Kaze bado anatembelea kijiti cha Zlatko Yanga

 


Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Cedric Kaze ana kazi ya kufanya kutokana na kushindwa kupata ushindi wa kuridhisha katika michezo yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara tangu alipochukua mikoba kuinoa miamba hiyo.


Kaze alipata ushindi wa zaidi ya bao moja wakati kikosi chake kikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Baada ya mchezo huo, Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya Gwambina, ikalazimishwa suluhu na Gwambina kabla ya sare ya 1-1 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.


Kaze alishindwa tena kuibuka na ushindi dhidi ya Namungo FC akilazimishwa suluhu kabla ya kurudi katika ushindi alipoifumua Azam FC bao 1-0 na ushindi kama huo dhidi ya JKT Tanzania, Jumamosi.


Katika michezo miwili iliyopita, kocha huyo raia wa Burundi alibadilisha wachezaji wake watatu wa mbele, Michael Sarpong, Carlinhos na Farid Musa, ambao walikuwa wanaanza na badala yake kuwaanzisha Yacouba Sogne, Ditram Nchimbi na Deus Kaseke.


Uwepo wa wachezaji hao umemsaidia Kaze katika michezo miwili ya mwisho dhidi ya Azam FC na JKT Tanzania, wakati pasi ya Yacouba ikitumiwa vizuri na Kaseke katika mabao yote mawili ya mechi hizo zilizochezwa kwenye viwanja vya Azam Complex na Benjamin Mkapa.


ADVERTISEMENT

Kaze, ambaye hajapoteza mchezo hadi sasa, amevuna pointi 18 katika mechi nane alizoiongoza Yanga tangu alipowasili nchini kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotik.


Akizungumza mara baada ya mchezo wa juzi dhidi ya JKT Tanzania, Kaze alikirui kuumia kichwa juu ya safu yake ya ushambuliaji kushindwa kumaliza mechi mapema licha ya kuwa na nafasi nyingi za kufunga.


Kocha huyo alisema katika kipindi ambacho amekuwa nchini kwa ajili ya kuinoa miamba hiyo ya soka, amefanikiwa katika maeneo mengi licha ya kushindwa kubadilisha ufinyu wa mabao.


“Ni tatizo,” alianza kwa kusema Kaze mwenye miaka 40 sasa.


“Unapokuwa na mchezo mzuri unatakiwa kutengeneza nafasi, lakini kutengeneza nafasi ni usla jingine na kufunga ni jingine.


“Hadi sasa bado naumiza kichwa katika suala hili, nimefanikiwa katika kusuka timu kuanzia nyuma na sasa tumekuja katika ushambuliaji, lakini bado tunapata matokeo ya mabao machache katika michezo ambayo tunaweza kufunga zaidi,” alisema Kaze.


Alitolea mfano mchezo dhidi ya Simba, ambao anaamini ulikuwa wa wazi kwao kuibuka na ushindi kutokana na kufanya mashambulizi yenye hatari bila kutumika ipasavyo.


Kocha wa zamani wa Tanzania Prisons, Mohamed Adolph Rishard aliwahi kusema kuwa Yanga imebadilika kwa kiasi kikubwa chini ya Kaze, japo ana changamoto katika ufungaji.


Rishard alisema: “Ukiiangalia Yanga ya sasa ina uthubutu wa kuanzia nyuma kwa pasi, lakini kidogo bado haijakuwa bora katika kutumia nafasi zao wanazotengeneza.”



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3lnaB5V
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI