MAUMIVU YA MAPENZI DAH ACHA TU INASIKITISHA


1.Unaweza kuta mtu amekonda yaani afya mbovu,,ukafikiri labda ana virusi vya ukimwi ukaanza kumpa ushauri nasaha na kumshauri akapime ili ajijue aanze dozi ya ARV mapema kumbe mwenzio anaugulia MAUMIVU YA MAPENZI.
2.Unaweza shangaa mtu kajiua,kanywa sumu au kujinyonga ukafikiri ni stress za maisha,madeni au kauawa,,,kumbe chanzo kaumizwa na MAUMIVU YA MAPENZI,,kashindwa kuvumilia kaamua kujiua.
3.Unaweza kutana na mtu njiani kachanganikiwa anaongea mwenyewe kama tahira au kichaa ukajua karogwa kumbe chanzo ni MAUMIVU YA MAPENZI,,kaumizwa na mtu ambaye hakutarajia,,haamini maana walipendana mbo.
4.Unaweza shangaz dereva anapindua gari kizembe ukajua labda alilewa kumbe alikuwa anaugulia MAUMIVU YA MAPENZI,, kashindwa kuvumilia mawazo yamemtawala hajielewi mzimu wa aliyemtenda umeitawala akili yake,,,anaona barabara imepinda kumbe barabara imenyooka mwishowe anatumbukiza gari mtaroni.
5.Unaweza shangaa mamaa anauza gari,nyumba,kiwanja,vitu vya ndani n.k,,na kutumia fedha zote kunywa pombe  kulewa na kulala baa ukafikiri labda kachanganikiwa kumbe anaugulia MAUMIVU YA MAPENZI,,akili yake inamtuma kwamba pombe ndiyo suluhisho la machungu na maumivu yake.
6.Unaweza kutana na rafiki au ndugu yako ukamsalimia asiitikie,,asitake kukujua wala kukuaminj,ukajua labda kaharibika tabia,,amekuwa na dharau,,si kiburi la hasha anaugulia MAUMIVU YA MAPENZI,,hamuamini mtu yoyote chini ya jua,,,kila akimkumbuka aliyemtenda anaona wanaume/wanawake wote kama mbwa tu.
7.Unaweza kuta njemba yenye miraba minne imejaza misuli kama anorld Schwarzenegger linalia kama mtoto mdogo,,ukatafakari ukahisi kutokana na nguvu zake hamna mtu kumfanya Amalia labda kafiwa na mzazi wake HAHAHAHA kumbe na yeye anaugulia MAUMIVU YA kaumizwa
Aisee bado nafikiria nini siri iliyojificha ndani ya mapenzi,,maana kiukweli ikatokea watu wakipendana na mwisho kubwagana kifuatacho huwa ni MAUMIVU MAKALI SANA zaidi ya msiba.



from Utundu kitandani http://bit.ly/2Jj57tC
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI