WCB ndio imeshikilia Bongo Fleva kwa sasa, very creative label

 


WCB (Wasafi Classic Baby) nadhani nikisema hivyo kila mtu anaelewa.

WCB nadhani kwa sasa ndio label iliyoshikilia industry ya Bongo Fleva hawa watu wako very Creative na Wanafikra yakinifu. Tena isitoshe tu kusema ni label namba moja Tanzania bali hata Afrika inajizolea umaarufu kwa sasa.


Label Ina combination ya wasanii wenye majina makubwa Kama vile;

Diamond Platnumz (The C.E.O)

Rayvanny

Mbosso

Zuchu

Lava Lava


Zipo fununu pia zinasema Hanstone aliyeshirikishwa na Maua Sama kwenye ngoma ya Iokote naye yuko WCB anasubiri utambulisho tu.


Label hii Ina wasanii wachapakazi haswa ikiongozwa na Diamond Platnumz.


Wamejizolea mashabiki wengi sana East Afrika na Afrika kwa ujumla kiasi kwamba kila msanii anayepita hapati wakati mgumu sana kuizoea na kuendana na Game.

Mashabiki wa WCB wako very supportive sana na wana mapenzi ya kweli na label yao.


Ukiacha hivyo wasanii wao wana majina makubwa tayari hivyo hawatumii nguvu kubwa kupromote mziki wao.


Ukizungumzia trends na talk of the town bongo (Kiki za Mitandaoni)hawa jamaa ndo kwao kabisa hata wasipotoa nyimbo wanabaki kuongelewa na mashabiki muda wote kwa sababu ya drama zao za kimtandao.


Ni ngumu kwa label nyingine kushindana na hawa jamaa. Clouds Media na media nyingine zilijaribu kuua mziki wao kwa kuacha kupiga nyimbo zao Ila kwa nguvu ya mashabiki zao nyimbo zao zilikuwa zinapeta kitaani kama kawa watu walikuwa wana download na Ku stream Kama kawa.


Ukiangalia WCB iko full oriented sio Kama label nyingine Ina departments za kusimamia kila mahali

For instance

1.Social Media Department

2.Artists Managers

3.Directing Team

4.Music Department.


Lakini pia uanzishwaji wa kituo cha Wasafi Media umeongeza chachu na ufanisi kwa label kwa sababu kazi zao sasa zinapigwa bila masharti na kwa vyovyote vile mpenzi wa Wasafi Media asiye mpenzi wa WCB ataanza kuvutiwa nao tu.


Mwisho nimalizie kwa kutaja label nyingine ambazo binafsi naona bado zinatania katika uwekezaji

1.Kings Music(Alikiba)

2.Konde Music Worldwide (Harmonize)

3.African Princess(Nandy)


Hata hivyo hawa jamaa kwenye upande wa Ku shoot Video wako very serious ndo maana video zao zina quality na ni nzuri.


Wanajua kuimba nyimbo za miondoko yote Singeli,Mapenzi,Club Banger na wanatisha.Hakuna label itakuja kuifikia WCB kwa uwekezezaji walioufanya na kwa Hardworking spirit waliyonayo.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2HyPBL5
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI