Waziri Mkuu: Wanasiasa Waeleze Watakayo Fanya Kuliko Kubeza Yaliyofanyika


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu mara kampeni za Uchaguzi Mkuu zitakapofunguliwa ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani

Majaliwa amesema ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu

Amefafanua, “Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za kubeza, tujiepushe na lugha za kashfa, kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi”

Amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha yenye kujenga

Aidha, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge kuunda Tume maalum kuchunguza matukio ya kuungua kwa moto mfululizo kwa shule za msingi na Sekondari zinazomilikiwa na taasisi za dini ya Kiislamu nchini

from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/39JKm5e
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story