HELA MAMA ANAPOUMWA"
Hii sentensi iliniacha na maswali ambayo yananitatiza sana juu ya mtazamo wa huyu mwenzangu kwa sababu yeye nimekuwa nikimsapoti ninapoweza bila kujali ana ndugu na wazazi sasa kwanini yeye aseme hivyo kipindi ambacho mzazi wangu yupo serious anaumwa?
Ninachoomba ushauri hapa ni kwamba,
1. Nifanye nini ili hili alilonijibu lisiendelee kunifanya nimfikirie tofauti, maana tangu kipindi icho najikuta upendo nlokuwa nao kwake unapungua kidogo kidogo
2. Hilo jibu linaleta picha gani juu ya mahusiano yetu huko mbeleni ( Na hasa juu ya kuwakumbuka wazazi waliotupambania mpaka tunafika hatua tuliyopo)
3. Hatua gani nichukue maana ndo kwanza ni wachumba, ama nini nifanye ili nipate amani.
NATANGULIZA SHUKRANI




from Utundu kitandani http://bit.ly/2WfSeZ0
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI