Ramaphosa Aja na Masharti Mapya Kudhibiti Corona




RAISwa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa, amesema hali ya maambukizi nchini humo ni mbaya sana, hivyo serikali ya nchi hiyo imerejesha masharti mbalimbali yanayolenga kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona katika ambayo imeathirika zaidi barani Afrika.

 

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tangu nchi hiyo itangazwe kuwa nchi ya kwanza Afrika kufikisha visa 1,004,413 huku 26,735 wakipoteza maisha tangu kutangazwa kwa mlipuko wa virusi hivyo Machi, 2020.

 

Masharti yaliyotolewa ni pamoja na wananchi kutotoka nje kuanzia saa 3:00 usiku hadi saa 12:00 asubuhi bila kibali.  Mauzo ya pombe pia yamezuiwa, ambapo migahawa na maduka yatafungwa saa 2:00 usiku.

 

Pia watu wote wametakiwa kuvaa barakoa kila wanapokuwa katika maeneo ya umma na watakaokiuka agizo hilo watatozwa faini au kufungwa jela.

 

Hivi karibuni mamlaka nchini humo zilitangaza kuwepo kwa virusi vipya vya corona vinavyosambaa kwa haraka, hali iliyopelekea hospitali kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa.

 



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/34UfHBb
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI