FAHAMU JINSI YA KUPATA MPENZI BORA

Unapochagua mpenzi wa maisha unatakiwa kuhakikisha unachagua mpenzi ambaye mtaendana naye kitabia, wengi wa wanawake na wanaume wengi wao utawasikia wakisema mimi nataka mpenzi asiye mlevi wakati huo yeye mwenyewe ni mlevi, kwa kufanya hivi kama utapata mpenzi, ni lazima mapenzi hayo hayatadumu kwa sababu utakuwa umepata mtu ambaye hamuendani kitabia na kihisia pia. 

Hivyo ili uweze kupata mpenzi sahihi unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo: 

Lazima na wewe uwe bora kwanza. 
Huwezi kusema unataka mtu bora wakati wewe mwenyewe siyo bora. Kama unataka mpenzi bora na sahihi kwako unatakiwa kwanza wewe mwenyewe uwe bora kwanza katika kila eneo ambalo wewe linakuhusu ndipo na wewe utakapopata mwenza bora pia. Hii si kwa wanawake tu bali hata kwa wanaume pia kama unataka msichana ambaye ni bora anza kwanza wewe kuwa bora ndipo mambo mengine yatafuta. 

Lazima na wewe ujiheshimu. 
Utasikia wadada / kwa wakaka wakisema mimi nataka mtu ambaye anajiheshimu, ni heshima gani ambayo unaizungumzia wakati wewe mwenyewe huna heshima hiy?. Kila wakati kumbuka huwezi kupata heshima unayoitaka kama wewe hauna heshima hiyo, kumbuka kila kitu unachokitaka kutoka katika jinsia tofauti ni lazima wewe uwe wa kwanza kuwa na tabia hiyo kabla ya kumuangalia mtu mwingine. 

Kama unataka mwenye gari hakikisha na wewe unalo la kwako. 
Hii ni kwa wadada utasikiawa kisema oooh mimi nataka mkaka mwenye gari, binafsi huwa najiuliza wewe unalo kama unalo basi una haki ya kusema hivo, kama unataka mtu mwenye gari basi na wewe uwe nalo ili muwe nayo mawili. Acha kujifanya unachagua watu wenye mali wakati wewe hizo mali hauna ni kapuku wa kutupwa. Kumbuka mali hutafutwa. 

Ukitaka msomi hakikisha na wewe umesoma 
Maara utasikia ooh mimi nataka msomi, mmmh ni usomi upi unaouzungumzia wakati wewe mwenyewe elimu yako huwezi hata kutamka hata mbele ya mtu?. kila wakati acha kujifanya bingwa wa kuchagua vitu ambavyo wewe huna, kama unataka msomi basi hakikisha na wewe ni msomi. 

Mwisho naomba kwa kusema maisha ya mahusiano siyo vitu bali ni hisia, ukijifanya bingwa wa kuchagua vitu kuliko kusikiliza hisia zako zinasema nini basi neno ndoa utakuwa ukilisikia kwa waliopo ndoani pekee, 

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI