Maskini Diamond Platnumz Afunguka HAYA Kuhusu Wasanii Wanaomwimba Vibaya

 


Nyota wa muziki nchini na bara la Afrika kwa ujumla, msanii Nasib Abdul @diamondplatnumz amesema hawezi kukasirika anaposikia wasanii wengine wanamuimba katika nyimbo zao kwa mabaya au mazuri.


Akizungumza na Wasafi TV, #Diamond amesema hilo linatokana na nguvu kubwa ya ushawishi aliopewa na Mungu hivyo hawezi kuchukia.


“Ni baraka namshukuru Mwenyenzi Mungu, hutakiwi kuchukia, Mungu amenipa nguvu kubwa ya ushawishi, kwa hiyo sitakiwi kununa. Wao ni binadamu wanatafuta riziki kupitia mimi, sasa nikinunua nakuwa namkasirikia kwanini kanipa huu ukubwa,” amesema.


Ameendelea kusema kuwa kuna wasanii wengi wapo mtaani wangetamani kupata nafasi hiyo lakini wameikosa, hata ile ya kuzungumziwa.


Kwa sasa nyota huyo, ambaye pia ni boss wa lebo ya @wcb_wasafi anafanya vizuri na wimbo wake "Waah" ambao amemshirikisha Koffi Olomide kutokea DR Congo.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2MnOpgb
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI