SIMULIZI : RAHMA 03





Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

👉NAMBA 03

Tunaendelea ......

Fatuma alistuka na kustajabu kwa mshangao mkali na msisimko wa ajabu akapiga kelele kali sana alipo ona damu nyingi zilizosambaa maeneo yale , Fatuma alilia zaidi  na kushika mikono kichwani, fatuma alijutia sana kwa kumuacha mtoto wake eneo lile na bila shaka alitambua mwanae ameshaliwa na wanyama wakali wanaotembea usiku. Fatuma alijilaumu sana kwa kitendo alichofanya , alitamani kujinyonga ili apoteze maisha.

Usiku huo huo majira ya saa sita usiku yule mbwa alizidi kumvuta rahma hadi kwenye nyumba moja iliyokuwepo mbali sana na maeneo yale , Pamoja na umbali mrefu lakini yule mbwa alijitahidi kuendelea kumvuta rahma japo mazingira yalikuwa magumu sana. Baada ya muda mrefu kupita Mbwa yule alifanikiwa kufika katika nyumba moja iliyokuwa pembezoni mwa mji, mbwa alianza kubweka kwa sauti ya juu zaidi. Sauti ile ilimstua mama mwenye nyumba, Yule mama mwenye nyumba aliamka na kutoka nje hakuamini kumuona mbwa wake akiwa na mtoto mdogo , alafu mtoto huyo akiwa analia sana. Yule mama mwenye nyumba alipo muona mbwa wake yupo nje ya nyumba na mtoto mdogo alirudi ndani akiwa na mshangao mkali sana akamuamsha mume wake , Baada ya mume wake kuamka walitoka nje wakamchukua yule mtoto wakaingia ndani pamoja na mbwa wao. Wakati wanamchukua yule mtoto ile cheni aliyokuwa kavalishwa rahma na mama yake  ilidondoka chini eneo hilo .

Walipofika ndani yule mama na mume wake, Waliinua mikono juu na kumshukuru sana mungu kwa sababu walikuwa wanatafuta mtoto kwa kipindi chote katika maisha yao ya ndoa bahati mbaya hawakubahatika kupata mtoto lakini leo hii mungu kawajalia mtoto,  Mume wa yule mama pamoja na furaha yote aliyokuwa nayo alipatwa na wasiwasi akamuuliza mke wake :-

"" Mke wangu unajua japo ninafuraha lakini ninahofu moyoni kwa sababu huyu mtoto hatumfahamu tumemkuta nje akiwa na mbwa wetu cha ajabu mbwa alikuwa anadamu mdomo, hatujui imekuaje mpaka akafika hapa, tusije tukapata kesi mke wangu mmmh .

"" Hapana mume wangu hii ni riziki yetu ametushushia mungu kutokana na maombi yetu tuliyokuwa tunaomba kila siku mume wangu hakuna kesi hii ni bahati na ninaahidi nitamlinda vyema na nitampatia mtoto huyu malezi bora ahsante mungu wangu kwa zawadi hii.

Mke hakuhitaji kabisa kumsikiliza mume wake alichemsha maji akamuogesha mtoto kisha akamkorogea uji akamnywesha japo ulikuwa usiku mrefu mama yule hakujali hilo aliendelea kumpatia uji mtoto hadi alipohakikisha mtoto kashiba akamlaza akiwa anaimba wimbo mzuri taratibu taratibu rahma akapitiwa na usingizi .

Fatuma baada ya kuona mambo yaliyotokea sehemu alipomuacha mtoto wake alichanganyikiwa  sana akawa anaenda ovyo na hajui  anakwenda wapi alitembea usiku mzima hadi palipo pambazuka , Kwa mbali akaona nyumba moja hivi na alikuwa na njaa Kali pamoja na kiu cha maji akasogelea ile nyumba akaomba maji ya kunywa. Cha ajabu mama yule yule aliemuokota mtoto ndiye aliyempatia maji ya kunywa.

Fatuma alipomaliza kunywa maji alishukuru mama huyo kisha akaondoka wakati anaondoka chini aliona kitu kama cheni yake  aliichukua hakuamini kuona ni cheni yake aliyomvisha mtoto wake rahma, akaanza kusema  mwanangu , mwanangu, huku akilia alimfuata yule mama aliyempa maji akamuuliza kuhusu mtoto Yule mama alikataa kwamba hajamuona mtoto yeyote kwa mbali ilisikika sauti ya mtoto akilia fatuma aligeuka kisha......

___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI