Mataifa 8 ya Magharibi yaitaka Urusi iondoshe wanajeshi wake Georgia
Marekani na mataifa saba ya Ulaya yameitaka Urusi kuondowa wanajeshi wake katika majimbo ya Abkhazia na Ossetia Kusini nchini Georgia, na kuruhusu huduma za kibinaadamu kufikishwa kwenye maeneo hayo hasa katika kipindi hiki cha korona.
Mataifa hayo ya Magharibi yalisema hapo jana baada ya kikao cha ndani cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Miroslav Jenca, kwamba kuendelea kuwepo kwa ukaliaji wa kijeshi wa Urusi katika majimbo ya Abkhazia na Ossetia Kusini na kuutambuwa kwake kile kiitwacho uhuru wa majimbo hayo, ni hujuma dhidi ya mamlaka ya Georgia.
Georgia iliwahi kujaribu kutwaa udhibiti wa jimbo lake lililojitenga la Ossetia Kusini wakati wa utawala wa Rais Mikhail Saakashivli, hatua iliyogeuka vita kati yake na Urusi vilivyoanza tarehe 7 Agosti 2008.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2XwKIaL
via IFTTT

Comments
Post a Comment