MAMBO YA KUZINGATIA IWAPO UNATAKA KUSHIKA MIMBA
































Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu asishike mimba. Sababu hizo zinaweza zikawa zinamhusu mwanamke, mwanamume au wakati mwingine kutojulikana kabisa hali hiyo imesababishwa na nini. Wataalamu wanasema kwamba kwa miaka 20 iliyopita matatizo yanayohusu kushindwa kuzaa yameongezeka kwa kiwango kikubwa na asilimia 25 ya watu wanaotaka kubeba mimba na kuzaa mtoto wanakabiliwa na tatizo hilo.

Ni kweli kuwa kwa kawaida watu wengi hubeba mimba na kujaaliwa mtoto pale tu wanapofanya tendo la ndoa. Lakini jambo hilo halitokeo kwa watu wote na ingawa kwa baadhi ya watu kila kitu huonekana kwenda sawa lakini pia hushindindwa kubeba mimba. Utafiti unaonyesha kwamba katika kila familia au 'couples' 5 zinazojamiiana katika wakati muafaka wa ovulation ni moja tu ndio hufanikiwa kupata mtoto, huku karibu wanawake 9 kati ya 10 wakifanikiwa kushika mimba baada ya kujaribu kutafuta mtoto kwa mwaka mmoja mzima bila kuzuia mimba. Hivyo basi nawaomba wale ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kufuata maelekezo ili waweze kushika mimba lakini hawakufanikiwa, wasife moyo kwani ipo siku jitihada zao hizo zitazaa matunda.

Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba…

• Kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa kabla ya yote unamona dokta wako au unakwenda hospitalini na kufanyiwa vipimo ili kujua kama afya yako iko salama au la kwa ajili ya kushika mimba. Baadhi ya vipimo vinavyoshauriwa kufanywa ni pamoja na

1. General examination au uchunguzi wa jumla.

2. Kipimo cha kensa au Pap smear.

3. Kipimo cha magonjwa ya zinaa (STD) kama vile Chlamydia ambao wanaweza kuathiri uwezo wako wa kushika mimba.

4. Kipimo cha damu cha kuangalia kama una upungufu wa damu, Rh na kinga yako ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Rubella.

5. Kipimo cha mkojo cha kuchunguza iwapo una ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa wa kisukari huweza kumzuia mtu asishike mimba hata iwapo mzunguko wake wa mwezi uko sawa, anapata Ovulation na kidhahiri anaonekana hana tatizo lolote.

6. Kama una paka nyumbani au unakula sana nyuma (red meat) pengine si vibaya pia kupima kipimo cha Toxopmasmosis infection.

7. Kuyajua na kuzingatia baadhi ya mambo yanayoathiri kushika mimba ambayo ni pamoja na:-

• Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwiilini.

• Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo 'stress' huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.

• Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanamme baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)

• Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanamme.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomsaidia mwanamke kushika mimba:

• Anza kutumia vidonge vya Folic Acid, vidonge hivyo mbali ya faida nyinginezo humkinga mtoto atakayezaliwa na magonjwa ya ubongo. (Neural Tube Defect) kama vile Spinal Bifida na mengineyo. Dozi ni kwa uchache miligramu 0.4 za Folic acid kwa siku, miezi mitatu kabla ya kuanza hata kutafuta mtoto.

• Endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanamume aweze kuboreshe na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio. Kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.

• Jiepushe kunywa kahawa na binywaji vinginevyo venye caffeine. Waataalamu wanasema caffeine huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.

• Jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.

• Usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri. Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.

• Hakisha mwenzi wako hafanyi kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. Kufanya kazi kwenye mazingira ya joto kali sana kama vile mwanaume wanaofanya kazi kwenye matanuri ya kupika mikate, viwanda vya mafuta na miale hatari baadhi ya wakati huwa na matatizo ya kutozaa. Hivyo kabla mwanamke hajaanza kujilaumu kwa nini hashiki mimba, mwanamme wake pia anapaswa kufanyiwa uchunguzi kamili kuhusiana na suala hilo. Pengine ni suala ambalo wengi hatulijui kwamba katika tiba iwapo mke na mume au mtu na mwenzi wake wana tatizo la kutopata mtoto, wawili hao kwa pamoja hupaswa hufanyiwa vipimo na wala sio mwanamke mwenyewe. Hivyo iwapo unashindwa kushika mimba, hakikisha pia mwenzi wako hana tatizo pia. Wanaume pia kama walivyo wanawake hukabiliwa na matatizo mengi tu yanayosababisha familia kukosa watoto. Matatizo kama vile upungufu wa mbegu za kiume, uchache wa mbegu, kutokuwa na kasi mbegu na mengineyo ni miongoni mwa matatizo kibao ambayo mwanamume anaweza kuwa nayo na kukosa mtoto. Hivyo tabia ya kuwatizama wanawake kwa jicho la lawama katika jamii na kuwanyooshe kidole pale mimba inaposhindikana kushika ni kinyume cha ukweli wa kitiba na uhalisia.

• Usichoke kufuata mzunguko wako wa Ovulation na kufanya tendo la ndoa katika wakati ambao mwili wako (ewe mwamamke) uko katika siku za kuweza kushika mimba.





from Utundu kitandani https://ift.tt/2JgIWT1
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI