Mwakinyo Abakiza Nyota 2 Kufikia Viwango vya Kina Manny Pacquiao, Agoma Kupigana na Twaha Kiduku



Bondia namba moja nchini, @hassan_mwakinyo_jr kupitia ukurasa wake wa #Twitter amejibu kuhusu kupigana na Bondia mwenzake Mtanzania, #TwahaKiduku.


Ikumbukwe kuwa kupitia viwango vilivyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia, boxrec Ijumaa iliyopita, #Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya 78 hadi ya 41 duniani kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa Super Welter na kuwa na nyota tatu.


Hivyo #Mwakinyo anahitaji kutafuta nyota nyingine mbili ili kuingia anga za mabondia wanaotamba duniani akiwamo #MannyPacquiao mwenye nyota tano.


Akijibu swali la Shabiki yake aliyemuuliza kuhusu kumkimbia Bondia Twaha Kiduku, #Mwakinyo alijibu, "Nimebakiza Nyota 2 Kufika Level za kina Manny Pacquiao so kupigana Na Kiduku sidhani kama nitapata izo 2 star zilizobaki Lets focus on internation Levels"



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3mu4VbI
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI