Chege na Rosa Ree Waingia Studio Kupika Kitu....


Staa wa muziki nchini, msanii @chegechigunda, ameingia studio kurekodi wimbo na rapa @rosa_ree ambaye ni mmoja wa marapa wa kike tishio zaidi Afrika Mashariki na anayetafutwa zaidi kwa collabo.


Ikiwa tayari ni mwezi mmoja umetimia tangu @hegechigunda aachie ngoma yake "Top Shatta" ambayo kwa sasa inafanya vizuri kwenye chat mbalimbali za TV na radio nchini, ameposti kipande cha wimbo mpya ambao amemshirikisha #RosaRee, na huenda ukawa mbioni kuachiwa.


Ndani ya miezi hii mitatu ya karibuni, @rosa_ree tayari ameshirikishwa kwenye ngoma mbili za wasanii wazito ambao ni @bellachristian1 pamoja na @mrbluebyser1988.


#Chege aliyewahi kuvuma na Kundi la TMK Wanaume lililokuwa linamilikiwa na Said Fella, wiki hii naye amemnasa kwenye ngoma yake ijayo.


Huu ni muendelezo mzuri kwa rapa @rosa_ree kuendelea kufanya vizuri ambapo kwa hapa nyumbani, thamani yake inazidi kuongezeka kila kukicha.


#SNSEnt



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2HQzQ2E
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI