Fahamu Kwa Undani Aliyoyaacha Mama Rwakatare

 


Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God,  Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare, alifariki dunia Alfajiri ya Aprili 20, 2020, katika hospitali ya Rabininsia iliyopo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua maradhi ya moyo.


Taarifa ya kifo cha Mama Rwakatare ilitolewa mapema na mwanaye wa kiume Mutta Rwakatare, alipozungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, taarifa ambayo baadaye pia ilitolewa na Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.


Mama Rwakatare alizaliwa Desemba 31, 1950, huko Ifakara mkoani Morogoro, na alisoma Shule ya Msingi Ifakara, akajiunga na Sekondari ya Korogwe hadi kidato cha sita na baadaye alijiunga na Chuo cha North London Polytechnic nchini Uingereza na baadaye pia alijiunga na Chuo cha Eastern and Southern Africa Management Institute alikopata shahada ya kwanza ya mawasiliano ya umma.


Aidha marehemu Mama Rwakatare pia alijiunga na chuo kikuu cha kikristo cha Moody, na safari yake ya kielimu haikuishia hapo, aliendelea hadi kufikia hatua ya udaktari wa falsafa (Philosophy Doctorate- PhD).


Marehemu Mama Rwakatare pia atakumbukwa kwa maneno yake kutoka katika vitabu vitakatifu, ikiwemo upepo wa kisulisuli ambao kwa imani yake alikuwa akiwaombea mabinti ambao hawajaolewa kwamba waume zao watakuja kwa kupeperushwa na upepo huo.


Marehemu Mama Rwakatare pia alikuwa akisifika kwa makongamano na mafundisho ya ndoa, ujasiriamali, malezi pamoja na mafundisho ya Biblia.


Marehemu Mama Rwakatare ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliofanikiwa kujenga majumba ya kifahari jijini Dar es Salaam, yaliyopo Mikocheni B, na nyingine ikiwa ufukweni mwa Bahari ya Hindi huko Mbezi.


Mbali na hayo marehemu Mama Rwakatare, pia alikuwa ni mmiliki wa kituo cha Redio cha Praise Power, shule na vyuo vya St. Mary’s kwenye mikoa mbalimbali chini, vitu ambavyo bado vinaendelea hadi sasa.


Ikumbukwe kuwa marehemu Mama Rwakatare aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Mvomero, kuanzia mwaka 2008 hadi 2015, na baadaye aliteuliwa na Rais Dkt. Jakaya Kikwete kuwa mbunge.


Askofu Dkt. Getrude Rwakatare,  alizikwa  Alhamisi ya Aprili 23, 2020, katika viunga vya kanisa lake lililopo Mikocheni B, jijini Dar es Salaam



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/381i5YH
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI