Rais Venezuela amechapisha nambari yake ya simu nambari yake ya simu mtandaoni




Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, amechapisha nambari yake ya simu mtandaoni kupitia akaunti yake ya Twitter, na kusema "Nialikeni kwenye vikundi vyenu."
Maduro alirekodi video na kutoa ujumbe uliosema,

"Venezuela, ninashiriki katika vita vya maoni kwenye vikundi vya WhatsApp na Telegram kwa nambari 04262168871. Nijumuisheni kwenye vikundi vyenu vyote na tupambane pamoja kutetea Venezuela."

Katika nambari hiyo aliyoitoa, ilionekana kuwa na picha yake Rais Maduro iliyobeba maneno yanayosoma "Rais wa Venezuela" kwenye profile ya WhatsApp na Telegram.

Maduro pia alichapisha video za ujumbe aliotumiwa kwake kupitia akaunti kituo rasmi cha Telegram.  

Maduro alimalizia kusema, "Mapokezi yamekuwa makubwa sana, maelfu ya vikundi vimenijumuisha."




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/39vxiCs
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI