SIMULIZI :RAHMA 02




Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

         
👉NAMBA 02


Tunaendelea ......

Yule mbwa alianza kukimbilia sehemu aliyokuwepo mtoto kwa kasi zaidi alipomfikia mtoto yule mbwa alimrukia nyoka mkubwa aliekuwa karibu na mtoto (rahma ) Mbwa yule alipambana sana na joka lile hatimae yule mbwa akamuangamiza yule nyoka . Baada ya nyoka kufa  yule mbwa alisogea sehemu aliyokuwepo  mtoto Akabweka sana wakati huu akiwa na njaa kali , Yule mbwa alimuangalia sana, rahma kwa muda mrefu kidogo kisha akalala pembezoni kwa mtoto ( rahma) . Ulipita muda kiasi mvua yenye  upepo mkali ilianza kunyesha kwa kasi sana , Rahma alianza kulia kilio toka kwa rahma kilizidi kutokana na baridi kali pamoja na maji ya mvua yaliyokuwa yakimdondokea usoni kwake.

Yule mbwa alianza kubweka na kutembea huku na kule kwa muda mrefu akitafuta msaada kwa bahati nzuri  kuna mwanaume mmoja alikuwa anapita barabara hiyo, Yule mbwa alipomuona yule mwanaume alimfuata kwa kasi huku akiwa anabweka kuashiria anahitaji msaada, Lakini kwakua lugha ya mbwa haieleweki, yule mwanaume alikimbia na kurudi alipotoka akiwa na hofu  alipoona yule  mbwa anakuja upande aliokuwepo kwa kasi huku akibweka, yule mwanaume  aliogopa kung'ata na mbwa yule hofu aliyokuwa nayo ilimfanya aongeze mwendo zaidi.

Yule mbwa alipoona binadam yule akikimbia alisimama akarudi alipokuwa mtoto (rahma) yule mbwa alijilaza pembeni ya mtoto japo mvua kubwa ilizidi kunyesha kwa kasi , Baada ya muda kiasi kupita  yule mbwa alisimama akang'ata nguo aliyokuwa amevalishwa mtoto (rahma) kisha akajaribu kumbeba kwa kutumia mdomo wake lakini alishindwa kwakua mwili wa mtoto ( rahma) ulikuwa Mkubwa. Mbwa yule alisumbuka sana hatimae akang'ata kitambaa kile upande wa miguu na kuanza kumvuta taratibu taratibu kwenda anapopajua yeye.

Mama wa rahma ( Fatuma) alikuwa analia sana chumbani kwake kwa kitendo kigumu na ukatili alioufanya kwa mtoto wake rahma, baada ya kumtupa huko porini, Japo mvua ilikuwa inanyesha lakini hakuisikia kwani akili na fikra zake zilikuwa mbali sana. Mara ghafla akastuka aliposikia mlio wa radi  alipotazama dirishani aliona mvua kubwa ikinyesha Fatuma alisema :-

"" Maskini mwanangu hivi nimefanya ujinga gani sifai kuwa mama Mimi, Hapana haiwezekani namfuata mwanangu , namfuata mwanangu mimi "

Fatuma alitoka nje  huku akiwa hajavaa viatu akakimbia kwenda sehemu alipomuacha mtoto wake alikimbia sana, sana, sana, sana kwa muda mrefu kwa sababu kulikuwa na umbali mrefu toka alipokuwa anaishi na sehemu alipomuacha mtoto. Baada ya muda fatuma alifika eneo alilomuacha mwanae , Fatuma alistuka na kustajabu kwa mshangao mkali na msisimko wa ajabu akapiga kelele kali sana alipoona......... 

___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO


Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI