Morrison Aipa Bodi ya Ligi Mamilioni



MBALI na kupigwa faini ya Sh 500,000, nyota wa Simba, Bernard Morrison amehusika moja kwa moja kwenye kusababisha adhabu ya wachezaji wengine watatu kwa mwezi Oktoba waliokutana na rugu la kutoa kiasi hicho cha fedha na kufungiwa michezo mitatu ya ligi.

Adhabu hiyo iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TBLB) inamfanya Morrison ahusike kwenye jumla ya Sh 2m kati ya shilingi milioni 6,500,000 zilizokusanywa kutokana na makosa mbalimbali

Morrison alikutana na balaa hilo baada ya kumpiga ngumi nyota wa Ruvu Shooting, Juma Nyosso kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru, wakati Simba ikifungwa bao 1-0, Oktoba 26.

Pia Nyosso naye amelimwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kumkanyanga mguuni Morrison pamoja na kufungiwa mechi tatu za ligi. Nyota mwingine ni Shaban Msala ambaye naye alimpiga teke Morrison kwenye mchezo huo na kupigwa faini ya Sh 500,000 pamoja na kufungiwa mechi tatu na alionyeshwa kadi nyekundu.

Kiraka wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya amepigwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kumpiga ngumi Morrison, ilikuwa Oktoba 22, wakati Simba ikifungwa bao 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela.

Pia Kimenya amefungiwa mechi tatu za Ligi Kuu BaraPia timu ya Tanzania Prisons imepigwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kuingiza uwanjani magari ya viongozi na mashabiki wakati mchezo ukiendelea.

Timu nyingine zilizokutana na rugu la TPLB ni Dodoma Jiji ambayo imepigwa faini 500,000 kwa kosa la kuingia vyumba vya kubadilishia nguo kwa kutumia mlango wa nyuma wakati wakilazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Daruesh Saliboko wa Polisi Tanzania ametozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji na amefungiwa mechi tatu kwa kuwa alionyeshwa kadi nyekundu wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gwambina Uwanja Sheikh Amri Abeid.


Katika mchezo huo Gwambina ilipigwa faini ya Sh3m kwa kosa la wachezaji wake kucheza dakika 90 bila kuwa na nembo ya mdhamini mkuu wa ligi ambaye ni Vodacom.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2TIp3Kl
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI