Alichokisema Mzee Msekwa kuhusu Spika Ndugai

  


Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kuwa hakuna ugumu wowote anaoweza kukutana nao Spika wa Bunge la 12, Job Ndugai, mara baada ya wabunge 19 wa CHADEMA, kufukuzwa uanachama kwa kuwa yeye ni kama daktari tu anayepokea wagonjwa kuwatibu kisha kuondoka.

 

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, kufuatia sakata la wabunge 19 wa viti maalum ambao wamefukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA baada ya kwenda kula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama, ambapo alisisitiza kuwa kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni basi hata ubunge wao umekoma.


"Spika Ndugai hapati ugumu wowote, hakupata ugumu walipoletwa hapati ugumu wowte wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, hana ugumu na wala hafaidiki na lolote ni kama mganga wa hospitali yeye anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka, wakifa wanaondoka yeye hana jukumu zaidi ya hilo", amesema Spika Mstaafu, Pius Msekwa.


Tazama video hapa chini



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2Jl9HtB
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI