Watanzania Milioni 14.8 Hawajapiga Kura Uchaguzi Mkuu 2020



Matokeo ya urais yaliyotangazwa usiku Ijumaa Oktoba 30, 2020 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yanaonyesha kuwa Watanzania milioni 14.8 sawa na asilimia 49.8 hawakujitokeza kupiga kura.


 

Idadi hiyo ya watu milioni 14.8 ni kati ya Watanzania milioni 29.8 waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.


 


Uwiano huo wa watu ambao hawakujitokeza ni mkubwa ikilinganishwa na asilimia 33 ya ambao hawakujitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hata hivyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 waliojiandikisha kupiga kura walikuwa milioni 25.5.


 


NEC imemtangaza mgombea wa CCM, John Magufuli


kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kupata kura 12,516,252 sawa na asilimia 84.4 kati ya kura halali 14,830,195.


Kwa mujibu wa matokeo hayo mgombea wa Chadema, Tundu Lissu amekuwa mshindi wa pili baada ya kupata kura 1,933,271 na kufuatiwa na mgombea kupitia ACT- Wazalendo, Bernard Membe aliyepata kura 81,129 na Leopord Mahona wa NRA kura 80,787.


 


Matokeo hayo yametangazwa leo usiku jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Semistocles Kaijage aliyebainisha kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa 29,754,699 walioandikishwa katika daftari la kudumu la NEC na lile la Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).


 


“Idadi halisi ya waliopiga kura ni 15,091,950 na idadi ya kura halali ni 14,830,195. Kura zilizokataliwa ni 261,755.”


Nec inamtangaza Magufuli mgombea wa CCM kuwa rais wa Tanzania na Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu. Baada ya kumtangaza mshindi wa kiti cha urais sasa ni wakati muafaka kwa mawakala kusaini fomu,” amesema Kaijage.


 


Wagombea wengine na idadi ya kura walizopata katika mabano ni John Shibuda wa Ada Tadea (33,086), Muttamwega Mugaywa wa SAU (14,922), Cecilia Mwanga wa Demokrasia Makini (14,556), Yeremia Maganja wa NCCR-Mageuzi (19,969), Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF (72,885).


 


Philipo Fumbo DP (8,283), Queen Sendiga ADC (7,627), Twalib Kadege UPDP (6,194), Hashim Rungwe wa Chaumma (32,878), Khalfan Mohammed Mazrui wa UMD (3,721) na Seif Maalim Seif wa AAFP (4,635).



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3mF8qM8
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story