Roberto Carlos afunguka dili la kusaini Chelsea



Legendary, nyota wa Brazil, Roberto Carlos amezungumzia namna alivyokaribia kujiunga na klabu ya Chelsea kutoka nchini England mwaka 2007.



‘Icon’ huyo wa Brazil aliyeitumikia Real Madrid kwa mafanikio makubwa akicheza jumla ya michezo 527, makombe 13 akiwa na umri wa miaka 34 akitangaza kustaafu huku watu wengi walikuwa bado wakimuhitaji kwakuwa walikuwa wakiamini bado anacho kitu cha kufanya uwanjani.

Carlos amesema alikuwa katika nafasi ya mwisho kujiunga na Chelsea chini ya mipango ya kocha wake kwa wakati huo Jose Mourinho.

Roberto Carlos: What stopped me from Joining Chelsea | TrueNEWS Sports

Kwa wakati huo Kocha huyo raia wa Ureno alikuwa tayari na Ashley Cole, ambaye amekuwa anamhakikishia matokeo mazuri kunako uwanja na beki huyo wa kushoto Carlos akiwa bora kweli kweli duniani

Kwa sasa Carlos ana umri wa miaka 47, wakati ambao anagusia namna alivyonukia kutua Blues. Akiiambia Goal mchezaji huyo aliyekuwa katika ubora wa dunia amesema “Nilikuwa na mapendekezo kutoka klabu mbili, Fenerbahce na Chelsea. Chelsea haikufanya kazi hivyo nikasaini Fenerbahce.”

“Lakini nilikaribia sana kujiunga na Chelsea. Nilibidi niende huko hivyo nikaamua kusaini. Ilikuwa ni wiki moja tu kabla ya kusaini Fenerbahce na nilikuwa Paris nilikwenda kukutana na Roman Abramovich na Peter Kenyon.




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2Jn2iJY
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI