Mwanamke Amwambia Mumewe Anatamani Wanaume Wengine


 ANITA CASSIDY (40) mwanamke ambaye amekuwa katika ndoa kwa miaka ipatayo kumi, alimwambia mumewe aitwaye Marc (46) kwamba anaona maisha na ndoa ya mume na mke yamemchosha na alitaka kuwa na wenza wengine wa kufanya nao mapenzi.

Katika mazungumzo ya wawili hao ambao ni raia wa Italia, mumewe alikubali kwamba wote wawili kila mmoja angekuwa na wapenzi wengine.    Lakini, je, katika ndoa moja panawezekana kuwa na watu zaidi ya wawili?
Anita Cassidy (katikati) akiwa na mpenzi wake wa kiume Andrea (kushoto) na mumewe Marc (kulia) wakichangia penzi la watu watatu.

 “Mwaka mmoja uliopita niliweka kila kitu bayana kwenye mtandao wa Facebook kwa picha niliyokuwa na mume wangu na watoto wetu wawili.  Marafiki zangu wakaanza kuniuliza kwamba mwanamme mwingine aliyekuwa katika picha alikuwa nani.  Niliwaambia alikuwa Andrea – mpenzi wangu wa kiume.


… Watatu hao wakiwa pamoja kando ya bahari wakipunga upepo.

“Nafahamu wengi watashangaa kwani walijua Marc ndiye mume wangu halisi.   Lakini ukweli ni kwamnba nilikaa naye jikoni mwaka mmoja tukafanya mjadala  mgumu wa aina yake miaka mitatu iliyopita kuhusu maisha yetu.  Nilimwambia Marc kwamba yeye peke yake alikuwa hatoshi kumaliza hamu yangu ya mapenzi.

“Baada ya kukubaliana naye, nilianza kutafuta mpenzi mwingine kwenye mitandao na tukagunduana mimi na Andrea ambaye tulianza kukutana na hatimaye kufanya naye mapenzi.

“Nilikuwa na umri wa miaka 28 nilipokutana na Marc, hivyo wazo la kufanya mapenzi na mtu mmoja kwa miaka zaidi ya 40 ambayo ingefuata, lilinivuruga akili.  Ni kweli nilikuwa nampenda Marc lakini kimapenzi nilijiona kama nilikuwa peke yangu.  Matokeo yake nilimtambulisha Andrea kwa Marc akawa anakuja nyumbani na tunafurahi naye wote.

 “Muda si muda, Marc naye akawa na uhusiano wa wazi na wanawake wengine, akawa anaondoka kwenda kufurahi nao kwengine.  Mwanzoni nilijisikia vibaya kwani alikuwa amenionyesha wanawake hao.  Hata hivyo, sikuwa na la kufanya.

 “Sikutaka kuwaambia watoto wangu kilichokuwa kinatokea, kwani umri wao ulikuwa mdogo mno na wasingenielewa.  Tuliendelea hivyo kwa furaha hadi ikafikia mimi na Marc tukatengana na kila mtu akawa analala chumba chake kwenye nyumba ileile.  Hivi sasa tunasubiri kutengana kabisa ili niondoke na watoto.
“Tangu tutengane miezi 18 iliyopita, bado nampenda Marc na atakuwa nembo muhimu katika maisha yangu.. Ni vyema kuwa na maisha ya wazi, kuliko maisha ya kudanganyana kwa siri….”


 Wakifurahi bila ya chuki wala uchungu.

Naye Andrea anasema kabla ya kukutana na Anita alikuwa na mpenzi mwingine ambaye aliachana naye baada ya mwanamke huyo kukataa kuwa na uhuru wa kufanya mapenzi na watu wengine nje ya wao wawili.

 Hivyo,  alikazania kwa Anita ambaye walipendana na kushirikiana kila kitu likiwemo penzi kabla ya kukutanishwa na mumewe mwaka mmoja baadaye.  Mumewe alikubali kila kitu na watoto wakajua baba yao alikuwa Marc na Andrea alikuwa ‘boifrendi’ wa mama yao…



Hivi sasa Anita na Andrea wanasubiri kuendeleza penzi mara Marc na Anita watakapoachana rasmi.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA

from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3iMnIg0
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI