Mume Wangu Hana Wivu Kwangu..Nataka Nichepuka Ajue ili Apate Wivu Tugombani....


Anaomba ushauri wako, nimeolewa na ndoa yangu ina miaka miwili sasa, shida ni mume wangu. Anafanya kazi, anahudumia familia,a nanijali kwa kila kitu, haninyanyasi lakini shida moja mume wangu hana wivu. Yaani naweza kumuaga naenda sehemu falani hata hanikatazi, nikichelewa kurudi hata hapigi simu, nikimuuliza kwanini hajali hivyo hata nikirudi usiku ananiambia kuwa mimi ni mtu mzima.

Kaka najikuta kuwa nina kisirani, ni mtu wa hasira ila mume wang hajali kabisa, kuna wakati nachelewa makusudi hata mpaka saa nane lakini nikirudi ataniuliza nilikua wapi na jibu lolote nitakalompa atakubali. Kaka nashindwa niishije na huyu mwanaume, yaani nawaonea wivu wanawake wenzangu wanavyojaliwa na waume zao.

Kuna wakati natamani hata kuchepuka ili ajue apate wivu anigombeze tugombane, yaani ni wale wanaume ambao hata nikimuudhi basi ataomba msamaha yeye akiniambia kua hataki kuniudhi hivo yaishe...yaani natamani ugomvi

Kuna wakati hata naongea na wanaume wengine lakini hajali, sio kama nachepuka nafanya makusudi ili aumie lakini yeye haumii, kaka naomba nisaidie nifanye nini?

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI