Mexico yakaribia vifo 50,000 vya wagonjwa wa COVID-19
Wizara ya Afya ya Mexico imesema kwamba watu wengine 6,139 wamethibitishwa kuambukizwa virusi ya korona na wengine 829 kufariki dunia ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita. Hisabu hii inaifanya sasa Mexico kuwa na jumla ya watu 456,100 walioambukizwa, ambapo takribani 50 alfu kati yao wamepoteza maisha.
Taifa hilo la Amerika Kusini ni la tatu kwa kuwa na vifo vingi zaidi vinavyotokana na maambukizo ya COVID-19, ikitanguliwa na Marekani na Brazil. Nchini Marekani, watu wengine 1,262 wamefariki dunia ndani ya masaa 24 yaliyopita, na imeongeza wagonjwa wengine 53,158 ndani ya kipindi hicho.
Kwa sasa, Marekani imeshasajili watu milioni 4, laki nane, alfu 18 na 328 walioambukizwa virusi vya korona. Jimbo la Florida linaongoza nchini Marekani ambapo sasa limepindukia wagonjwa laki tano. Katika jimbo jengine la Arizona, wafungwa zaidi ya 500 wamegunduliwa kuambukizwa virusi vya korona.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3kffEpz
via IFTTT

Comments
Post a Comment