Nahisi Kushindwa na ndoa; Mume Wangu Anatembea na Kondomu na KY Kwenye Gari



Mimi ni mwanamke nimeolewa na nina watoto wawili, mume wangu tulioana tukiwa tunapendana, lakini siku hizi mwenzangu matendo yake yamekuwa ya hovyo hata sina mapenzi naye tena.


Mara kwa mara namkamata katika mawasliano na wanawake tofauti tayari wakiwa kwenye mahusiano.


Kinachonichosha zaidi condoms haziishi kwenye gari anayokuwa nayo, mwanzo nlikuwa nazikuta anasingizia ni za rafiki yake hapo naye ni mtu mzima ana mke, nikawa napotezea hapo nilijua fika mume wangu ndo mtumiaji, imeniuma zaidi siku kipindi fulani gari yake imepata ajali wakati ikiwa kwenye matengenezo tukawa tunatumia ya kwangu sometimes nikaanza kukuta tena condoms kwenye gari, kubwa zaidi na ky gelly, moyo wangu uliuma sana yaani toka siku hiyo sipendi tena mume wangu na natamani kutengana naye kabisa ndugu zangu nifanye nini juu ya hili?


Ni mengi ya kueleza lakini yanayoniumiza zaidi ni hayo, na hiyo KY hata kwenye gari yake niliwahi kuikuta akaniambia ni ya rafiki yake, kilichokuja kinishtua zaidi ni pale nilikuta ameihamishia kwenye gari yangu na alisema sio ya kwake, nikatamani nimuite rafiki yake nipate ukweli lakini nikaona nitajidhalilisha tu nikaacha moyo unaniuma tu hadi sasa sina jamani tena katika moyo wangu na hata sina hisia naye jamani.






Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI