Msanii Harmonize Atupa Kijembe Kwa Wasanii wa Tanzania Waliokosa Kuwekwa Tuzo za Grammy

 

Msanii @harmonize_tz amedai kuwa tuzo za Grammy hazihitaji kelele nyingi ili kuteuliwa kuwania.

Kauli ya #Harmonize inakuja mara baada ya wasanii wachache wa Muziki nchini, ambao ni Diamond Platnumz, Rayvanny na Zuchu kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya kujadiliwa (Consideration) kwa ajili ya kuingia kuwania Tuzo za Grammy.


Hata hivyo wasanii hao hawakufanikiwa kuteuliwa kuwania. Maneno hayo ya #Harmonize yamepokelewa kwa hisia tofauti tofauti, ikielezwa kuwa huwenda ikawa ni kijembe kwa wakali hao.


Akizungumza hayo akitokea kwenye show yake ya Mtwara iliyofanyika wikiendi iliyomalizika, #KondeBoy ama #Jeshi kama anavyojiita kwa sasa, pia amesema, kwa mwaka huu amechaguliwa kuwania tuzo karibia zote isipokuwa Grammy pekee.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3qfoo1S
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI