Ujerumani yarekodi vifo 1,129 vya COVID-19 ndani ya saa 24




Ujerumani imerekodi vifo 1,129 kutokana na virusi vya corona ndani ya saa 24 zilizopita.Idadi hiyo ya juu zaidi kuwahi kurekodiwa Ujerumani ni kwa mujibu wa takwimu kutoka katika taasisi ya kupambana na magonjwa ya kuambukiza ya Ujerumani Robert Koch mapema leo.
Aidha kwa mujibu wa data za Robert Koch, jumla ya maambukizi mapya 22,459 pia yamerekodiwaKatika wiki za hivi karibuni, Ujerumani imeimarisha vikwazo vya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, ikiwa ni pamoja na kufunga maduka na shule, kuhimiza watu kuvaa barakoa, kutosogeleana na kuepusha mikusanyiko ya watu.

Uingereza pia imerekodi idadi ya juu zaidi ya maambukizi ya virusi hivyo. Serikali ya nchi hiyo imetangaza kuwa jumla ya maambukizi 53,135 mapya yamerekodiwa ndani ya saa 24 zilizopita.Hayo yakijiri, Uingereza imetangaza kuidhinisha matumizi ya chanjo ya pili ya COVID-19, iliyotengenezwa na kampuni ya nchi hiyo AstraZeneca kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Oxford.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2KMkQEw
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI