Ajibu, Sheva Waugomea Uongozi Simba




JUMLA ya wachezaji watano wa Simba wamegoma kutolewa kwa mkopo kwenda kucheza katika klabu nyingine zilizoomba barua za kuwahitaji nyota hao katika usajili huu wa dirisha dogo.

 

Wachezaji wanaotajwa kutolewa kwa mkopo ni Kennedy Juma, Miraji Athumani ‘Sheva’, Charles Ilanfya, Ibrahim Ame na Ibrahim Ajibu ambao wamekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

 

Simba imepanga kuwatoa wachezaji hao kwa mkopo baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Sven Vandenbroeck, kupendekeza nyota hao kutolewa ili wakalinde vipaji vyao baada ya kukosa nafasi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, wachezaji hao wamegoma kutolewa kwa mkopo kwa

kuhofia kutelekezwa na timu hiyo.Mtoa taarifa huyo aliwataja baadhi ya wachezaji waliogoma kutolewa kwa mkopo ni Kennedy, Ajibu, Sheva huku Ame akionekana kuwatega viongozi wengine wakipendekeza abakie hapo.



Aliongeza kuwa wachezaji waliobakishwa wakiwa katika hatua za mwisho za kutaka kutolewa kwa mkopo ni kiungo Francis Kahata na David Kameta ‘Duchu’ ambao wataendelea kubaki baada ya uongozi kufurahishwa na viwango vyao katika mchezo ya juzi wa Kombe la FA dhidi ya Majimaji FC.“

 

Simba imepanga kuwatoa wachezaji watano kwa mkopo katika dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka huu ambao wote hao wamegoma kuondoka hadi mikataba yao itakapomalizika.

 

“Kati ya hao waligoma kuondoka kwa kuhofia kutelekezwa na viongozi wa timu hiyo, kwani mara wanapowatoa kwa mkopo ndiyo kama wamewaacha jumla, hivyo hawataki kusikia, ni bora wakaendelea kukaa hapo Simba,” alisema mtoa taarifa huyo.

Stori na Wilbert Molandi,

 



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3hxgqx9
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI