MO Dewji atoa ya moyoni “sitamvumilia anenivunjia heshima”



Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema mwaka 2021 hatowavumilia wale wote wanaotoa lugha za matusi na kumvunjia heshima.
MO ametoa onyo hilo jana kupitia ujumbe wake mrefu wa kufunga mwaka 2020 aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

“Azimio langu kwa mwaka ujao humu mtandaoni ni kutovumilia wale wenye lugha za matusi na kunivunjia heshima mimi binafsi, nitalazimika, japo kwa shingo upande na moyo mzito sana, kuwa-block, ku-report na ikibidi, kuchukua hatua za kisheria. Naamini kutumia lugha ya matusi na kudhalilisha dhidi ya mtu katika hadhara si ustaarabu wetu Watanzania, si maadili ya dini zetu na si uungwana pia” MO dewji

“Sote tuna maisha nje ya mtandaoni. Wengi wetu ni wazazi, tunao pia wazazi, wategemezi na watu wengine muhimu kwetu ambao tunawaheshimu, wanatuheshimu na wana matarajio juu yetu, haipendezi kuwakwaza na kuwaumiza hao wanaotuthamini na kutuheshimu kwa figisu za maisha yetu ya mtandaoni” MO Dewji 

“Nachukua fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza mtandaoni katika mwaka huu unaoishia. Nami nimesamehe wale wote ambao walinikwanza kwa namna moja au nyingine,” MO

Kuhusu Klabu ya Simba, Mo amesema; “Tunapomaliza mwaka, nawashukuru wote humu mtandaoni kwa kunikosoa, kunijenga na kunishauri mengi mimi binafsi na klabu yetu ya




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/391znED
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI