Mondi, Harmo Waiteka Nigeria!



BURUDANI ya muziki ni sehemu inayofuatiliwa na wengi duniani kwa sababu ni kitu ambacho kinaleta furaha kwa watu hata kwenye matatizo.


Lakini kwenye burudani hii, kumekuwa na chachu ya wanamuziki ambao wanajua kuitendea haki kwa kutoa ngoma kali ambazo zinakonga mioyo ya wapenda burudani.


Barani Afrika, kumekuwa na wimbi la wanamuziki wengi ambao wanafanya poa na kutikisa kila kona, ambapo panahitajika burudani hiyo ikiwemo nchi ya Nigeria ambayo ina wanamuziki wengi wakali.



 

Wanamuziki wengi, wao wamekuwa wakifuatiliwa kila pembe ya Dunia, lakini pia Nigeria imekuwa ikifuatilia muziki wa Bongo na kufanya kazi na baadhi ya wanamuziki. Katika uwanda wa Bongo Fleva, ukitajiwa orodha ya wanamuziki wanaofanya poa, huwezi kuacha kusikia majina ya mabosi wa lebo kubwa hapa Bongo, nazungumzia Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’ na Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Harmo’ au ‘Konde Boy’.


Mondi ambaye ni bosi wa Wasafi Classic Baby (WCB), amekuwa ni mwanamuziki ambaye anafuatiliwa na kujikusanyia mashabiki kibao ndani na nje ya Bongo kutokana na uzuri wa kazi zake, ambazo nazo zimekuwa zikisikilizwa mno.


Harmo ambaye ni bosi wa Konde Gang Music Worldwide, naye amekuwa akifuatiliwa na kusifika kama mwanamuziki ambaye anapeperusha vizuri bendera ya Tanzania.


Nigeria ni nchi ambayo imejaaliwa kuwa na wanamuziki wengi wenye vipaji vikubwa. Hata ngoma zao zimekuwa ni hoti na zinafanya wandazi.


Lakini Nigeria imekuwa ni nchi ambayo inakoshwa na wanamuziki wa Bongo na ndiyo sababu wamekuwa wakifanya kazi nao ndani na nje ya Bara la Afrika.


Kwa mujibu wa Mtandao wa BBNaija wa Nigeria, Bongo Fleva imeweza kuikuna vizuri burudani ya muziki nchini humo, licha ya wanamuziki wa nchi hiyo kuwa wanafu-atiliwa zaidi duniani kote.


Ripoti hiyo inasema kuwa, wanamuziki wa nchini humo, wamekuwa wakivutiwa kufanya kazi na wasanii wa Bongo, huku wakitanabaisha kuvutiwa na lugha ya Kiswahili.


Mtandao huo unasema kuwa, miongoni mwa wasanii wa Bongo waliowateka na ngoma zao kusikilizwa zaidi, ni Mondi na Harmo.


Zifuatazo ni kolabo kali walizofanya Mondi na Harmo wakishirikiana na wanamuziki wakali wa Nigeria, kiasi cha kufanya ngoma hizo kusikilizwa zaidi nchini humo.


NUMBER ONE REMIX-DIAMOND FT DAVIDO


Number One Remix ni ngoma ya Mondi ambayo alimshirikisha mwanamuziki wa Nigeria na mkali wa Ngoma ya Fall, David Adedeji Adeleke ‘Davido’.


Ngoma hiyo imetoka miaka sita iliyopita na ilifanya poa kwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 41 hadi sasa, na kubaki kwenye rekodi ya ngoma za Bongo Fleva zilizosikilizwa zaidi kwa muda wote.


KIDOGO-DIAMOND FT P SQUARE


Ni ngoma ambayo Mondi aliwashirikisha wanamuziki wenye majina makubwa wa Nigeria, waliokuwa wakiunda Kundi la P-Square; Peter na Paul Okoye.


Kidogo ni ngoma ambayo imetoka miaka minne iliyopita na kufanya vizuri kwenye platforms za kupakua muziki ikiwemo YouTube na kutazamwa zaidi ya mara milioni 33.


Kama tujuavyo, P Square ni kundi ambalo lilitoa kazi nyingi kali na kuliteka soko la muziki duniani kote kutokana na ukali wao, japokuwa kwa sasa wametengana na kila mtu kufanya kazi zake.


NANA-DIAMOND FT MR FLAVOUR


Ngoma nyingine inayotajwa kusikilizwa zaidi nchini humo, ni Nana ambayo Mondi alipasua anga kwa kufanya kazi kali akiwa na mnyama Flavour N’abania ‘Mr Flavour’.


Nana ni ngoma ambayo ilifanya poa kwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 65 kwa muda wa miaka mitano kwenye Mtandao wa YouTube.


LOVE DIE-PATORAKING FT DIAMOND


Ngoma nyingine iliyo kwenye listi hiyo ni Love Die kutoka kwa mwanamuziki mkali na mwenye maajabu yake kutokea nchini Nigeria, Patrick Nnaemeka Okorie ‘Patoranking’, akiwa amemshirikisha Mondi.


Ngoma hiyo iliyotoka miaka miwili iliyopita, imefanya poa kwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 46 kwenye YouTube na kusikilizwa sana kwenye platforms zingine ndani ya Bongo na nchini Nigeria.


FIRE-DIAMOND FT TIWA SAVAGE


Ni ngoma nyingine kali ambayo Mondi amemshirikisha mwanadada na staa mkubwa wa Nigeria, ambaye anasikika sana; Tiwa Savage.


Ngoma hiyo imetazamwa mara zaidi ya milioni 9 kwa muda wa miaka mitatu kwenye YouTube na bado inaongoza kusikilizwa nchini Nigeria.


SOUND-DIAMOND FT TENI


Ni ngoma nyingine inayofanya poa kutoka kwa Mondi akiwa amemshirikisha mwanamuziki ambaye anafanya vizuri Nigeria, Teni.


Sound imefanya poa kwenye YouTube kwa kutazamwa mara zaidi ya milioni 10 kwa muda wa miezi tisa hadi sasa.


DM CHICK-HARMONIZE FT SARKODIE


Ni ngoma kali kutoka kwa Harmo akiwa amemshirikisha mwanamuziki wa Nigeria, Sarkodie ambaye naye amekuwa akifanya wandazi kwenye ngoma zake.


Ngoma hiyo ambayo ina miaka miwili mpaka sasa, imetazamwa mara zaidi ya milioni 5 kwenye YouTube na kusikilizwa kwenye mitandao mbalimbali nchini Nigeria.


KAINAMA-HARMONIZE FT BURNA BOY


Kainama ni ngoma kutoka kwa Harmo akiwa amemshirikisha mwanamuziki wa Nigeria ambaye kwa sasa anaitetemesha ramani ya muziki, Damini Ebunoluwa Ogulu ‘Burna Boy’.


Ngoma hiyo ambayo ina mwaka mmoja tangu kutoka, imetazamwa mara zaidi ya milioni 18.


Bado inafanya poa kwa kusikilizwa kwenye mitandao mbalimbali na kupigwa kwenye vyombo vya habari nchini Nigeria.


SHOW ME WHAT YOU GOT-HARMONIZE FT YEMI ALADE


Ngoma hii Harmo amemshirikisha Yemi Alade, mwanamuziki ambaye anafanya makubwa nchini Nigeria.


Show Me What You Got, imetoka mwaka mmoja uliopita na kutazamwa mara zaidi ya milioni 4 na bado inatajwa kwenye listi ya ngoma za Bongo Fleva zinazotikisa nchini Nigeria.


FIRE WAIST-SKALES FT HARMONIZE


Fire Waist ni mkwaju mkali kutoka kwa mwanamuziki Skales wa Nigeria na amemshirikisha Harmo.


Ngoma hiyo imetazamwa mara zaidi ya milioni 5 mpaka sasa kwa muda wa miaka miwili kwenye YouTube.


Mbali na mkwaju huo, hivi karibuni Harmo alimtambulisha Skales kama msanii anayemsimamia kwa upande wa Afrika Mashariki kwenye kazi zake chini ya Lebo ya Konde Gang.


TEPETE-HARMONIZE FT MR EAZI


Ni ngoma nyingine ambayo Harmo amemshirikisha mwanamuziki wa Nigeria ambaye naye anafanya poa kwa sasa, Oluwatosin Ajibade ‘Mr Eazi’.


Ngoma hiyo imetazamwa mara zaidi ya milioni 1 kwa muda wa miezi mitano na kusikilizwa kwenye platform nyingine nyingi, hasa nchini Nigeria.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3cFp3U1
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI