Mwinyi Zahera "Simba Ina Kikosi Bora Msimu Huu"

 


 KOCHA wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Gwambina, Mkongomani Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa Simba wana kikosi imara kwa msimu huu wa 2020/21.

 

Zahera aliwahi kuwa kocha wa Yanga kwa kipindi cha msimu mmoja na nusu, aliyasema hayo baada ya kushuhudia kikosi chake kikipoteza baada ya kucheza na Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara. 


Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 26 ulikuwa ni wa mzunguko wa nne.


Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere, Pascal Wawa na Chris Mugalu.Zahera amesema Simba ina kikosi cha wachezaji wengi ambao wana vipaji vikubwa jambo ambalo linaweza kumuweka kwenye hatari mpinzani yeyote wanayekutana naye.


“Ni jambo lisilopingika kuwa Simba msimu huu imejipanga kufanya mambo makubwa kutokana na ubora wa kikosi chao ulivyo.


“Kabla ya mchezo dhidi yao tulikaa na wachezaji wetu na kuwaambia kuwa tunakwenda kucheza dhidi ya timu bora zaidi ya zile tulizocheza nazo hapo awali hasa kwa kulinganisha uwezo wa mchezaji mmojammoja.


“Kwa upande wangu nadhani miongoni mwa michezo yetu minne iliyopita huu ndiyo mchezo pekee ambao unaweza kusema tulistahili kupoteza kwa sababu tulizidiwa lakini kwenye michezo mitatu iliyopita tulicheza vizuri lakini hatukuwa na bahati ya kupata mabao,” amesema Zahera.


Gwambina kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 ikiwa imecheza mechi nne imepoteza tatu na kupata sare moja ya bila kufungana mbele ya Kagera Sugar Uwanja wa Gwambina Complex.


Imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Biashara United, Ruvu Shooting 1-0 Gwambina.





from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/34ccV93
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI