FAHAMU NINI CHA KUFANYA ILI KULINDA MAHUSIANO MAPYA


Hisia za mapenzi na msisimko huwa mkubwa kipindi ambacho upo kwenye penzi jipya. Ukiwauliza watu wengi leo ambao wanateswa na mapenzi, wanata­mani siku zirudi nyuma ili warudie kufaidi mapenzi kama ilivyokuwa siku za mwanzomwanzo.
Lakini wachache wanaojua nini cha kufanya unapoanzisha penzi jipya ili hisia na msisimko unaoupata, udumu kwa muda mrefu na uendelee kuyafurahia maisha ya kimapenzi. Mapenzi ni kama nyumba, ukijenga msingi imara, nyumba yako itakuwa imara na ukijenga msingi legelege, usitegemee nyumba yako kuja kudumu baadaye.
Kama upo kwenye mapenzi mapya na unatamani raha na msisimko unaoupata leo udumu, ni vizuri ukazingatia mambo yafuatayo:
MUONYESHE HESHIMA NA SHUKRANI
Wanandoa, wachumba au wapenzi wengi, hulalamika kwamba wenzi wao hawawaheshimu, hawana shukrani na ndiyo maana hawafurahii maisha yao ya kimapenzi. Unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za mapenzi, jenga heshima kwa mwenzi wako bila kujali umri, cheo au hali ya kiuchumi. Hata kama mwenzi wako ana udhaifu fulani, kwa sababu umem­penda na kuamua kuwa naye, jifunze kumheshimu.
Pia jifunze kuwa na shukrani hata kwa yale mambo ma­dogo anayokufanyia. Wen­gi huwa hawaoni umuhimu wa kuwashukuru wenzi wao na matokeo yake wanajenga ufa am­bao baadaye unasa­babisha matatizo makubwa.
PATA MUDA WA KUMCHUN­GUZA KWA KINA
Kuchungu­zana nina­komaani ­sha hapa, siyo ku­taka ku­jua kabla yako alikuwa na nani au amewahi kutoka na nani, wahenga wanasema bata ukimc­hunguza sana huwezi kumla. Kuchungu­zana ninakokuzungumzia hapa, ni vizuri kufuatilia kwa kina ili ujue mwenzi wako anapenda nini, hapendi nini, kitu gani kinamfurahisha na kitu gani kinamtia hasira.
Mchunguze akiwa na hasira anakuwa­je na akiwa na furaha anakuwaje, ana­penda sana kufanya mambo gani (hobi) au anapenda sana zawadi za namna gani. Ukishamjua, ni rahisi sana kuishi naye hata pale anapokasirika au ana­pokerwa na jambo fulani kwani tayari utakuwa unajua kwamba akiwa hivi, ujue amekasirika au akifanya hivi ujue jambo fulani halipendi.
Pia itakusaidia kwenda naye sawa kwa sababu akikasirika, utajua ufanye nini ili afurahi kwa sababu tayari unavi­jua vitu vinavyomfurahisha. Ni makosa makubwa kufanya jambo wakati unajua kabisa mwenzi wako hapendi.
JENGA UTARATIBU WA KUMUOM­BA MSAMAHA UNAPOKOSEA
Wanaume wengi wanaamini kwamba hata wakikosea, hawatakiwi kuomba msamaha kwa sababu kuomba msama­ha ni ishara ya udhaifu, matokeo yake wanaendekeza mfumo dume bila kujua kwamba mapenzi ni demokrasia!
Bila kujali kwamba wewe ni mwa­naume au mwanamke, mkubwa au mdogo, una fedha au huna, inapotokea umeziumiza hisia za mwenzi wako, iwe kwa jambo dogo au kubwa, ni lazima uombe msamaha na kuahidi kutorudia makosa.
Ukishajenga utara­tibu huu, hata kama mwenzi wako hakuwa na kawaida ya kuom­ba msamaha, tara­tibu utambadilisha. Utashangaa na yeye anaomba msamaha na huo unakuwa mfu­mo wa maisha yenu. Kuwa makini kwamba ukiomba msamaha leo, siyo kesho unarudia tena kosa lilelile, ataona unam­fanyia makusudi.

akubwa tuu🔞 Bofya Hapa kupakua App ya Utundu kitandani na upate mautundu na maufundi yoote
       Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome


ona jinsi ya kusugua G spot
bonyeza hapa

BONYEZA HAPA      HAPA








Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story