Lukamba Auchambua Ugomvi wa Wake Zake



BAADA ya kuwepo kwa tetesi nyingi mtandaoni kuwa wake wa mpigapicha wa msanii mkubwa Bongo Nasibu Abdul ‘Diamond’, Ashraf Ibrahim ‘Lukamba’, Shuu Mimi na Ceccy hawapiki chungu kimoja, hatimaye mpigapicha huyo ameibuka na kuweka kila kitu sawa.


 


RISASI lilimtafuta mpigapicha huyo na kupiga naye stori nyingi kuhusu maisha yake, ambapo kwa kumuangalia kiumbo anaonekana mdogo, lakini ndiyo tayari anamiliki wake wawili, karibu umsikie:


Risasi: Lukamba tuambie, maisha ya ndoa unayaonaje?


Lukamba: Yako poa, namshukuru Mungu siku zinaenda.


Risasi: Hivi ni kweli kwamba umeshaachana na mke mkubwa (Shuu) kwa sababu ya mke mdogo (Ceccy)?


 


Lukamba: Hapana, mimi na mke mkubwa hatujaachana bado tupo pamoja na tunaishi vizuri tu na hata leo asubuhi nimetoka kwake.


 


Risasi: Siku chache zilizopita uliposti picha ya mke mdogo kwenye akaunti yako na kuweka makopakopa mengi, jambo lililoibua minong’ono mingi miongoni mwa watu, hadi mke mkubwa akafikia hatua ya kusema wewe na yeye mmeshamalizana yaani mmeachana, ulivyoona ile komenti ya mke mkubwa, ulijisikiaje?


 


Lukamba: Niliona hiyo komenti, lakini najua alijibu vile kwa hasira tu, baadaye aliniomba msamaha na kuniambia alijibu vile kwa sababu hakupendezwa na yale maneno maneno ya watu, basi nikamsamehe na kumsihi asisikilize maneno ya watu ovyo, badala yake anisikilize mimi, maana ndiyo mume wake.




Risasi: Shuu ni mtu wa aina gani?


Lukamba: Mpole, ni mwanamke fl’ani ambaye ana mapenzi na mume wake na anapenda sana kuwa karibu na mume wake, lakini pia ni mwanamke mmoja anayenisikiliza sana, mwisho ni mchangamfu sana. Ukiwa naye, huwezi kuboreka.


 


Risasi: Unapokutana na haya maneno mtandaoni kuwa una upendeleo kwa mke mdogo kuliko mkubwa, huwa unajisikiaje?


 


Lukamba: Mimi na mke mkubwa tuna miaka karibia minne, huyu mdogo ndiyo kwanza hata mwaka hajafikisha. Kwa hiyo, kuna vitu vingine lazima umpe mtu priority kidogo na yeye, akikaa sawa basi, lakini sio kwamba napendelea, nafanya sawa kwa kila mtu.


 


Risasi: Kwa nini humposti sana mke mkubwa?


Lukamba: Unajua suala la mitandao kila mtu na maamuzi yake, mke mkubwa sio mtu ambaye anadili sana na masuala ya mitandao, ni mtu ambaye sio mpenzi wa hivyo vitu, ndiyo maana hata ukiona kwenye akaunti yake Instagram, huwa anaposti mara moja moja.


 


Risasi: Ni kweli umeacha kufanya kazi na Diamond?


Lukamba: Hapana, sio kwamba nimeacha kufanya kazi na Diamond, bado nafanya naye, yaani bado ni bosi wangu na hata juzi tulikuwa Arusha tumetoka huko tukarudi hapa Dar.


Risasi: Ukipita mitandaoni na ukaona wake zako wanatukanana, huwa unachukua hatua gani kama mume?


Lukamba: Lazima ukae nao chini uwakanye, kwa sababu unajua mwanzo mwanzo kuelewana inakuwa vigumu sana na sio rahisi mtu kukubali kuongezewa mke wa pili, lakini nashukuru Mungu angalau sasa hivi mambo yamekaa sawa, nipo na amani.


Risasi: Unaamini kuna siku wataelewana na kuwa marafiki wazuri tu?


Lukamba: Naamini kabisa, kuna siku watakaa vizuri, ni jinsi mimi nitakavyokuwa naishi nao, hivyo kuna kipindi itafikia hatua wataelewana.


Risasi: Una mpango wa kuongeza mke wa tatu?Lukamba: (Anacheka) Sina na hata sitaki.Risasi: Kwa nini unasema hutaki?


Lukamba: Yaani sitaki kabisa hata kusikia hilo jambo, siongezi tena mke mwingine kwa sababu hawa wawili wenyewe sio mchezo, asikwambie mtu, yaani ni stress (msongo wa mawazo) kila siku, mara huyu kafanya hiki yule kafanya kile, tafrani kabisa, halafu ndio niongeze mke mwingine, hapana siwezi.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3cEcnwK
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI