SIMULIZI : RAHMA 01





Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

         
👉NAMBA 01

___ANZA NAYO
     Ilikuwa majira ya saa mbili na nusu usiku , kilikuwa ni kipindi cha baridi kali sana. Ilisikika sauti ya mtoto mdogo ( Mchanga) akilia , mtoto huyo alikuwa amebebwa mgongoni na dada mmoja aliyekuwa anapita maeneo hayo akiwa na wasiwasi na hofu kubwa moyoni mwake. Mdada huyo alitembea kwa kiasi kidogo akafika sehemu moja katika eneo hilo akaona kichaka pembezoni mwa barabara. 

Yule dada alikaa chini katika kichaka hicho akamtoa mtoto mgongoni akamuweka kifuani kisha akawa anamnyonyesha mtoto yule, Mtoto wakati ananyonya alipatwa na usingizi na akalala fofofo, Yule Dada alipomuona mtoto kalala , Alimwangalia mtoto huyo machozi yakiwa yanamtoka kwa wingi 

Alisema .....:-
Mwanangu RAHMA nisamehe Mimi mama yako kwa ukatili huu ninaokufanyia , Sina budi kufanya hivi mwanangu nisamehe sana.

Baada ya maneno hayo, alimbusu mwanae rahma akavua cheni yake alafu akamvisha mwanae , baada ya kumvisha ile cheni alimuacha rahma katika kichaka hicho akaondoka nafsi yake ikiwa inamuuma sana.Ulipita muda kiasi hadi saa nne usiku baridi ilizidi kuwa kali, baridi hiyo ilisababisha RAHMA aamke toka usingizini na kuanza kulia , rahma alilia sana , akalia zaidi masikini , Sauti ya kilio hicho ilisambaa sana kwakua ulikuwa ni usiku sauti ilisambaa sehemu kubwa .

Sauti ile ilimfikia mnyama mmoja (mbwa) aliekuwa karibu na maeneo hayo, Mbwa yule alianza kufuata sauti hiyo hadi alipofika maeneo aliyokuwepo mtoto (Rahma), Mbwa yule alianza kunusa huku na huko na kubahatika kugundua sehemu aliyokuwepo mtoto rahma, Yule mbwa alianza kukimbilia sehemu aliyokuwepo mtoto kwa kasi zaidi alipomfikia mtoto yule mbwa ali.....

___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI