Ridhiwani Kikwete Ampa Shavu Harmonize, Ataja Wimbo wa Jeshi Ndio Wimbo Wake Pendwa



Tumebakiza siku chache tuumalize mwaka 2020 na tuingie 2021, kama ilivyo kwa Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama ambaye hutoa orodha ya ngoma kali zaidi kwake kila mwaka kuelekea mwisho wa mwaka, sasa Mbunge wa jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete yeye anaitaja #Jeshi ya @harmonize_tz kama wimbo wake pendwa mwaka 2020.


Wimbo Jeshi (Video) ambao unafanya vizuri YouTube, tangu video hiyo ipandishwe Agosti 11 mwaka huu, umemkosha vilivyo Mh. Ridhiwani 2020.


Kupitia Instagram, Mh. @ridhiwani_kikwete amepost video ya wimbo wa "Jeshi" na kuandika, "Kuna nyimbo zinakuwa na hisia fulani hata unapokuwa unaoga unasikia inaimba kichwani. That Number toka kwa Konde Boy inakuwa katika list ya Nyimbo hizo".


Mheshimiwa #Ridhiwani anaungana na maelfu ya mashabiki mtaani kuipokea Jeshi kama wimbo bora



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2WWZ4Az
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI