Kaze Atafuta Rekodi Mpya Leo Yanga



LEO Jumamosi, Kocha Mkuu wa Yanga anatarajiwa kuandika historia mpya wakati timu hiyo ikijiandaa kuwavaa Biashara United ya mkoani Mara katika mchezo wa raundi ya nane ya Ligi Kuu Bara.


 


Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga ambao kama watashinda, watafi kisha pointi 22, na kuzidiwa mchezo mmoja na Azam ambao jana walitarajia kucheza na JKT Tanzania.




Yanga hadi hivi sasa ikicheza michezo saba, hajaipoteza na imefanikiwa kushinda michezo yake sita mfululizo huku wakitoa sare ya 1-1 dhidi ya Prisons ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya msimu huu.Hata hivyo mchezo dhidi ya Biashara hautarajiwi kuwa mwepesi kutokana na ubora wa timu zote.


 


Biashara wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi 16 wakicheza michezo nane.




Rekodi anayoisaka Kaze ni kupata ushindi wa kwanza kwenye Uwanja wa Karume, Musoma ambao tangu Biashara imepanda kucheza ligi, Yanga haijawahi kupata ushindi wowote.Yanga wamekutana na Biashara kwenye uwanja huo mara mbili kati ya michezo hiyo, wamepata sare mmoja huku mwingine wakifungwa bao 1-0 baada ya kupanda daraja.


 


Hivyo katika mchezo wa leo, Kaze atakuwa na jukumu la kuhakikisha anaandikisha historia mpya kwa kuipa Yanga ushindi wake wa kwanza hapo Musoma.Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Kaze alisema kuwa: “Maandalizi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Biashara yanakwenda vizuri, kikubwa ni kutarajia mabadiliko ya kikosi changu cha kwanza.




“Tunacheza michezo minne katika siku 12, hivyo hakuna mchezaji ambaye ana uhakika wa kuanza mechi zote. Baadhi ya wachezaji hawakuwa wamecheza kwa muda mrefu hivyo ni vyema kuwatumia kwa tahadhari kuwaepusha na majeraha.


 


“Lakini kingine, hali ya viwanja ambavyo tunavitumia havipo katika hali nzuri, nimepata taarifa Uwanja wa Karume upo kama Uwanja wa CCM Kirumba ni tofauti na Uwanja wa Uhuru tuliocheza mchezo uliopita, hivyo upo uwezekano wa kuanza na washambuliaji wawili ili kuhakikisha tunaitumia vema mipira mirefu ya kushambulia.”



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2TJRBTu
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI