Ijue heshima ya mwanamke kwenye mahusianon ya kimapenzi


Mwanamke ni kama Jua unaweza usione umuhimu wake, yaani kila siku unaenda mjini jua lipo tu, unaliangalia lakini huangalii umuhimu wake kwako. Wakati mwingine likiwa kali unaanza kulalamika kuwa linachoma na lina kera. Lakini ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila jua maisha yasingekuwepo.

Chakula tunachokula ni kwasababu ya Jua, mvua ikinyesha sana mafuriko yakitokea tunatamani jua, kwenye baridi tunatamani pia jua, Hatuliwazii kwasababu lipo tu na linatimiza majukumu yake kimya kimya bila kelele.

Hiyo ni sawa na mwanamke, ukishaoa kuna mambo ambayo mwanamke huyafanya na baada ya muda unaanza kuyaona ya kawaida kawaida, chakula kinakuwa mezani kila siku hujui kinapikwaje na vyombo vinaoshwaje, anabeba mimba na watoto wanazaliwa hujui maumivu aliyoyapata lakini unatabasmu na kucheka ukijisifia watoto wangu na hata mkigombana unasema niachie wanangu wewe nenda tu, utafikili unajua maumivu aloyapata kipindi anawaleta duniani hao watoto.

Watoto wanaumwa mpaka wanapona hujui hata wameponaje, wanalia usiku hujui hata nani alikuwa anawabembeleza, ukirudi unakuta nguo safi chumba kisafi hutoi hata shukurani kwakuwa ushasahau kua kuna mtu anasafisha siwe safi muda wote.

Na anafanya vitu vyote hivyo kama Jua bila kelele lakini wewe ukitoa elfu mbili ya sukari utamnyanyasia mpaka ndugu zake kuwa unawalisha wewe! Hembu siku aondoke akuachie hao watoto unaojisifia kila siku kuwa ni wakwako na kumuambia hajaja na kitu, uanze kuwapikia na kuwaandaa kwenda shule, ufue nguo zao na zako. Unaweza kuajiri mfanyakazi lakini hawezi kufanya hata nusu ya kile anachokufanyia mkeo, kwani yeye atafanya kama kazi lakini mkeo anafanya kwa mapenzi, hahitaji umlipe chochote zaidi ya kutimiza majukumu yako na kumheshimu kama mke katika maisha yenu.

Vuta picha umeamka mkeo hayupo, watoto wanataka kuogeshwa kunywa chai na kwenda shule, hapo unatakiwa kuwahi kazini na mchana watoto wale.

Mheshimu sana mkeo kuna mambo mengi ambayo anayafanya ukiambiwa uyafanye Wewe utachanganyikiwa na mkeo huyafanya kwa upendo. Mwanamke anachohitaji kwa mume ni upendo na heshima tu.

Mhudumie, mpe upendo, muheshimu na muonyeshe kuwa kwako ana umuhimu mkubwa, mfanye mkeo atabasamu kila mara na familia nzima





































Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI