Polepole kula kiapo leo, Ndugai kuzingatia hili

 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo saa 10:00 jioni, atawaapisha wabunge wawili wa Bunge hilo walioteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli, mapema jana.

 

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Novemba 30, 2020, na ofisi ya Bunge, ambapo imeeleza kuwa wabunge watakaoapishwa hii leo ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole, na aliyekuwa mbunge wa viti maalum katika Bunge la 11 kupitia chama cha CUF, Riziki Lulida.


Spika Ndugai anawaapisha wabunge hao kwa kuzingatia kanuni za kudumu za Bunge inayoeleza kuwa endapo mbunge atachaguliwa au kuteuliwa kipindi ambacho hakuna mkutano wa Bunge unaoendelea, Spika atamwapisha katika eneo atakalolipanga yeye. 



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2VjrCDe
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI