Mashabiki wa muziki Kenya wapagawa na Kutajwa kwa Khaligraph Jone kwenye orodha ya Tuzo za BET kama Rapper bora 2020
Ni ndoto ya kila mmoja kuona chochote anachokifanya haswa kwenye sanaa iwe ya uigizaji, uimbaji ama riadha anapata nafasi ya kutambulika na ulimwengu, haswa hata kufikia hatua ya kutajwa kwenye tuzo za ulimwengu kama zile za BET. Na ndoto hii imekua kwenye kichwa cha rappa wa nchini Kenya Khalighraph Jones, ambae ameonekana kutolegeza kamba kwenye juhudi zake za kuubembeleza ulimwengu kumukubali kuwa anauwezo zaidi katika uandishi na kufoka mashairi adimu kwa lugha fasaha haswa kimombo japo Kiswahili pia yumo.
Rapper huyu ambae ameshawi fanya kazi na kundi la ROSTAM linalo jumlisha Roma na Stamina hapa Tanzania, ameshawahi kutajwa na kushinda kama rappa bora barani Africa kwenye tuzo za Soundcity zenye makao makuu yake jijini Lagos Nigeria mwaka wa 2018. Tokea wakati huo, Khaghraph Jones amezidi kutuoa vibao motomoto na pia amekua mwepesi katika kukubali kushirikishwa kwenye kazi za mastaa wenzake haswa wa Africa Mashariki.
Akiongea na Bongo5 kupitia muandishi wetu wa nchini Kenya Changez Ndzai, staa huyo amesema ni hatua kubwa sana kwake na amefurahia kutajwa kwakwe kwenye tuzo hizo za heshima ambazo anafahamu zitazidi kumtangaza zaidi kimataifa.
“Yooooooooh, KHALIGRAPH JONES IS A MOVEMENT, My 1st Ever BET Nomination in The Best International Flow Category, The OG Shall be respected๐๐๐ Cc @bet_africa @bet_africa,” Rapa huyo aliandika kupitia Instagram yake.
Upande mwingine mashabiki wake wameivamia akaunti yake ya instagram kwa mbwembwe na tafrija za kipekee kwani wanaamini staa huyu ndie muakilishi wao ambae atawakilisha Kenya duniani kupitia muziki.
Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya.
from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2GkMl5w
via IFTTT
Comments
Post a Comment