YUPI Anayefaa, Tajiri ila Hana Muda na Mimi au Mwenye Uwezo wa Kawaida ila yupo Nami Muda Wote

Kama kichwa cha Habari kinavyojielezea mimi ni binti mrembo tu Nina kaxi yangu nzuri Namshukuru Mungu, nimepita kwenye mahusiano kadhaa changamoto hazikosekani Nimekutana na wenye uwezo wanaoweza kanipa Nitakacho na wenye uwezo wa kawaida tu.

Nilichojifunza ni kwamba Unaweza kuwa kwenye mahusiano na mtu Anaejiweza akakupa kila utakacho ila hana muda na wewe hamna out wala muda wa kukaa mkayajenga hata mazungumzo ya kawaida maana mimi ni mpambanaji

Mkikutana ni show basi siku zinaenda mwaka umekatika hamna la maana na sio kwamba anamahusiano mengine Hapana ingawa Mwanaume huwezi msemea ila ni mtu ambaye uko nae huru ila yuko busy muda wote hawezi kujenga muda kwa ajili yako ila muda wa kufanya mengine kama kwenda Bar, karaoke nk anao

Pili Mwanaume Ambae hawezi kukuhudumia kwa chochote mnapata muda wa kuzungumza kushauriana kupanga Mambo ya maendeleo ingawa hamuwezi kwenda out nk kutokana na kipato ila mapenzi mnayafurahia hata kwa kukaa ndani tu coz mimi sio mtokaji na haijawahi kunipa chochote wala sijawahi kumuomba coz namjua Hali yake

Ingawa ana wasiwasi na mimi kutokana na uwezo wake na urembo wangu ila mimi sina tatizo coz najimudu kwa kila kitu. sasa huyo mwenye uwezo miezi4 hatuko vizuri na naona nimeshindwa mimi kwa moyo mweupe coz sijawahi kuenjoy nae hata siku moja nataka kumpokea huyu wa Hali ya kawaida kwa moyo mmoja tujenge familia maana kule naona utumwa naombeni Ushauri ndugu zangu

By Vantz

from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/31A9SYu
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI